Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini


Mkandara unjua hizi lugha za kigeni somtime inaniacha njia panda na kwenye mataaa. Sasa labda nifafanuliwe hii sentesi hapa chini ina maana gani in relation to Mou

.....In order for the memorandum to take effect the government had to ammend article 30 of the Education Act No. 25 of 1978."

Naomba kujulishwa

  • Je mpaka Sasa education act ya mwaka I978 imesimama na ndiyo inatumika kwenye masuala ya elimu (wich means among the things serikali inaweza kutaifisha shule yeyote, etc )
  • Kama hiyo act ilikuwa ammended for favor of church ilikuwa ammended ni kwa kifungu gani na kwa sheria ipi ya mwaka gani?

Maana Tusidanganye kuwa Hii Mou ndio katiba. Hii sheria aliyo refer Mdondoaji ilikuwa ammended kama zilivyokuwa ammended sheria za biashara, usafiri , huduma, ect as a pressure of IMF to Tanzania
Nadhani inawezekana hata act hiyo ya elimu ilikuwa ammended hata kabla ya Mou.
 

Hicho kipengele kinaweza kuhusu shule za Kiislamu vile vile au zinazomilikiwa na Waislamu?
 
Hicho kipengele kinaweza kuhusu shule za Kiislamu vile vile au zinazomilikiwa na Waislamu?

It seems so kama wanapata financial grant from the government yes. Swali linakuja je kuna MoU ya serikali na waislamu? Na wanalipwa bei gani? Mwanakijiji nimekuomba unipatie kiasi gani Aga Khan wanalipwa na serikali hadi leo hujanipatia.
 
hakuna kukimbia
Haya taja shule moja ya Kanisa inayopokea grants kwa kuwa ni shule ya kanisa au kwa kuwa kuna Mou lakini shule nyingine hazipokei .

Kifupi Shule nazojua mimi zinzopkea Grannt ni zile za

  • Jumuiya za CCM kama shule za wazazi. tena nyingine imebidi wazirudishe serialini wenyewe sababu wmeshidnwa kuziendesha kwa faida na hapo hapo hapo wanafunzi kufaulu.
  • Pia kuna shule kama za vyama vya ushirika
 

Zing,

Sheria unayotumika sasa Education Act of 1995 ambayo imefanyia amendment Education Act of 1978. Usiseme uongo. Sasa hivi inajulikana kama Education Act Cap 353. Hakuna kutaifisha tena mashule ya binafsi. Sijaona point yeyote hapa.
 
 

Waulize wanaopokea Bilioni 91 kila mwaka za nini? Maana ile MoU inasema the government shall provide financial assistance to the church institutions.
 

Nyambala,

Act yeyote inayofanyiwa amendment lazima katiba ihusishwe. Katiba ndio sheria mama ya nchi na hivyo kama katiba inakinzana na sheria ya nchi basi walioandika Memorandum of Understanding wanaweza kuwa hatiani. Kasome jinsi sheria zinavyofanya kazi nchini hakuna sheria inayotungwa nchi hii bila ya kuihusishwa katiba kawaulize wanasheria watakuambia.
 
Wakuu bila numbers tunakuwa tunajadili huu mjadala kama mazuzu. Kwa nnavyofahamu mimi shule zote zenye mchepuo wa dini haziqualify financial assistance kutoka serikalini. Mfano ni seminari za kufundishia upadri. Ok nimeattach hapa kwa mara ya pili shule zote binafsi zilizokuwepo Tanzania by 2005 (At least that's all I could get). Sasa basi aje mtu atuambie huo mgawanyo fedha kwa mujibu wa MoU uko vipi hapo. Lakini busara binafsi na mihemko tutaishia kukejeliana tu. Numbers should be brought forward. Na hiyo itatusaidia kuwa more specific na kutafuta solution unless kama nia ya mjadala ni kupiga soga tu!
 

Attachments

It seems so kama wanapata financial grant from the government yes. Swali linakuja je kuna MoU ya serikali na waislamu? Na wanalipwa bei gani? Mwanakijiji nimekuomba unipatie kiasi gani Aga Khan wanalipwa na serikali hadi leo hujanipatia.

Well sijui hiyo lakini unaposema "wanalipwa" ina maana nyingi. Aga Khan wako tax exempt as an NGO na wana diplomatic immunity sijui vina thamani gani. Lakini pia ni swali zuri ambalo watu wanaweza kulifanyia utafiti. MoU ya Waislamu na Serikali kwa uelewa wangu wa kipengele hicho inaa maana inawezekana. Swali ni kwanini tangu 1992:

a. Kwanini Constitutionality ya MoU haijawahi kuhojiwa mahakamani na kundi lolote uhalali wake ili kufutwa?
b. Kwanini taasisi za Kiislamu hazijawahi kutengeneza MoU kama hii ili kusaidia hospitali na shule wanazoendesha?
c. Kwanini - kama kweli watu hawataki serikali isaidie taasisi zakidini - hawajapinga misaada ya serikali kwa taasisi za Kiislamu vile vile?
d. Je unachotaka ni kuwa serikali iache kutoa ruzuku kwa hospitali za Kanisa? na ifanye hivyo vipi bila kusababisha matatizo katika utoaji wa huduma huko?
 

Mwanakijiji.

Tax exemption and financial grant are two different things. Sijui unataka tujadili kipi kwasababu hata taasisi za kanisa zinapata tax exemptions. Bilioni 91 ni financial assistance by the government to the church institutions. Sasa nataka unifahamishe je serikali ya Tanzania inatoa katika government coffins any financial assistance to Aga Khan institutions? Sijibu maswali yako mengine hadi hujibu langu kwanza maana ni muda nakuuliza hujibu.
 
Zing,

Sheria unayotumika sasa Education Act of 1995 ambayo imefanyia amendment Education Act of 1978. Usiseme uongo. Sasa hivi inajulikana kama Education Act Cap 353. Hakuna kutaifisha tena mashule ya binafsi. Sijaona point yeyote hapa.

sijakuelewa Mdodondaji
  • Ina ana hujaona kasosro au kitu kibaya au kizuri kwa msikiti au kanisa kweye hiyo ammendment ?
  • au tumuulize Mohme said uliyemnukuu atumbie ni kifungu gani hasa?
What is wrong specificaaly kwenye ammendmendt kilicho favour kanisa pekee.?
 

1. Ni hospitali za Teule za wilaya kama Sengerema, Huruma-Rombo, Namanyere-Nkansi n.k (serikali ilianzisha wilaya mpya lakini haikuwa na hospitali ya serikali kwenye maeneo hayo) , na za rufaa KCMC na Bugando ndio zinapata fedha toka serikalini. Fedha zenyewe zinakuwa kwenye bajeti ya wizara ya afya. Kuna fungu maalum kwa ajili ya Hospitali za rufaa. Pia kila wilaya inatengewa fedha zake za huduma za afya. Pale ambapo hospitali teule ya wilaya inamilikiwa na kanisa ndipo tu ambapo fedha hizo zinaenda. Mganga mkuu wa wilaya anaripoti wizarani, na mahesabu yanakaguliwa. Serikali ikiacha kutoa fedha hizo kwenye hospitali teule kwa kuwa haizimiliki itakuwa imezitenga wilaya hizo kwenye huduma za afya. Labda hapa serikali ijipange kujenga hospitali zake ijitosheleze na iache mtindo huo wa Designated District Hospitals. Hata hivyo hilo kutekelezeka itachukua muda sana

2. Hospitali nyingine zote za kanisa zisizokuwa Hospitali teule za wilaya wala za rufaa hazipati fedha yoyote toka serikalini.

3. Hakuna shule yoyote ya kanisa inayopokea msaada wowote toka serikalini.

4. Hata kabla ya kusaini MOU mwaka 1992 serikali ilikuwa ikitoa fedha hizo kwa hospitali teule za wilaya na hospitali za rufaa na hakikubadilika kitu chochote.

Kama una ushahidi vinginevyo unakaribishwa.
 
 

Ni hivi Zing,

Kama MoU imeanzishwa hali ya kwamba sheria ya 1978 inasema vile basi ujue kwamba waliosign MoU wangelikuwa hatiani. Lakini kama umesoma amendments za 1995 zimewatoa katika matatizo kwa vile sheria imeruhusu kuwepo na shule au taasisi za elimu zinazopewa misaada. Ndio hapo Mohamed Said akasema hilo suala la MoU lisingeliweza kukamilika pasina kufanyika marekebisho ya sheria mbali mbali. Therefore, he was right to say that labda watuambie akina Lowassa walikuwa na malengo gani hasa wakati wanasign MoU ile?

Umeniuliza kuna ubaya gani okay ngoja nikuambie ubaya wake:-
a. Financial assistance means taasisi zote zisizokuwa za kiserikali zinaweza zikapata misaada hiyo. Sasa tunarudi katika MoU ya akina sheikh Ponda je hadi leo inafanyiwa tafakari ya nini? (Maana Topical anasema bado serikali imeikalia katika kiti inaitafakari). Mbaya zaidi akina sheikh Ponda according to Mohamed Said walikuwa wa kwanza kupeleka maombi kabla ya TEC na CCT je what is taking them long. Utaona something smelly is going on.

b. Kwanini serikali itoe aid kwa non-governmental organisations? Religious institutions are controversial kwasababu zinagusa imani za watu. Serikali ilitakiwa iseme inaanzisha community schools. Serikali itakuwa inasaidia kulipa mishahara, gharama za uendeshaji. Hivyo shule zote za private na serikali zibadilishwe na kuwa community schools ambapo serikali igharamie kwa pamoja. Religious institutions wakianzisha shule zao za faith based wawe wanapewa option kama wanataka iwe secular basi wasaidiwe kama wanataka iwe religious basi wajifadhili wenyewe.

c. Serikali ijitoe kusaidia hospitali za kidini kwani this is controversial issue. Badala yake wajenge hospitali za serikali na ziwe za rufaa tu. Hospitali zengine ziwe private owned na watu au taasisi za kidini zijifadhili zenyewe. Serikali iwe inasaidia kuwafadhili WAGONJWA NA SIO HOSPITALI!!!! Hili litaondoa upendeleo uliopo katika mahospitali ya kanisa. Hospitali za kanisa au za private zijitegemee zenyewe bila ya msaada wa serikali. Badala yake serikali ijikite kuwasaidia matibabu wagonjwa.

Huu mjadala nawaageni nilikuwapo sitarudi maana inatosha hapa nilipofikia hayo ni mawazo yangu tu
 
Mdondoaji,
Hapo umegonga msumari na kukomelea na komeo kabisaaa! Kwa kuongezea tu na shule ziwe vile vile wanapewa wanafunzi fedha na sio shule maanake shule huwatoza wanafunzi fedha juu ya ruzuku na misamaha waliyopewa - Huu ni Ufisadi..
 
ahsante kwa kutufungua macho tatizo natumia Rununu ila nikienda cafe nitaisoma vizuri. Na log off
 

Kwa hiyo ukibadilisha act umebadilisha katiba? Dude are u serious?

Ok twende taratibu, unayakumbuka haya maandishi yako hapa chini?


Mkuu kumbuka ukisoma act yeyote waziri amepewa madaraka ya kuammend vipengele au kuvitafsiri. Yes utaratibu ni kwamba inabidi aziangalie hizo ammendments au tafsiri kuwa hazivunji sheria mama ambayo ni katiba lakini hiyo haiipi "act" kuwa katiba hata siku moja. An "act" is not a "constitution"

Naomba nikuulize swali, toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imebadilishwa mara ngapi?
Hivyo basi ni upotoshaji kuita mabadiliko ya "act", ni mabadiliko ya "katiba".
Ntakusaidia kwa 2 ili upate big picture ya ninachouliza

1. Tulipofanya muungano 1964.

2 .Tuliporudi mfumo wa vyama vingi in 1992.
 

ningekuwa najua nisingesita kusema ninachojua ni kuwa taasisi hizo nazo zinafanya kazi katika mazingira na mfumo ule ule wa taasisi za kikanisa. Sasa kwa mfano hospitali ya Aga Khan inapata ruzuku yeyote kutoka serikali kuendesha shughlui zake au inapewa benefits mbalimbali kwenye vifaa n.k? sijui! Lakini nitashangaa kama ikijulikana kwamba baadhi ya watumishi wa Aga Khan wanalipwa toka serikalini? nope! Will I be offended kuwa fedha za umma zinaenda kusaidia taasisi ya Aga Khan kutoa tiba? absolutely not.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…