Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

nafikiri hakutakuwepo na malumbano tena kati ya wakristo na waislam kuwa kuna baadhi ya dini zinapendelewa napenda nirudie kauli ya mh kikwete kuwa acheni kulalamika na nyie jengeni za kwenu ndio mwone kama serikali haitawasaidia
 
Wee ni mnafiki kuliko hata sheitwani mwenyewe. Mara nyingi unajitapa humu kuwa unafahamiana, unawasiliana na huwa unakutana na watu wakubwa (mawaziri) wa serikali hii... Ajabu kwa chuki na unafiki wako maswali ya kuwauliza walio serikalini unamuuliza asiye huko. Siyo wewe wakati fulani ulikuwa kwe tafrija Ikulu ya magogoni?! Au ulishiriki kama jini?! Ulisahau nini kuwauliza hayo kina Kikwe.te??? Unafiki.
 
Unapolinganisha idadi ya wafanyakazi walioajiriwa katika elimu lazima ujue kwamba Wakristo walitangungulia kuelimika. Wakati waislamu walipokuwa wakiogopa kupeleka watoto wao kwenye shule za misheni wasije wakabadilishwa dini, wakristo walikuwa wakiendelea kusoma hivyo kufanya idadi ya wakristo wasomi kuwa wengi kuliko idadi ya waislamu wasomi. Kumbuka Ukristo ndio ulioleta hiyo elimu unayolilia kwamba umepunjwa. Wamishenari walikuja na Kanisa Shule (Elimu) na Mahospitali. Uislamu ulikuja na Misikiti na madrasa. Kwa hiyo waliosoma kwanza nchi hii ni wakristo na waislamu wachache waliothubutu kupeleka watoto wao kusomeshwa na misheni ndiyo maana unaona hakuna equality katika idadi ya waajiriwa.
Katika nchi yetu Tanzania waislamu ni wachache sana ingawa wao hudhani ni wengi kiidadi. Waislamu wanapatikaka Kigoma Ujiji sehemu zingine wamejaa wakristo. Wanapatikana unapofuata njia ya reli ya kati lakini sehemu za ndani mbali na reli ya kati utakuta kuna wakristo na wapagani. Tabora waislamu wako Urambo na Tabora mjini sehemu zingine wamejaa wakristo. Singida maeneo ya wanyaturu ndio yana waislamu wengi hata hivyo bado na wakristo wako. Dodoma waislamu wanapatikana Kondoa na Dodoma mjini kwa uchache sana hata linganisha idadi ya misikiti na makanisa utakuta makanisa ni mengi sana mara kumi kuliko misikiti. Morogoro wakristo ni wengi mjini na vijijini, Pwani waislamu wanaweza kuwa wengi lakini bado wakristo ni wengi pia. DSM Kwa sasa wakristo ni wengi kuliko waislamu ukizingatia kwamba kwa sasa watu wa kuja ni wengi kuliko wenyeji wa asili wa Dar hiyo inafanya Wakristo kuwa wengi kuliko waislamu Dar. Tanga Waislamu wanapatikana kwa wingi Pwani lakini unapotoka pwani unakuta wakristo ni wengi kuliko waislamu Kilimanjaro: Same wanapatikana waislamu wachache kuliko wakristo. Ukienda Lindi na Mtwara Waislamu wako kando kando ya bahari na ndani ya nchi wakristo wamejaa, Iringa Waislamu wako mijini vijijini hawako na hata mjini Iringa Wakristo ni wengi kuliko waislamu. Mikoa mingine yote iliyobaki ina wakristo wengi kuliko waislamu kwa idadi ya asilimia kama 90% Wakristo na 10% waislamu. Kanda ya ziwa ambako kuna msongamano mkubwa wa watu idadi kubwa ni wakristo kwa asilimia hizo hizo, pamoja na Mbeya, Rukwa, Katavi Arusha, Manyara na kadhalika. Sasa unapoona wakristo ni wengi katika ajira ni wengi pia katika nchi hii, na wamesoma kwa wingi kabla ya waislamu na hawajaacha kusoma na hawataacha kusoma maana ukristo, Elimu na Tiba vinaenda pamoja kwa wakristo.
Ingawa kwa sasa waislamu wamejitahidi kujenga mashule bado ndani ya shule hizo wanafunzi wakristo ni wengi kuliko waislamu. Waislamu wanalazimisha wanafunzi wa kike wavae hijabu cha ajabu wakisharudi nyumbani hawavai hijabu hata kama ni waislamu ikionyesha kwamba wangepewa hiari ya kuchagua wangechagua vazi lingine mbadala ya hijabu.
Pamoja na yote hayo ni wanawake wangapi wanavaa kiislamu; kama tutatafuta kuwafahamu watu kwa mavazi yao wanaovaa kiislamu nchi hii watakuwa ni wachache sana.
Kwa hiyo takwimu hizo ni sahihi waislamu wasomi nchi ni wachache kati ya wakristo wasomi wengi.
 

Serikali haijarudisha hospitali na shule zote. Zilizorejeshwa hazifiki hata 1% ya zilizotaifishwa!
 
Hili shirika linapokea pesa toka serikali ya ujerumani kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo kupitia makanisa.



Nadhani hukumuelewa Dr. Slaa. Shirika hilo linapata misaada toka mashirika ya kidini ya Ujerumani si serikali ya Ujerumani. Isipokuwa dini na mashirika ya dini nchini Ujerumani hupata ruzuku toka Serikalini.
 


Sababu za MOU bado zipo hadi leo. Kumbuka hospitali za DDH yaani hospitali teule za wilaya na hospitali za rufaa na nyingine kama CCBRT bado zinahudumia watu wengi sana bila kujali itikadi ya dini zao. Kuhusu Serikali kushindwa kujenga hospitali zake hilo nadhani inabidi muiulize serikali dhaifu na legelege ya CCM. Lakini pia Serikali haijapangisha Hospitali bali Hospitali hizo huendeshwa kwa ubia. Serikali hutoa hadi 50% wakati Makanisa hutoa 50% na zaidi ya gharama za uendeshaji kutegemeana na utaratibu kwenye hospitali husika.
 
Sasa kama Tanzania haiwezi kujiunga na OIC kwa kuwa haina dini, mbona Tanzania hiyo hiyo inaomba misaada nchi za nje kwa ajili ya kanisa? Au dini ya Tanzania ni Katoliki?

Watu ni wagumu kuelewa. Kama ungesoma post ya Dr. Slaa vizuri ungeelewa. Serikali haiombi misaada nchi za nje kwa ajili ya makanisa. Baada ya serikali kutaifisha taasisi za makanisa mashirika ya dini ya nje yalisitisha misaada yao maana hayo mashirika ndiyo yalitoa misaada ya kujenga hospitali na shule hizo. Baada ya seriakali kukubaliana na makanisa na kusitisha utaifishaji hayo mashirika ya dini ya nje ndo yakarejesha misaada ambayo yalikuwa yanatoa kwa makanisa. Na hadi sasa misaada huwa inatolewa na mashirika haya.
 
Kina yahe wanatumia akili yao kama wao kidogo sana,mambo mengi wanaigaiga kutoka nchi za kiarabu ambako miaka ya nyuma nao hawakuthamini elimu,waraabu kwa kiasifulani wanatambua elimu ni nini tatizo lipo kwa bongo sleep wa tz na kwingineko afrika.kz kubwa waijuayo ni kuwatoa b.k.r.za buzy dada zao kwa kigezo cha kulinda heshima ya familia pindi waolewapo.
 
Mama POROJO ni Mfuasi na shabiki mkubwa wa mtuhumiwa mmojawapo wa wanaotaka kuisambaratisha CHADEMA.Soma post zake za Nyuma.

wewe ben usaliti wako na sumu unayotembea nayo hadi bar unayotaka kuwalisha wenzako umeumbuka acha kutumika
 
Ndugu zangu wanaforum kwanza namshukuru Dr. Slaa kwa kutolea ufafanuzi suala la MOU maana limeibua mjadala na manungúniko mkubwa sana ktk makundi mbalimbali ya jamii wengine bila hata kulielewa vema. Mimi binafsi nimeshalieleza sana kwenye facebook mara nyingi sana. Lakini nachokiona kwa wengi pamoja na ufafanuzi wa Dr. Slaa bado wengi hawaelewi. Napenda kuongezea maelezo yafuatayo:-

(1) Watu wanasema hajaeleza juu ya pesa zinazotolewa na serikali kwenda kwenye uendeshaji wa hospitali. Ni kweli Dr. Slaa hajaeleza juu ya masuala ya pesa. Yeye ameeleza tu mazingira yaliyopelekea kuwepo kwa makubaliano yaani MOU kati ya serikali na Makanisa na si taratibu au kanuni zilizowekwa na serikali ili kutekeleza makubaliano hayo.


(2) Ikumbukwe kuwa ni jukumu la serikali kikatiba kutoa huduma za jamii kama afya kwa wananchi wake. Lakini baada ya hali ya kiuchumi kuwa ngumu hasa ktk miaka 80's baada ya vita ya Uganda na Tanzania 1979, serikali ilikosa uwezo wa kutoa huduma za kijamii kwa watu wake waliokuwa wameongezeka na kuzidi idadi ya hospitali na shule zilizokuwepo ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zimetaifishwa hapo kabla. Ilishindwa kabisa kuendesha hata shule na hospitali walizokuwa wamezitaifisha na pia ikashindwa kujenga nyingine kwa hiyo huduma za elimu na afya zilizidi kuwa duni. Kama njia ya kutatua tatizo la wananchi kukosa huduma za afya serikali ikataka kuendelea kutaifisha hospitali za madhehebu ya dini zilizokuwa zimejengwa tena baada ya utaifishaji wa kwanza ili izitumie kuwahudumia wananchi. Lakini baada ya mvutano mkali na makanisa ilishindwa kuzitaifisha hizo hospitali ikabidi serikali ikubaliane na makanisa iwahudumie wananchi wake kupitia hospitali hizo za makanisa.


(3) Kuhusu Pesa: Kwanza napenda ieleweke kuwa sihospitali zote za makanisa zilizoko kwenye makubaliano ya serikali kuwahudumia wananchi wake kupitia hizo hospitali kwa kuzipatia ruzuku. Zinazopata ruzuku ni zile za wilaya na mikoa yaani Hospitali teule (District Disignated Hospitals –DDH) na zile za rufaa kama Bugando, KCMC na nyinginezo kama CCBRT. Ilibidi serikali iwe inatoa ruzuku ya 0%-50% ya gharama za uendeshaji ili gharama za huduma ktk hospitali hizo ziwe nafuu ukilinganisha na hospitali ambazo ni za binafsi kwa 100% huku makanisa yakitoa 50%-100% ya gharama za uendeshaji. Kwa maneno mengine makanisa hutoa pesa zake kugharimia huduma kwa watanzania wote bila kujali dini zao. Na mara nyingi serikali inapochelewa kupeleka hata hizo ruzuku makanisa hutoa gharama zote. Kwa maneno mengine makanisa huikopesha serikali bila hata riba yoyote kwa ajili ya kuwahudumia watanzania wote!

>>Ruzuku hizo za hadi 50% hutolewa kama fedha, madawa, misamaha ya kodi, mishahara, kuendeleza watumishi wa hospitali, vifaa tiba na vifaa vya maabala. Kumbuka gharama za uendeshaji ktk vipengere vyote hivyo nilivyotaja hutolewa kwa ubia yaani 0%-50% serikali na 50%-100% makanisa. Kwa maneno mengine tunaweza kusema uendeshaji wa hospitali hizo nusu ni wa umma na nusu wa binafsi. Makubaliano haya yamewekwa kwa lugha ya kisheria ktk MOU. Taratibu za utekelezaji wake hazipo kwenye makubaliano hayo (MOU) ndo maana watu hawaelewi wanadhani serikali hutoa tu hela na kupeleka makanisani. Bajeti za serikali ziko wazi zinaonyesha ruzuku zinazovyotolew. Na mtu akisoma kwenye MOU kwamba serikali itatoa support anadhani Pesa zinapelekwa tu na uendeshaji wote unatumia pesa ya serikali; HAPANA! Support hiyo ambayo ni ruzuku inatolewa ili gharama za matibabu ziwe nafuu na za chini zenye ulinganifu na hospitali za umma. Mfano ukiangalia gharama ktk hospitali za rufaa za Bugando na KCMC zina ulinganifu na zile za hospitali za rufaa za Mbeya na Muhimbili; za wilaya na mikoa hivyo hivyo. Na huduma nyinginezo kama za mama na mtoto hutolea bure tofauti na hospitali za binafsi mfano za Aga Khan. Magonjwa mengine kama Fistula na mengineyo kwa akina mama na wazee wagonjwa hutibiwa BURE (mfano CCBRT).

>>Sasa watu wanahoji kama serikali inatoa ruzuku za uendeshaji ktk hospitali za makanisa kwa nini huduma hazitolewi bure. Jamani ebu jaribuni kuelewa mfumo wa utoaji wa huduma za jamii hapa nchini. SERA YA SERIKALI NI KUCHANGIA HUDUMA ZA JAMII kama AFYA, ELIMU n.k. Hata kwenye hospitali za umma kama Muhimbili na nyinginezo ambako serikali hupeleka ruzuku ya kuziendesha kwa 100% kuna gharama za kulipia. Mfano mimi huwa naenda MOI na kumuona daktari bingwa (Specialist) au daktari wa mazoezi huwa natoa 30,000/= (Consultation fee) hapo bado madawa ambayo nayo inabidi uchangie na wakati mwingine unaambiwa hayapo kwa hiyo inabidi ukanunue kwenye maduka ya dawa binafsi. Na hata kama sio first track kumuona daktari bingwa (specialist) kwa kawaida inaenda hadi 20,000/=. Sasa swali la kujiuliza ni hili: Kama kuna uchangiaji kule ambako serikali imejenga kwa pesa ya wananchi na ambako inatoa pesa ya wananchi kama ruzuku ya uendeshaji kwa 100%, iweje gharama za huduma ziwe bure kule ambako serikali haikujenga na ambako hutoa ruzuku ya 0%-50% (si 100%) kwa ajili ya gharama za uendeshaji tu? Ebu wanaforum tuache jazba tufikirie na kuchunguza ukweli sahihi ili tupate uhalisia badala ya kuendelea kukaririshwa taarifa za uongo.

(4) Wengine wamehoji na kusema kuwa serikali inayaombea makanisa misaada toka nje. Ni upotoshaji mkubwa. Serikali haiombi misaada kwa ajili ya makanisa hata kidogo! Ikumbukwe kuwa Mashirika ya dini ya kikristo ya nje hata kabla ya uhuru yalikuwa yakitoa misaada na kutoa huduma za kijamii hapa nchini. Hata baada ya uhuru mashirika hayo yameendelea kutoa misaada kwa makanisa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali na shule. Lakini kutokana na serikali ya Tz kubinafsisha shule na hospitali za makanisa ambazo zilijengwa kwa misaada ya Mashirika ya Kikristo ya nje yalijiondoa ktk kutoa misaada hiyo. Kwa hiyo makanisa ya TZ yakawa tena hayapati misaada toka kwa mashirika ya makisa yao huko nje, matokeo yake ujenzi wa shule na hospitali ukazorota. Baada ya hali hiyo ilibidi makanisa yajadiliane na serikali juu ya hali hii na serikali ya TZ ilibidi ikubali kuhusika ili kurejesha uhusiano na mashirika hayo ya Kikristo ya nje ili yaendelee kutoa misaada kwa makanisa ktk ujenzi wa shule na hospitali ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii. Kwa hiyo kusema kwamba serikali inayaombea makanisa misaada toka nje ni kuelewa vibaya maelezo yaliyoko kwenye MOU au kuamua kupotosha ukweli halisi. Na kama kuna mtu ana ushahidi wa serikali kuomba misaada kwa ajili ya makanisa alete huo ushahidi. Misaada inayoombwa na serikali kusaidia bajeti yake inapokuwa ya wizara ya afya na kuipeleka kwenye hospitali zinazomilikiwa na makanisa ni katika mpango ule ule wa serikali kutoa hadi 50% ya gharama za uendeshaji wa hospitali hizo ili kuwahudumia wananchi wake. Isichukuliwe kwamba serikali inomba misaada kwa ajili ya kuendesha ibada au mambo ya kiimani ya makanisa! Bali ni misaada ya kusaidia bajeti yake ikiwemo wizara ya afya na hivyo kupelekwa kwenye hospitali. Na hii haina itikadi za kidini watu wote hutibiwa na kupata ajira ktk hospitali hizo kwa usawa.

(5) Kuhusu support ktk shule za mashirika ya dini naomba kuwaelewesha hivi: Support hiyo ktk shule haitolewi kama FEDHA! HAKUNA fedha inayotolewa na serikali kwenda kuendesha shule za makanisa. Support inayoongelewa hapo kwenye MOU ktk shule ni kupitia walimu waliosoma ktk shule na vyuo vya umma. Waalimu na watumishi wote waliosomea shule za serikali na vyuo vya serikali wamesomeshwa kwa pesa za wananchi aidha bila wao kuchangia (yaani waliosoma bure) au kwa huchangia karo na michango. Mfano karo ya shule za boding (sekondari) ni 70,000/= au day ni 20,000/=. Sasa hii si gharama halisi ambayo mwanafunzi alitakiwa kutoa bali ni gharama ambayo mwanafunzi huchangia tu, gharama kubwa kwa ajili ya kumsomesha hutolewa na serikali. Kwa hiyo wanafunzi hao wanapomaliza mafunzo yao mfano waalimu HAWAZUIWI kwenda kuajiriwa na shule za makanisa au za watu au mashirika binafsi kwa kuwalazimisha waajiriwe serikalini tu ili warudishe gharama. Bali serikali inawaruhusu waajiriwe hata kwenye shule hizo za makanisa au za watu na mashirika binafsi mengine kama huduma kwa jamii. Na wanapoajiriwa huko wanalipwa na makanisa. Hii ndiyo support inayoongelewa kwa upande wa shule za kawaida za makanisa. Hakuna hata senti moja inayopelekwa kuendesha shule binafsi. Makanisa huendesha shule zake kwa karo na pesa za sadaka na misaada toka mashirika ya kidini ya nje. Bajeti za serikali ziko wazi kama kuna mtu ana ushahidi huo anikosoe na asipotoshe!

>> Kwa hiyo suala la support watu walielewe vizuri iwe ni kwa Hospitali au shule. Liko kama nilivyolieleza. Pia ieleweke kuwa makanisa ni wamiliki tu wa hospitali na shule hizo. Hakuna ibada yoyote ktk hospitali hizo. Hospitali hizo hazihitaji mchungaji, padre au askofu wala kutumia msitari wowote wa biblia au kitabu chochote cha dini ili kutoa huduma. Lakini pia huhudumia na kuajiri watu wote bila kujali itikadi za kidini, kabila, kanda au hata uzanzibar na ubara. Vigezo vya ajira ni taaluma ya mtu na huduma kwa wagonjwa ni kwa watu wote. Tofauti na mahakama za kadhi ambazo huduma zake ni ibada kwa waislamu na huhitaji viongozi wa dini yaani Makadhi na kutumia mistari ya Quran na vitabu vingine vya kiislamu ktk kufanya kazi zake.

(6) Wengi wanajiuliza kwa nini serikali iliingia makubaliano na madhehebu ya dini ya Kikristo na si madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu na Waislamu au hata mashirika mengine binafsi? Jibu lake ni kuwa makubaliano haya yana msingi wake kutoka kwenye utaifishaji uliofanyika miaka ya 70's ambapo waathirika wakubwa yalikuwa ni madhehebu ya dini ya Kikristo. Lakini pia baada ya serikali ya CCM kushindwa kutoa huduma za afya na elimu kulingana na uhitaji, miaka ya 90's madhehebu ya dini ya Kikristo yaliamua kuingilia kati ili kuokoa maisha ya watanzania na kuanza kujenga tena hospitali na shule. Lakini hofu na maumivu ya utaifishaji vilikuwa havijasahaulika. Hivyo madhehebu ya dini yalipoanza kujenga tena hospitali hizo na shule, Kwanza ilibidi yahakikishiwe na serikali kuwa haitataifisha tena hospitali na shule zao. Pili kulikuwa na suala la gharama. kumbukeni kuwa ni jukumu la serikali kutoa huduma za afya na elimu kwa wananchi wake. Sasa kwa hali halisi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa, madhehebu ya dini yasingeweza kutoa huduma za afya bure au kwa gharama ya chini. Hivyo serikali ilibidi itoe ruzuku ili baadhi ya huduma kama kwa akina mama na watoto, wazee na kwa baadhi ya magonjwa kama kifua kikuu, fistula,n.k ziwe bure na kwa wengine huduma ziwe za bei nafuu kwa ulinganifu na hospitali nyingine za umma.

(7)Kuhusu Misaada: Serikali haiombi misaada nchi za nje kwa ajili ya makanisa. Bali baada ya serikali kutaifisha taasisi za makanisa hapa TZ mashirika ya dini ya Kikristo ya nje yalisitisha misaada yao maana hayo mashirika ndiyo yalikuwa yakitoa misaada ya kujenga hospitali na shule hizo kwa kushirikiana na sadaka za waumani wa hapa TZ. Baada ya seriakali kukubaliana na makanisa na kusitisha utaifishaji, hayo mashirika ya dini ya nje ndo yakarejesha misaada ambayo yalikuwa yanatoa kwa makanisa ya hapa TZ. Na hadi sasa shule na hospitali zinaendelea kujengwa kwa misaada ya mashirika hayo pamoja na sadaka za waumini hapa TZ. Misaada inayoombwa na serikali ni ile inayoombwa kwa ajili ya kuboresha sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na sekta ya afya. Sasa serikali inapochukua pesa kutoka ktk misaada hii na kuipeleka kwenye sekta ya afya na hatimae kwenda kwenye Hospitali za makanisa, ni katika yale makubaliano niliyoyaeleza ya kuendesha hospitali hizo kwa ubia; yaani 0% -50% ya gharama za uendeshaji toka serikalini na 50% - 100% ya gharama hizo za uendeshaji toka ktk makanisa. Na hapa ndipo ninaposema kuwa inabidi watu wa dini nyingine ikiwa ni pamoja na waislamu washukuru makanisa maana yanatoa pesa zao kuwahudumia kwa njia ya matibabu na ajira.

>>Sasa ili haya yote yatekelezeke, yaani ya kutokutaifisha hizo hospitali na kutoa huduma kwa bei kama hospitali za umma ilibidi yawekwe kwenye makubaliano, yaani MOU. Sasa kwa bahati mbaya Mashirika mengine ya binafsi, NGOs na madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu, Waislamu n.k miaka hiyo ya 90's hawakuweka kipaumbele ktk huduma za kijamii kama afya na elimu. Hawakujihusisha na utoaji sana wa huduma za kijamii kama kujenga hospitali au shule. Kwa hiyo hawakuwa na hospitali zenye hadhi ya wilaya, mikoa na za rufaa ambazo zingewafanya wawe sehemu ya MOU. Ndo maana kwa miaka ya 90's wao hawakuhusika ktk MOU. Ila kwa miaka ya hivi karibuni NGO na madhebu ya dini nyingine yameanza nayo kujihusisha na utoaji wa huduma za kijamii ila kwa kiasi kidogo ukilinganisha na madhehebu ya dini ya Kikristo. Kwa hiyo hoja si kuchukia MOU au kuwachukia wakristo kwa sababu ya MOU. Lazima tuangalie na sababu zilizopelekea kuwepo kwa MOU na wengine kutokuwemo kwenye MOU.
>>Lakini pia kama hoja ni kupewa ruzuku za kuendesha hospitali, basi Waislamu, NGOs na dini nyingine nazo zijenge hospitali mahali ambapo kwanza serikali haina hospitali au zijenge hospitali kubwa ukilinganisha na hospitali za umma ktk maeneo husika ili ziingizwe kwenye mpango wa kupewa ruzuku ili zitoe huduma kwa bei nafuu kama hospitali za umma na za Makanisa. Lakini si kueneza chuku tu na uhasama wa kidini pasipo sababu. Au kama wanaoeneza chuki wana hoja wanipe hata hospitali kubwa yenye hadhi ya hospitali ya wilaya, mikoa na rufaa hata moja iliyojengwa na waislamu, NGOs au wahindu miaka ya 90's mahali ambapo serikali haikuwa na hospitali au ilikuwa na hospitali ndogo ukilinganisha na hospitali ya dini au NGO hizo ili waseme serikali iliwatenga kwenye MOU.

 
Mama POROJO ni Mfuasi na shabiki mkubwa wa mtuhumiwa mmojawapo wa wanaotaka kuisambaratisha CHADEMA.Soma post zake za Nyuma.

wewe tatizo lako unatumia kichwa kufugia nywele,badala ya kuchangia hoja katika mjadala unaanza kutueleza habari za mtu binafsi, punguza njaa hiyo mkuu.simama kwa miguu yako
 
kaka Mpenda.Haki umeeleza vizuri na kitaalamu sana, lakini naomba nikumbushe kitu kimoja ambacho najua hata wewe unakielewa. watu wasifkiri kina sadeeq, kina mzee mohamed Said na wengineo hawaujui ukweli huu bali ni kwamba wanaujua vema sana ila kwa kujua waislamu wengi hawajasoma sasa wanatumia mbinu ya blanketi la dini za kikoloni kuwachochea vijana wa kiafrika, wa kitanzania, kwa kuwalisha uongo, brainwashing, ili vijana wa kitanzania tuwachinje mama zetu na baba zetu, na wakati tunatumbua hayo matumbo ya mama zetu wao watapanda ndege kwenda saudia kula bata. kwa hiyo wanajua ila wameamua tu kutunyea uchafu wao kwa makusudi yao maalumu. ndo maana wengine humu tumeamua kuwa hawa hamna haja ya kupoteza mda kuwapa maelezo ya kitaalamu ila ni kuwangojea tu watunyee. wakitunyea mavi sahani moja sisi tunawanyea debe nzima, daadake..jino kwa jino tu. tumeshawageuzia shavu zote na makofi wametutwanga sana, sasa ni kuwapasukia tu waabudi fikra za kikoloni hawa...no cavity, enough is enough![/QUOTE]


Ndugu yangu Moshdar, ni kweli waislamu wanaujua ukweli ila tu tamaa, ubinafsi na kutaka kuleta udini ktk nchi hii ndo vinawasukuma kuwachochea vijana ambao hawajui hata hiyo MOU ilikujaje licha ya ukweli kuwekwa bayana. Lakini hawa ni wa kusamehewa tu maana hawajui walitendalo. Kisasi ni juu yake Bwana; kwa hiyo kisasi tumwachie yeye aliyezifanya mbingu na nchi.
 
UILAM NA ITIKADI YAKE DHIDI YA WAKRISTO. ANACHOCHEA VIONGOZI WA KIKRISTO WAUWAWE NA MPAKA SASA HAJAKAMATWA. JEURI HII ANAIPATA WAPI.
 
Last edited by a moderator:

Ndugu yangu umeona: watu ni wagumu kuelewa. Hasa pale wanapokuwa na ajenda zao.
 
Nadhani hukumuelewa Dr. Slaa. Shirika hilo linapata misaada toka mashirika ya kidini ya Ujerumani si serikali ya Ujerumani.
Ndipo nilipokuwa ninamtaka (Mwana Ukweli) tuwafikiane hapa ili tuanze kutiririka lakini wapi!

Anyway nafikiri kuna haja ya hili shirika nalo liombwe kutoa ushirikiano ili tupate baadhi ya maelezo kutoka kwao.
 
Ndipo nilipokuwa ninamtaka (Mwana Ukweli) tuwafikiane hapa ili tuanze kutiririka lakini wapi!

Anyway nafikiri kuna haja ya hili shirika nalo liombwe kutoa ushirikiano ili tupate baadhi ya maelezo kutoka kwao.
Ni kulekule kukosa pa kushikia sasa mnatapatapa. Mashirika yapo mengi na yalikuwa yanasaidia katika huduma hizi tangu tunapata uhuru. Hata mkipewa maelezo kutoka kwa hayo mashirika mtaanza kutafuta maswali mengine...ndivyo mlivyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…