Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,718
- 1,441
Huwa nashindwa kuelewa wanaoendekeza mijadala isiyo na tija kuhusu udini wana malengo gani. Kwenye maisha cha muhimu ni mtu kupata mahitaji yake bila kujali anapata mahioitaji/huduma zinapatikana kutoka dini gani tofauti na ya kwake.
Huu udini ni hadithi za walafi wa madaraka kwa malengo yao binafsi. Wakishafanikisha malengo yao wataendelea na zambi yao ya kutenga wenzao. Kama wanatumia ukristo wakifika mbele wataanza sisi wakatoliki hao waluteri. Wakiwa waluteri watasema sisi waluteri halisi nyie walokole mpaka mwisho wanaoumia ni wananchi wa kawaida. Hivyo hivyo kwa wasilamu sisi BAKWATA nyie BALUKTA.
Mabishano na hoja za udini hazitatufikisha popote ,tumesoma na watu wa dini zote .Kilchokuwa kinatuunganisha ni utamaduni wetu kupitia lugha yetu ya Kiswahili, Utanzania kwanza vingine baadae.