Mkandara nimeleta mambo haya kwa ajili ya kuleta mwanga zaidi maana watu wengi wanaangalia kwa mwanga wa 'sisi vs them' hivyo hawataki hata kuangalia ule upande wa pili hoja. Kwa kiasi kikubwa inachangiwa na serikali yenyewe kuficha mambo ya msingi. Fikiria kwa mfano ikija kuwekwa hadharani kuwa hata baadhi ya hospitali za Waislamu zinapokea fedha kutoka serikalini - kwa ajili ya madara, ajira n.k - je watu wanaopinga hospilitali za kanisa kupatiwa watasimama na kusema na misikiti isipewe?
Lakini jambo la pili ambalo nalo ni kubwa ambalo unakutana nalo hata kwenye nchi kama Marekani ambazo zinazo hicho cha "separation of church and state" ni kuwa hata taasisi za makanisa na za kidini zinapata fedha kutoka serikalini (federal au state) kwa masharti kwa mfano haziwezi kuwa na ubaguzi katika huduma au ajira either under civil rights act ya 1964 au Title IX. Hili ndilo ambalo limekuwa likitokea nchini hata kabla ya wakati wa ukoloni na of course hospitali za wamisheni kwenye utawala wa kikoloni ni wazi zilikuwa na advantage zaidi kuliko hospitlai na shule nyingine.
Lakini kubwa ni hili kwa mfano - hospitali za Ndanda, Peramiho na cliniki zao mbalimbali zinaweza vipi kulipa watumishi waende kufanya kazi mazingira ambayo tayari watu wanayakimbia? Lakini kama mtumishi wa Ndanda Hospital au Peramiho Hospital ameajiriwa na serikali kuu na mshahara na posho zake zinatoka serikali kuu - na haijalishi dini yake mtu huyo - je endapo serikali ikijitoa kwenye mishahara yake na kanisa likashindwa kumlipa ni nani anayelipa hilo kama siyo wagonjwa wa maeneo hayo?
Nadhani tatizo ambalo tunalo na ambalo linaweza kuondolewa ni kukaa pamoja na taasisi mbalimbali ili kutengeneza sera ambayo itasimamia mahusiano ya serikali na taasisi za kidni na zile zisizo za kidini. Kuna watu wanafikiria kuwa serikali inaweza kuendesha mashule na hospitali zote ukweli haiwezekani. Kwa kadiri nijuavyo sidhani kama kuna nchi yeyote ambayo serikali inatoa huduma zote mbili bila kusaidiwa au kusaidia taasisi binafsi. Karibu kiila nchi ina mfumo wake wa ushirikiano huu.
Maswali ambayo sisi kama Watanzania jwa pamoja tunahitaji kujiuliza ni:
a. Taasisi za kidini zinaweza vipi kupewa misaada au kuwekewa mazingira ya kufanya kazi zake vizuri katika nchi ambayo bado ina matatizo ya umaskini, maradhi na ujinga? Kwa mfano - tukisema taasisi zote za kidini ziwe kama za kibiashara zilipe kodi katika huduma yake na bei ya vifaa na madawa ni zile zile zinazouzwa madukani je ni taasisi gani zitaweza kusimama?
b. Je sasa hivi mfumo unaotumika una mapungufu gani na ni jinsi gani mapungufu hayo yanaweza kuboreshwa. Kwa sababu kwamba makanisa na taasisi za Kikristu ni nyingi zaidi halina shaka lakini suluhisho ni nini? Wengine wanasema fedha zote ambazo zinatolewa kusaidia taasisi hizi ziondolewe mara moja. Well hiyo ni rahisi lakini matokeo yake ni nini mara moja? Fikiria kwa mfano, serikali inasema kuanzia kesho hakuna hospitali ya kidini ambayo itapewa fedha kutoka serikalini kwa shughuli yoyote na fedha zote zitapelekwa mahospitali ya serikali je hiyo kesho kutakuwa nini kwenye mahospitali ya Bugando, KCMC, Peramiho, Ndanda n.k Nini kitakuwa kwenye zile jamii ambazo hospitali hizo zipo? Nini kitatokea kwa wale wagonjwa Waislamu na Wakristu na Wapagani ambao wanazitegemea hospitali hizo? Wale wanaosema serikali ikatishe ni vizuri watoe pendekezo zuri la jinsi gani serikali iondoe hiyo ruzuku bila kuathiri huduma kwenye mahospitali hayo. Kusema kwamba "makanisa yatatafuta misaada kwingine" is not an option.
c. Upande mwingine ambao watu hawaangalii ni kuwa je hizi hospitali zinahudumia walipa kodi wote kwenye maeneo hayo? Je kuna Waislamu wanaotibiwa Bugando, KCMC, Ndanda au Peramiho? au kwenye kliniki zaidi ya 450 za makanisa? Je hawa Waislamu wanalipa kodi? Kama wanalipa kodi na fedha za kodi zao zikirudishwa kwenye mahospitali ambayo wao wanapata huduma tunaweza kusema kuwa kodi yao imetumika vibaya? Je WAislamu ambao wameshatibiwa huko na watoto wamezaliwa huko kwenye mahospitali ya misheni na Waislamu ambao wameajiriwa katika mahospitali hayo wanaweza kusema kweli kuwa serikali isitoe fedha kwenye taasisi hizo kwa sababu ni taasisi za makanisa? Binafsi ningependa kuona watu wa maeneo ya hospitali hizo waulizwe hata kwa kupiga kura kama wanataka kodi zao ziingizwe kwenye hospitali hizo tuone kama watataka zisitishwe.
MMM
Mkuu wangu nimekuelewa sana na nipo na wewe kabisa...
Tatizo la ruzuku hizi sii swala la Kanisa linahudumia watu gani bali lipo ktk makosa ya kikatiba na morally wrong kiasi kwamba serikali ndio inakuwa ikiendesha Ubaguzi kama ule wa Apartheid. Ebu fikiria tu kwa njia nyingineyo, serikali iwe inawapa wahindi ruzuku ili waendeshe biashara za maduka yao na sii watu weusi. Ukiuliza unaambiwa jiulize wahindi wanatoa huduma kwa wananchi wangapi na wa aina gani? wahindi wanajua sehemu za kufuata mali, wazuri ktk biashara, wanatoa ajira na kadhalika...Yaani sababu ambazo hazihusiani kujibu swali kwa nini weusi HAWAKUPEWA nafasi hiyo kikatiba toka mwanzo...majibu rahisi na ya kihuni hutolewa - Nanyi ombeni mtapewa! wakati ahadi hii haipo kikatiba wala hakuna memorandum.
Hii tayari inawafanya watu weusi second class citizen na hakuna mantiki yoyote kufikiria huduma zinazotolewa na wahindi hata iwe kwa ubora gani... Ndivyo ilivyokuwa South Afrika makaburu wakizungumza kuhusu uwezo wao wa kutoa huduma safi kwa wananchi wote ili hali wazungu ndio waliofanikiwa zaidi ya watu weusi..Na mara zote walijenga hofu ya kwamba wakiondoka wao watu weusi wenye shida nani atawahudumia..
Kwa hiyo hakuna sababu ya kutazama kanisa linawasaidia vipi wananchi wakati kazi hiyo ilitakiwa kuwa ya serikali toka mwanzo na makosa yamefanyika kupendelea upande mmoja na kuweka mkataba. Hii inabadilisha sura nzima ya sera za kitaifa kwa kujumuisha kanisa kuwa sehemu ya serikali na utoaji huduma. Kwa hiyo ugonvi uliopo wa 'US against THEM' umetokana na mkataba huu ambao kwa waislaam wanaona wamebaguliwa kikatiba. Na hakika katiba inapoandikwa huwa ni kwa taasisi zote za aina hiyo zinafungwa na sera kama hii ya MoU na sii kuchagua kundi moja kati ya makundi mengi.. Kwa kutofanya hivyo serikali imefanya ubaguzi na kosa kubwa ambalo Mdondoaji kila siku husema waislaam ni second class citizen..
Mfano wa Marekani hauwezi kujenga hoja Tanzania kwa sababu America was found under Christian values na ndio maana tunasema ukienda Amerika itakubidi uishi kama Waamerika. Hivyo taasisi za dini zilikuwepo toka kujengwa kwa taifa lao, lakini Je, iliwasaidia vipi wenyeji na wakazi wa nchi hiyo Wahindi wekundu ambao kimsingi elimu ilikuwa ikitolewa kwa raia wote! Kwa hiyo tatizo la elimu ya makanisa Marekani ilikuwa kinyume cha wahindi wekundu kwa sababu elimu ilikwenda sambamba na mfumo wa kiutawala...
Sisi Tanzania ambao watu na mazingira yetu ni tofauti kabisa na Marekani hatutakiwi kuiga lolote kutoka ktk mfumo wa Marekani ama nchi yeyote ile isipokuwa tunatazama mfumo bora kwa watu na mazingira yetu kama Azimio la Arusha lilivyoasisiwa na mwalimu Nyerere kwamba shule zote za dini zinazotoa elimu dunia zilichukuliwa na kuwa mikononi mwa serikali isipokuwa zile zinazotoa elimu ya dini..Na Kama kuna taasisi yoyote inafungua shule ya private ifungue lakini hawatapewa ruzuku wala nafuu yoyote ya kodi kwa sababu hiyo ni biashara...Kwa hiyo kunakuwa na ushindani baina ya shule za Private na zile za serikali wakikaa mtihani mmoja darasa la saba kuingia form one, form IV kuingia form V, VI kwenda Chuo kikuu na kadhalika merits zilihitajika kuvuka sehemu moja kwenda nyingine bila kujali uko shule gani..
Kwa hiyo hayo maswala Ndanda, Pehaminho, Bugando, KCMC kote huko kumefanyika makosa na kibaya zaidi ni kwamba vyombo hivi serikali haikushidnwa kuviendesha laa hasha. Ni uhuni umefanyika na toka vyombo hivi viondolewe serikalini elimu nchini imeshuka vibaya sana...Yes, yawezekana elimu bora inapatikana ktk shule za makanisa lakini sii hivi ndivyo ilivyokuwa toka wakakti wa mkoloni? Sii hivi ndivyo ilivyokuwa hata huko South Afrika kwa Makaburu yaani shule za wale Elites ndizo hutoa huduma bora zaidi lakini hakuna haki wala usawa na mwisho wa yote hujenga matabaka baina ya wananchi...
Kwa hiyo mkuu wangu, hali ya Wananchi kielemu ndio inatakiwa ku determine mafanikio ya mfumo huu ulotokana na mkataba wa MoU, na sio kutazama mkataba wenyewe unasaidia watu wangapi...it's morally wrong hakuna sababu ya kutafuta sababu nje ili kupamba makosa yalofanywa na Mwinyi.. Kosa ni kosa, athari za upendeleo wa kutoa ruzuku ndio uloleta mjadala mkubwa na pengine hata kusababisha chuki baina ya waislaam na Wakristu, haijalishi shule hizi zinawafaidisha wangapi.. Ghadaff kaondolewa kwa sababu ya demokrasia tu, watu hawakujali mambo yote alowafanyia isipokuwa ushenzi aloufanya ndio sababu ilomhukumu. Na siku zote mazuri ni sehemu ya wajibu wa binadamu ktk maisha, isipokuwa mabaya ndio mtu huipelekwa mahakamani na akafungwa hata kama ni kosa la kwanza na kafanya mazuri millioni.