Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Huwa nashindwa kuelewa wanaoendekeza mijadala isiyo na tija kuhusu udini wana malengo gani. Kwenye maisha cha muhimu ni mtu kupata mahitaji yake bila kujali anapata mahioitaji/huduma zinapatikana kutoka dini gani tofauti na ya kwake.

Huu udini ni hadithi za walafi wa madaraka kwa malengo yao binafsi. Wakishafanikisha malengo yao wataendelea na zambi yao ya kutenga wenzao. Kama wanatumia ukristo wakifika mbele wataanza sisi wakatoliki hao waluteri. Wakiwa waluteri watasema sisi waluteri halisi nyie walokole mpaka mwisho wanaoumia ni wananchi wa kawaida. Hivyo hivyo kwa wasilamu sisi BAKWATA nyie BALUKTA.

Mabishano na hoja za udini hazitatufikisha popote ,tumesoma na watu wa dini zote .Kilchokuwa kinatuunganisha ni utamaduni wetu kupitia lugha yetu ya Kiswahili, Utanzania kwanza vingine baadae.
 
Thanks Dr. Slaa kwa ufafanuzi ambao wengi wa watz tulikuwa hatuujui vema zaidi ya kusikia huku na kule juu ya MOU.
 

Yale yaleeee, uelewa finyu! Kwa mbali nakumbuka jinsi serikali ya Tanzania ikiongozwa na Ali Hasan Mwinyi ilivyokabidhiwa na serikali ya Uingereza kupitia Crown Agents pesa za waliokuwa wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iwafikishie walengwa. Kama kawaida ya serikali za kipuuzi iliyojaa mafisadi, viongozi wa serikali wakakalia hizo hela kwa madai kuwa ni hela nyingi sana...zikilipwa zote nchi inaweza ikayumba.

Kwa wivu kuna watu walifikia hatua ya kuhoji itakuwaje serikali ichote mapesa hayo yote (kodi zao kama walivyoziita) kuwalipa...mtu unajiuliza hizo zela zilizotolewa kama pensheni kwa wastaafu, zinahusishwaje na kodi zao. Laiti ingekuwapo MOU kati ya serikali na wastaafu kabla ya hizo hela kukabidhiwa hii serikali ya wezi labda serikali ingeheshimu makataba, isingekimbilia kuzidokoa hizo hela na kuwatesa wazee watu.

Katika misingi hiyo hiyo ndio maana swala la MOU inayoongelewa inawapa watu taabu...kama kawaida kuna waliojawa wivu hadi wanahusisha msaada unaotolewa na taasisi za Ujerumani kwa Makanisa kupitia serikali ya Tanzania nao sasa yadaiwa eti ni kodi za Watanzania. Kweli nchi hii imejaa mabumbumbu wasio kifani na hata ufafanuzi unapotolewa bado wamo tu wenye uelewa finyu, pyuu!

Ili Makanisa yapate msaada huo serikali ilitakiwa itoe tamko la kuondoa wasi wasi kwamba haitataifisha tena hizo huduma kama shule, hospitali nk. Hicho ndicho kiini cha MOU, msaada huo uwe wazi na utolewe kupitia kwa serikali iliyopo madarakani...sasa haya madai ya kodi za wananchi kuchotwa serikalini kupewa Makanisa yanatoka wapi? Wanaotoa msaada wako kimya, wezi na wajinga wanapayuka ovyo.
 
Hawa watu wenye elimu ya kupiga dufu plus phd madrassa hawawezi kuelewa kitu hapa.
 
CAN SOMEONE HELP PLEASE?...KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MoU (na ufafanuzi mzuri wa historia ilopelekea kuanzishwa kwake from Dr.) na OIC?!?
 



kwa kifupi kinachofanyika ni serikali inaajiri watumishi wa fani mbalimbali mfano walimu, watabibu n.k halafu vituo vyao vya kazi vinakuwa katika taasisi za madhehebu husika kama hospitali, mashule n.k Ikumbukwe kuwa hapa kuwa hawa ni waajiriwa wa serikali na wanalipwa na serikali.(unaweza kurejea wakati wa mgomo wa madaktari utapata jibu kwa hospitali kama bugando na KCMC)

Finacial assistance siyo kupewa fedha , hapa kinachofanyika ni kuondoa ushuru wa bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi.
 
Hawa watu wenye elimu ya kupiga dufu plus phd madrassa hawawezi kuelewa kitu hapa.
This is very unfortunate!hata BAADHI yao wenye elimu dunia ya kutosha tu wanashindwa kuelewa maelezo clear kama hayo...je,ni sumu ya kibaguzi wanalishwaga huko madrasa?ni wivu?au ni inferiority complex ya wengi wao,tena ya kulishwa?
 
Serikali kama haina hospitali katika wilaya fulani inatafuta hospitali gani ipo katika eneo hilo, bila kujali ya dini gani na baada ya kuipata inaiteua hiyo kuwa ya wilaya, na wataalamu wake watapelekwa hapo ili wawahudumie wananchi wa wilaya hiyo. Ikiwa inafanya hivyo lazima pia ipeleke dawa, fedha za kuwalipa wataalamu hao, kwa maneno mengine inabidi ishirikiane na taasisi hiyo kuiendesha. Kilichotokea mahala pengi hospitali zilizopatikana zenye viwango vinavyokubalika zilikuwa za madhehebu ya dini hasa ya kikristu. Kwa hiyo fedha hizo zikiwa zinatoka kwa pamoja na kuzigawa wengi hata wasomi wanasema tu zinaenda kusaidia makanisa, kitu ambacho si kweli tunatibiwa wenyewe na wanalipwa wataalamu wetu n.k Nashauri kuna wilaya mpya nyingi zimeanzishwa hazina hospitali nendeni mkajenge mapema serikali itatia mkono wake sasa hivi.
 
Hivi ninyi watu mbona inakuwa vigumu hivyo kuelewa kitu straightforward namna hiyo?
Kwani ni nani alekuwa ametaifisha hizo hosp na mashule ya kanisa?
Serikali ilitaifisha kutoka kwa Wajerumani au makanisa?
Baada ya serikali kushindwa kuziendesha/na makanisa kuzidai baada ya kuona hosp/mashule hayo kuwa ktk hali mbaya Serikali ilitakiwa 'kuingia huo mkataba' na hayo makanisa ili hao wafadhili watapotoa hela zao kuwe na uhakika wa kuendelezwa na kutunzwa kwa hosp na shule hizo(kusijekuwa na utaifishwaji tena na kukosa utunzaji na uendelezaji kama ilivotokea).
Kwa mantiki hiyo (kama ilivofafanuliwa vizuri na Dr.Slaa hapa) unafikiri hiyo MoU ilitakiwa kusainiwa kati ya makanisa na Ujerumani au na serikali ya Tanzania?
 

Ndio shida yenu WAFILISTI, hata kitu kielezewe vipi bado hamuelewi. Sasa nani anakula na anakula nini?

Kwa akili za kijinga, mtu atadhani kuwa Kanisa linanufaika kwa namna fulani na MoU, ilhali ni mzigo. Sasa mimi nataka nikuulize maswali machache:
1. Bunge linapitisha bajeti kila mwaka, na marejeo ya matumizi ya fedha hufuatiliwa kabla bajeti mpya haijapita, Je, wabunge woooote Waislam na waziri mwenyewe nao hawana akili, akili mnazo wewe na Sheikh Bassalleh tu mnaolalamikia MoU?
2. Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali ina wabunge Wakristo watupu? Au Bassalleh aliyekutuma na wewe ndio mnajua zaidi hesabu kuliko kina Mkulo?
3. Hiyo MoU ya Wafilisti ilipelekwa lini na kwa nani? Manake nikiyarejea maelezo ya mkuu wa kaya kwenye Baraza la Idi Dodoma mwaka juzi, alikuwa akiwalaumu kwa kutopenda kwenu kujihusisha na maendeleo badala yake mnaishia majungu na manung'uniko kama kondoo.

Kwa kumalizia, Dr.Slaa sio mchungaji, kama unashindwa kuelewa jambo dogo hilo, utaelewa MoU?

Serikali ingefanya juhudi hii MoU itafsiriwe kwa Kiarabu ili isomwe madrasa zote kwa lugha ile mnayowacharazia watoto mikwaju mchana kutwa kukariri maneno wasioelewa
 
Naam! kila kitu kiwekwe mezani:

Mabilioni mangapi serikali imeipatia makanisa tokea 1992.

Ni mabilioni mangapi Kanisa limefaidika kupitia misamaha ya kodi.

Mbali na pesa kutoka serikalini ni kiasi gani Kanisa limeingiza kwa njia ya kuwatoza wagonjwa ada/malipo ya matibabu.

Serikali imelipa mabilioni ngapi kama mishahara ya wafanyakazi wa Hospitali za makanisa.

Serikali imetumia kiasi gani cha pesa katika kukarabati Mahospitali ya kanisa n.k
 
hutajibiwa! MoU ilifungwa kiusiri na kila kinachoizunguka MoU ni usiri tu!
This is ridiculous!who is making it secret?the gvt??!!
The church has already come out clear and open demanding the gvt to explain this issue to the people wanolipotosha kama wewe!!na walisema wazi wapo tayari kama serikali itataka kuuvunja iamue yenyewe!!
Sasa nashindwa kukuelewa hapa!!
 
kah yamekuwa hayo tena?Na ikishajitoa ndo waislamu watagawiwa hizo shule na hospitali za makanisa au?je,unaifikiria tu dini yako au unafikiria welfare ya watanzania wenzako wa dini zote na wasokuwa na dini?
kwa mfano gharama kwenye hizo hosp ikiwa sawa na za private hosp watanzania masikini watatibiwa wapi?
Ulishaenda wewe/kupeleka ndugu yako kutibiwa MNH au MOI?
Je,matibabu huko ni bure?
Unalinganisha vipi huduma na gharama huko kulinganisha labda na hosp kama bugando,kcmc,peramiho,ifakara,ndanda nk?
 

Kimeshawekwa mezani. Mmesutwa kwa kauli yenu ya uwongo kuwa MOU inatoa fedha za serikali kwa hospitali za makanisa. Kumbe ni fedha za wahisani. Mmesutwa kwa uwongo wenu kwamba hospitali za makanisa zilijengwa kwa hela ya walipa kodi wa Tanzania, kumbe ni hela ya walipa kodi wa Ulaya. Mmesutwa kwa uwongo wenu kuwa serikali inapendelea wakristo, kumbe ilishindwa kuendesha zile shule ilizozitaifisha na kwa aibu wakatafuta njia ya kuzirudisha. Sasa mnakuja na single nyingine juu ya mabilioni ya serikali kwa makanisa, na misamaha ya kodi. Hata Bakwata wanapewa msamaha wa kodi. Ukweli ni kama nuru inayomulika na kutokomeza giza.
 
PLEASE!!!!!!!!!!! Kuwa composed na soma kitu kwa makini kabla ya kujibu.
Unajichanganya kwa kuonyesha kuwa serikali ilitaifisha shule za upande mmoja tu,si kweli.Shule zote zilitaifishwa ila wenzetu wakarudi kudai shule zao kutokana na sababu ambazo Slaa amezieleza wazi.
Mimi nimesoma shule ya msingi Lumumba hapo mnazi mmoja Dar na Bakwata walikuwa na ofisi zao hapo,miaka ya 70.Na wao walikuwa na haki ya kudai shule lakini zilijengwa na wahindi wa I smailia na kama unavyowajua wenzetu ni wafanyabiashara na hawataki kuingia katika mgogoro na serikali.
Tatizo letu Waislamu ni kukosa taqwaa (Ucha Mungu wa kweli na kusimamia mambo yetu kwa uadilifu).Wengi wa viongozi wetu ni wachumia tumbo ukiacha taasisi kama Islamic Foundation ambayo kwa kweli imetutoa kimasomaso,hao Bakwata ni kuuza mali za wakfu na viwanja.How on earth ukauza kiwanja Chang'ombe ili ukapewe kiwanja porini?Kwa mantiki ya kawaida kwa taasisi kama Bakwata inge maintain kiwanja cha Chang'ombe na at the same time ikanunua kiwanja hicho cha porini kwa malengo mengine.
Ukitoka Morogoro kuja Dar palikuwa na shamba la mkonge likititwa Kilimanjaro estate,leo angalia Wakatoliki walivyoitumia fursa ya kugawanywa viwanja nat ayari wamefungua Chuo Kikuu.Angalia ni nani aliyenunua kiwanja kile,ni MUISLAMu tena mwenye uwezo ambaye angewashauri kuwa msiuze,huu ni mfano mmojawapo kati ya mingi.
Soma kitabu "cha maisha na wakati wa Abdulwahid Sykes",Nyerere alizungumzia suala la kutokua na usawa wa elimu kati ya Wakristo na Waislamu na ndo maana akazitaifisha shule.
Waisalmu tuitathmini na tuanze upya,vijana wasome elimu zote mbili kwa bidii kabisa nawawe na ucha Mungu wa kweli inshallah tutapata maendeleo makubwa.Kulalamika si sifa ya Muislamu.
 

Heshima yako mkuu. Naona umechambua vyema juu ya hii MoU. Mimi nimekuwa nikiisikia tu lakini nilikuwa sijaelewa undani wake. Mimi ni msikilizaji mzuri sana wa Radio Imani. Hii Redio imekuwa ikiiipigia kelele sana MoU. Sasa naona naielewa baada ya huu ufafanuzi.

Lakini umeanza kwa kuonyesha kwamba BAKWATA, TEC na CCT zilikuwa zishirikishwe kwenye mazungumzo. Baafaye hapo mbele tunaona BAKWATA imeenguliwa na zinabaki TEC na CCT. Nini kilitokea hapa?
 

Acha porojo kaka, pitia hotuba ya rais Kikwete kwenye baraza la idd kule Dodoma ndiyo utajua serikali inatoa kiasi gani cha pesa kwa kanisa kila mwaka. Utasutwa wewe.
 
Wawepo washauri kumi kama wewe mkuu! mabadiliko ni dhahiri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…