Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Ha ha ha! amejikita kwenye historia ya MoU lakini HAKUJIKITA KWENYE MKATABA WENYEWE UNASEMAJE!
Hebu jikite wewe basi ili ucompliment maelezo yake - kama alivyosema mwenyewe Dr.
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti

Mkuu,kwani bakwata na yenyewe ni hospotali au unazungumzia hospital ya bakwata?
 
thanx dk kwa maelezo yako naomba ukipata muda uje utueleze kuhusika kwako na vurugu na mauaji ya mwembe chai.nipata kuona habar kwenye gazet la al nour[sijui kiarabu]mm nadhan ilikuchafua sana na kupunguza kura zako hasa ilipo fananisha na rwanda gc
 
thanx dk kwa maelezo yako naomba ukipata muda uje utueleze kuhusika kwako na vurugu na mauaji ya mwembe chai.nipata kuona habar kwenye gazet la al nour[sijui kiarabu]mm nadhan ilikuchafua sana na kupunguza kura zako hasa ilipo fananisha na rwanda gc
Mkuu Darasa linasaidia sana hawa jamaa wanakaririshwa ndio maana huwezi kuwa badilisha saa hizi wakina Ritz na Mingoi wanagoogle ili wajekupast uchafu wao hapa
 
Last edited by a moderator:
Tusisahau kuwa mpaka sasa maaskofu wametoa option mbili,serikali kuwaelezea uma ni nini kilichomo ndani ya MOU(sidhani kama kuna maelezo zaidi ya alioeleza Dr Slaa) au kuvunja MOU ambayo madhara yake yatakuwa makubwa kwani operational/administrative cost zitaenda kwa mtanzania pasipo kujali dini,kabila wala chama mfano sasa ivi kuna manesi/madokta wanaolipwa mshahara na serikali moja kwa moja kutokana na MOU kama mambo yakibadirika sio siri kuwa x-ray itakuwa 150000,wakina shehe ponda wajiulize ni waislam wangapi watamudu iyo????
 
Unauhakika kuwa mashek wengi hawana uwezo wa kufanya resarch?


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti

Kaka we unataka wapeleke wapi Bakwata? Kununua makanzu au huduma za jamii?????? Hebu jaribu kushawishi Bakwata wajenge hospitali kama watanyimwa. Tusilalamike.

Muhimbili ni ya serikali, hulipi? Feri, barabara, n.k. ni vya serikali hulipii? Na bado unalipa kodi, tena nyingi.

Pia hata we muislamu unaajiriwa tu bila kubagua lakini nenda taasisi za kiislamu. Maajabu mnaajiri kwa kuangalia kanzu, elimu baadaye.

Matokeo mnakosa focus.
 

sijakuelewa hebu weka hoja zako kwa kutoa fact. Unapopinga hoja kwa porojo bila evidence inakera na kuboa bora ukae kimya
 
Tunashukuru sana Dr. Slaa kwa maelezo ya kina na yanayoeleweka. Angalau sasa tuwacheni tupumue.

Sasa kama ndivyo, na kwa kuwa hili suala linaonekana kutaka kuigawa jamii, na kwa kuwa kwa sababu wanazozijua wao, CCM haitaki kuwaambia watu ukweli, na kwa kuwa kuna baadhi yetu kama akina Dr. Slaa wanaoujua ukweli, na kwa kuwa kuna wabunge, basi angalau hususan wa upinzani, wanaoujua pia ukweli, hivyo basi NI KWANINI HII HOJA ISIHOJIWE BUNGENI KUMALIZA KADHIA HII?

Hii homework akabidhiwe Makamu Mwenyekiti Bara, Mh. Arfi ale nayo sahani moja hadi Serikali ya CCM iitolee ufafanuzi wa kina. Tumechoka na huu upuuzi amba CCM wanataka kuutumia kama mtaji wa kisiasa ilhali wao ndio wahusika wakuu.
 
Mimi labda sijaelewa Slaa anatolea ufafanuzi kama msemaji wa kanisa au kiongozi wa chadema.Babu mbona unatuchanganya uko upande upi

Wewe hapo hujaelewa nini? Au unajitoa ufahamu makusudi ili uonekane umechangia hata kama ulichochangia ni pumba!
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti

Huduma za jamii ni kazi ya serikali, kwa hiyo mashirika ya dini yanafanya hivyo kwa hisani tu. kwa maneno mengine serikali ilitakiwa kufanya hayo yote, lakini tuyashukuru hayo mashirika kwa kuisaidia serikali. na nina uhakika mashirika ya dini zote yananufaika na fedha za serikali, ingawa yanatofautiana viwango kulingana na yalivyojiwekeza.
Ushauri: Tumieni haya mashirika kujiendeleza hasa kielimu, kwasababu miaka ijayo mambo yatakuwa mabaya zaidi. mimi watoto wangu nawapeleka shule yoyote iliyo bora bila kujari ni ya kiislamu au kikristo ilimradi inafuata maadili na kutoa elimu bora. Chonde chonde ndugu zangu badala ya kuendeleza malumbano ni vizuri ukatumia fulsa zilizopo ili baadae usiendelee kuwa mlalamikaji. Sisi ni ndugu ukristo na uislamu umeletwa ukatukuta, sasa iweje uwe bora zaidi ya udugu wetu? kama dini zinatugombanisha basi hizi dini hazina maana.
 
Mimi nilichogundua ni kuwa CDM na CCT/TEC ni faces of the same coin! Hushangai wapambanaji wa CHADEMA ndio hawa wanaopigania MOU!

Mkuu Shinto,
Kwa hiyo unataka kutuambia pia kuwa CCM na Bakwata ni faces of the same coin?

 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru sana Dr Slaa kwa maelezo hayo machache lakini yaliyoeleweka vema,kwa asieelewa basi atakuwa na matatizo yake kichwani na kutaka kurumbana bila sababu! Shukrani sana Dr.
 
November mwaka jana, askofu mkuu jimbo la Mwanza alifanya makubaliano na Dr Magufuli alipokuja kwenye mahafali ya chuo kikuu cha mt Augustine...kwamba serikali ijenge na kukarabati barabara ziingiazo chuoni. Naona greda zimeanza kazi. Hili nalo mtasema MOU? Tatizo lenu waislamu mnalala usingzi wa pono, mkishtuka mnakurupuka.
 
Ungepiga hesabu tokea 1992 mpaka leo Serikali imetoa kiasi gani kwa Kanisa, pesa hizi zingesaidia kujenga Shule, vyuo na Hospitali ngapi?

Je, Serikali iendelee kutoa pesa hizi mpaka lini? na baada ya miaka 20 mingine ni kiasi gani cha pesa itafikia? ni bora kuukata huu mrija sasa hivi kuliko kuja kukaa chini baada ya miaka 20 ijayo na kujilaumu kuhusu kiasi cha fedha zilizoachiwa kutiririka na kulineemesha Kanisa huku serikali ikiendelea kulitegemea Kanisa (hata baada ya miaka 20 ijayo).

Ni lazima kuwe na mwisho wa upelekaji wa hizi pesa Kanisani na wakati bora ndio huu.
 
Hata bugando kumbe ilikuwa hosptali ya kanisa! Hapa nimepata kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…