Lakini nafikiri ni jambo zuri zaidi kama serikali itawasaidia wagonjwa na wanafunzi badala ya fedha hizo kupewa taasisi hizi ambazo tumeona madhara yake tunajenga mgawanyiko mkubwa sana na hatari...JF ni mfano mdogo sana wa hasira za watu walioko huko nje mitaani. Bora kanisa waendeshe shule zao kama Private na serikali badala ya kutumia bil 600 kama alivyodai JK kutoa ruzuku na misamaha ya kodi (guess in his 6 yrs) izitumie hizi kulipia gharama za wanafunzi na wagonjwa huku ikijenga na kuimarisha shule na hospital zake..Si ndivyo ilivyo huku majuu au?
Ni kweli, tayari serikali inachangia gharama ya elimu ya juu kwa wanafunzi - je imeweza kuhakikishia wanafunzi wote wenye mahitjai wanapata fedha za kuendelea na masomo yao?
Pendekezo la serikali kutoa msaada kwa wagonjwa na wanafunzi moja kwa moja hili tayari limekuwa likitokea hasa kwa wanafunzi. Kwa mfano wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waalipiwa baadhi ya kozi zao na serikali moja kwa moja. Je hili ni baya au iwasaidie lakini wasiende kwenye vyuo vya kidini?
Huku majuu kama ujuavyo hata mahospitali binafsi yapo yanayopokea fedha za umma kutokana na program mbalimbali na tena wao wanazo hizo grants n.k Kwa mfano hospitali ya chuo kikuu inayofanya utafiti au inayojikita kutoa huduma fulani inaweza kuomba grants toka serikalini na ikapewa fedha hizo za umma. Hili liko kwa mahospitali mbalimbali ya makanisa na hat aya taasisi za Kiyahudi. Lakini katika Tanzania ni hospitali za Rufaa na zile Teule ndio zinapokea grants hizo na watumishi wake wengine ni waajiriwa wa serikali kuu. Serikali ikisema iondoe hizo grants na kulipa wafanyakazi kwenye hospoitali hizo kama KCMC au Bugando nini kitatokea? Well, inaweza kuwafurahisha wale ambao hawataki fedha za umma ziende kwenye mahospitali ya makanisa lakini itakuwa na matokeo mazito sana kwa wananchi na wagonjwa.
Lakini kuna option nyingine ambayo nayo ni kuwa serikali ijitoe kwenye kutoa misaada hiyo lakini makanisa yaanizshe huduma ya "for profit" kwenye mahospitali yake. Well mahospitali hayo kwa hakika kabisa yanaweza kuendelea lakini ni wananchi wangapi wataweza kupata huduma hiyo ya kulipia?
Binafsi nina mitazamo ifuatayo kwenye suala zima:
1. Ukoloni ulikuwa na matokeo - Hatuwezi kufuta historia yetu au kukana mifumo yote ambayo imetokana na ukoloni. Kuanzia sheria, miundo ya elimu vyuo vyetu na hata ofisi zetu nyingi ni matokeo ya ukoloni huo huo. Hatuwezi kukana wala kukimbia mifumo ambayo imetokana na ukoloni. Siyo sisi tu hata nchi za Kiislamu au India, China na Japan zote zimekopa miufumo mbalimbali kutoka kwa Wakoloni. Ni sehemu ya historia zao kama vile ilivyo sehemu ya historia yetu. Zanzibar kwa mfano wana mifumo ambayo inatokana na ukoloni vile vile na hawawezi kuikimbia. Sasa tuiite mifumo hii kuwa ni "Mfumo Muhammad" au "Mfumo Islam" kwa sababu waliouleta na kuuunda ni Waislamu? Je wale Wakristu wachache walioko Zanzibar wauone kuwa ni mfumo ambao umetengenezwa kuwakandamiza wao?
2. Ninajitahidi kusoma sana mjadala huu tangu ulipoanza na kitu cha kusikitisha ni kuwa wachangiaji wengi wanaanglai kwa misingi ya "Waislamu" vs "Wakristu" na hivyo Mcangajiaji Mkristu anajikuta analazimika kuonekana anatetea MoU na yule Muislamu anaatakiwa kupinga MoU simply kwa sababu ya dini. Sasa hili laweza kuwa ni sawasawa kwa imani na ni haki kabisa lakini kuangalia kwa msingi huo peke yake haitoshi kwa maoni yangu. Kwanini tusiangalie kama "Watanzania" ambao tumeona tatizo ambalo tungependa lishughulikiwe na badala yake kuna maneo ya kila aina ya kejeli kutoka pande hizi mbili za kidini? Ni kweli kabisa hatuwezi kuzungumza kwa staha na heshima kuzungumzia tatizo na hatimaye kutafuta ufumbuzi. Hivi kweli sisi tunaozungumza humu tunaweza kukaa meza moja na kuzungumza kwa lugha tunayotumia hapa na tukapatana kweli?
3. Kama kweli watu hapa wanataka mema yatokee katika mjadala huu ni wazi lazima tuzungumze kwa ukweli na kwa kupima kabisa lolote tutakaloamua kwani ni rahisi kweli kuondoa ufadhili unaofanywa na serikali kwenye taasisi za kidini kwa ajili ya huduma ya kijamii. Hili wala haliitaji ushawishi mkubwa tu. Kama watu wanaona ni jambo lililokiuka sheria au katiba au ni la kibaguzi:
a. Wanaoamini wameathirika (taasisi au watu binafsi) wafungue kesi ya kutaka serikali isitishe kufanya hivyo. Hii ni njia rahisi kwa sababu pande zote zitasikilizwa na ushahidi utalazimishwa kuletwa katika mahakama ya sheria na ukweli ukiwekwa bayana uongo utafunuliwa. Binafsi kweli kabisa ningependa Waislamu ambao wanaamini kuwa MoU ni kinyume na Sheria au Katiba au hata haki za watu wengine wafungue kesi mahakamani kupinga.
b. Kama hilo la "a" haliwezekani jukumu la pili ni kujitahidi kuhakikisha serikali ambayo inatekeleza sera zake hizi inaondolewa madarakani ili ije serikali ambayo itaondoa mfumo huu ambao "unapendelea" kanisa? Kinachonishangaza ni kuwa baadhi ya watu wale wale ambao wanailamu serikali kwa kupendelea kanisa ndio hao hao wanaitetea serikali hiyo ili iendelee kutawala na hivyo kutufanya wengine tuhoji kama ni kweli wanaona serikali ni sehemu ya Kanisa au wanasema tu kwa sababu inasikika vizuri. Sielewei mtu ambaye anasem a"kanisa linaendesha serikali" halafu yeye mwenyewe anasimama na kusema "serikali yetu inafanya vizuri" ! I don't understand it.
Mwisho wa yote ni kuwa suluhisho lolote ambao tunalitaka ni lazima liwe zaidi ya dini zetu, makabili yetu, rangi zetu au mahali tunapotoka. Ni lazima liwe ambalo linajali maslahi ya kila Mtanzania na kuheshimu utu wake bila kupuuzia tofauti zetu za kidini. Je suluhisho hilo litafananaje?