Haya mdondoaji nimesoma acct ya ya mwaka 1978
hii hapa naiattach
View attachment 40516
Kama niko sahihi section 40 inahusu nini
30 Take-over of private school by Government.
Mkandara sijui unafanya kusudi au ni bahati mbaya ni lini an act ikawa katiba? Or an act to be a constitution in that matter? Katiba ya Tanzania imebadilishwa mara ngapi toka tupate uhuru? Jamani hizi acts huwa zinaweza kubadilishwa au kutafsiriwa na waziri husika lakini si katiba. Iwekwe sawa hiyo hakuna siku katiba libadilishwa eti kwa ajili ya MoU huo ni upotoshajia at its best.
Mkuu nadhani unaruka vitu hapa.. Hizi shule zilikuwa zimetaifishwa chini ya kifungu cha sheria kikatiba, kurudishwa kwake kwa watu inatakiwa katiba ibadilishwe na kutengua ibara ilotangulia kutaifisha mashule hayo..Ndivyo tulivyofanya ktk mashirika na kadhalika.
Pengine mimi ndio sijui unachotaka mimi nijue, lakini navyojua mimi an act ni
sheria, ni statute ambayo inatanguliwa na maagizo ndani ya katiba kulinda act ama mamlaka ya waziri yeyote ktk utendaji kazi wake..
Kwa mfano, muafaka wa MoU umetangulia ammendment na ku fall ktk
31 (1) (b) grant aided schools which shall consist of all community schools owned and managed by a non-government organization but gets subvention or grant in aid from governmental organization;
Na hii ilikuwa mwaka 1995 wakati memorandum imeandaliwa miaka mitatu kabla..Halafu nenda chini utakuta muafaka wa MoU unaingia ktk kifungu hiki..
(2) Subject to subsections (1) and (3) the owner of any school of any category may, upon request made to the appropriate authority and upon approval being granted by
the Minister, move the school from one category to another.
(3) The approval granted under subsection (1) shall be published in the Gazette.
Kitu gani ambacho nimekosea mkuu wangu ama nikuulize wewe kwa nini wali ammend kifungu hiki kama haikuwa lazima. Hata chama kinafungwa na katiba kabla ya kutumikia sera zake...Sera haziwezi kutazama chochote bila kupitishwa na kufuata dira ya Taifa ili kuwa sheria hata kidogo. Kama katiba inaruhusu kurudisha shule au mali za kanisa then, waziri ana mamlaka kisheria ya kukataa au kukubali kutoa baadhi ya shule kulingana na ushawishi wake lakini lazima kwanza katiba iruhusu kuwepo kwa kitu hicho kuwa ni halali.
Binafsi tofauti na Waislaam wengi nasita sana kuona shule za kiislaam zikirudishwa kwa AghaKhan kwa sababu namwona kama mtu wa nje na ningependa sana kuona sisi wenyewe tukisimamia shughuli hizi kuliko wageni. Na sidhani kama serikali ipo tayari kuwarudishia EAMW shule zake kwa sababu toka mwanzo zilipochukuliwa ilikuwa swala zito sana kisiasa na linaweza kuwasha moto mpya. Pengine ndio maana serikali hadi leo imeshindwa kurudisha shule hizi kwa EAMW tofauti na kanisa..But, again bado sioni sababu kabisa ya serikali kuzirudisha shule hizi mikononi mwa kanisa..
Hivi wewe ulikuwa na taarifa hizi kweli kabla ya Waislaam kulalamika.Na sielewi kwa nini mnashindwa kuelewa kitu ambacho kiko wazi kabisa lakini bado mnataka kutetea kama makaburu walivyokuwa wakitetea utawala wao na utoaji kwa sifa ambazo mtu mweusi hakuzikubali..