Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

nafikiri ufunguke zaidi na kuzidi kuliangalia suala hili kwa mapana yake. Jiulize kwanini Serikali imerudisha maskuli na mahospitali tu. Kwanini haijarejesha majumba na mashamba kama yale ya mkonge kwa wamiliki wake wa awali au majumba kwa wenyewe. (Kumbuka Serikali ilitaifisha mpaka majumba na kuyakabidhi kwa MSAJILI WA MAJUMBA ambayo sasa mnaita Shirika la nyumba. Anzia hapo kisha endelea na masuala yangu ya awali.

wewe ndo utueleza kwa nini haikurudisha hayo majumba. kama hujui basi wa kuiuliza ni serikali na si wana-JF. For this particular question of yours the burden lies on you not others. kwa nini unamtaka mwenzio ndo akuambie? unataka ufanyiwe tu kila kitu. wewe sema halafu tutachambua na kujadili.
 
Mimi naamini wazi Dr Slaa ni msomi ingawa amebobea katika mas'ala ya sharia za kanisa katoliki lakin tunaamini kuwa ana Ph.d. Na msomi yoyote siku zote anapokuja na uchambuzi kama huu si vizuri kuandika historia bila kuweka SULUHISHO. Historia siku zote inajirudia. Tunajuwa wakti wa mchakato huo Dr Slaa alikuwa ni KATIBA WA TEC na ndiye aliye alyekuwa kiungo kikubwa katika kufanikisha MoU hiyo. Historia ya sakata hili inaanzia kwenye Azimio la Arusha ambalo kwa wakti huo 1967 lilikuwa na kila sababu ya kutaifisha skuli na mahospital hayo na kuyafanya yawe ya umma. na vile walitaifisha hata majumba na kuikabidhi MSAJILI WA MAJUMBA amnayo siku hizi mnaita SHIRIKA LA NYUMBA. Kwa kadri miaka ilivyokuwa inakwenda Serikali ikashawishika na kushawishiwa kurudisha maskuli na mahospital hayo kwa wenyewe na factor kubwa iliyotumika kurahisisha hilo ndio HIZO SABABU ALIZOZITOA Padre Slaa. Lakin hakugusia kuhusu majumba na hata baadhwi ya mashamba yaliyotaifishwa na Serikali na kushindwa kuendelezwa badala yake yakauzwa . Mfano mashamba ya mkonge kule tanga. Lakin Suala la msingi kwake. Je sababu hizo za Serikali yenu kuendelea kukodi maskuli hayo na mahospitali hayo ipo mpaka leo?

iulize hiyo serikali yako. kwani wewe hukuichagua hiyo serkali? na hata kama hukuichagua ndo yenyewe sasa ipo madarakani, kodi inakutoza, sasa kinachokuzuia kuihoji ni nini? kwa nini unataka sisi tujibu maswali yanayopaswa kujibiwa na serikali? kwani kanisa ndo linamiliki mashamba ya mkonge au hayo majumba? na wewe fanya kazi, amka katafute majibu, no one has time to babysit you.
 
Duh!

Ama kweli ****** mna mambo!

Hamlali?

sasa kuna watu wanataka kubadilisha maneno mara ohh Ujerumani mara ohhh sijui nini

waislam walipopeleka MoU yao ambayo ilikuwa ilikuwa sawa na hii wakaambiwa ohhh fanyeni Subra kwanza kuja kushtuka too late.

Mimi naona badala ya kubishana kila mmoja apige madili kivyake au mnasemaje maana hapa ni ngumu kutaka FAIR PLAY wakati the entire game is UNFAIR

kuna kitu unataka kusema lakini ukakizuia hivi em sema tena
 
mUNGU KAWAONYESHA MAPEMA KINACHOMSIBU DK SLAA HATA KUFIKIA UAMUZI WA KUGOMBEA URAIS. NI UDINI UDINI TU HAAN JENGINE
 
dr kumbe unajua kubomoa ni sekunde na kujenga inachukua muda.
Mbona kila kukicha unahamasisha migomo na maandamano na kuhatarisha amani ya nchi yetu?
JE, UNAIJUA THAMANI YAKE?
.

unaongelea dhana sahihi lakini unaipa jina si stahiki ili ufarakishe. wewe unachanganya kati ya migomo na maandamo na vuguvugu la mabadiliko a.ka M4C. Migomo na maandamo vilimuua osama na sadam lakini vuguvugu la mabadilko limemfanya Mzee Nelson Mandela kuwa shujaa wa dunia.. umeona tofauti sasaeeeee?
 
We unaumwa kweli, tena unaumwa wazimu. Ni msaada gani OIC inatoa zaidi ya tende na nyama za kondoo wakati wa Eid-Alhaji?

Hebu kabla hujaongea utumbo zikague hizo nchi wanachama wa OIC halafu jiulize wana nini. Hivi Uganda na Mozambique wanasaidiwa nini na OIC? Kama una mipango ya kufanya ugaidi sawa, lkn kama ni Elimu, Afya na Maendeleo hiyo hamna. Idadi ya vyuo vikuu katika nchi zooote za OIC ukijumlisha pamoja ni sawa na vyuo vikuu vya India.

Yaani unataka kuniambia kuna sababu ya kuionea gere Somalia?! Poor you. Sisi wengine hatuli nyama za kondoo any way

ungefuatilia comments zangu kwenye huu mjadala wala usingeandika uliyoyaandika. mimi sikuzote nitasimamia maslai ya wote awe mkristu, mwisilamu, mhindu, mbudha au mpagani. na ninarudia tena kama OIC wanatoa misaada basi MOU kati ya waisilamu na Serikali usainiwe kwa manufaa ya Watanzania wote kama vile MOU ya kanisa na Serikali unavyonufaisha watanzania wote.
 
Dr acha kufumba fumba watu macho kwa maneno yako kichwa cha mkataba kinatosha kubashiri nini hicho?kinahusu nini? Kwa nani na nani? Na kipi kilichopo ndani?
Hembu rudia kukisoma na dictionary pembeni.

dont judge a book by its cover dude, go inside, analyse, scan. tatizo ninyi likishakuwa suala la kusumbua ubongo kidogo tu basi hamtaki. yan mnataka vitu viwe tu lainiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kama mnanawa, halua halua tu. yaan wewe ukishasoma lile kava baaaaaaasi unaconclude wakristu wanapendelewa. haya kwa stahili hiyo utaweza kweli kuhoji kwa nini unadanganywa uvae mabomu ya kulipua binaadamu wenzako?!
 
Tatizo kuna watu ndio wanaanza kupata elimu ya mambo ya ulimwengu hivi karibuni,,,wanasahau hapo awali wali delay kwenye kupigania udini wanazinduka wanaanza lawama,,someni kwa bidihi ili mpate kazi muwe wengi sio kila kukicha takwimu zinasemaje ,,shule wavivu,
 
Namshangaa mtu anapoanza kufanya uchambuzi wa idadi ya waislamu na wakristo serikalini,hivi zinapotangazwa nafasi za kazi huwa wanasema dini gani waombe?Kama ni za uteuzi nani anateua?na anakuwa amepewa mamlaka na nani kuteua kama siyo na rais?Nafasi gani ni kubwa zaidi ya rais ambaye pia ni Mwislamu?mbona hamuijadili hiyo?Mwisho wa siku kama huna elimu ya kutosha kushindana na wenye elimu soma zaidi na si kuleta majungu na chuki zisizo na msingi
 
pADRI ni PADRI hata aingi kwenye siasa atabaki kuwa padri. SASA NAAMINI KINACHOMPOZA ZITTO KaBWE CHADEMA. washukuru waislam kumuonyesha mapema dk slaa kilichopo moyoni mwake. wangalijaribu kumpeleka Ikulu mengi yangaliwakuta. mungu hamfichi mnafiki.

hapo red, naskia jamaa anajitapa kuwa akiwa huko huko kighoma, anao uwezo wa kuuwa panya wote nyumbani kwangu huku lindi bila hata kulazimika kufika nyumbani kwangu. kwa kuwa ni rafikiyo vip waweza kujua anatumia technolojia gani?

kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kuwa huko CDM zito lazima ataponzeka tu ikiwa hatabadilika kwani kule jamaa kila saa wao wanamtaja tu Mungu Mungu kuwa ndo kimbilio lao, Ukiaacha zito sjaskia mwingine anayesema anategemea tunguli wala jini. sasa unaona jamaa lazima watofautiane kwa sababu mmoja anatumia giza(zito) katikati ya kundi(CDM) linalotumia mwanga.
 
Mimi naamini wazi Dr Slaa ni msomi ingawa amebobea katika mas'ala ya sharia za kanisa katoliki lakin tunaamini kuwa ana Ph.d. Na msomi yoyote siku zote anapokuja na uchambuzi kama huu si vizuri kuandika historia bila kuweka SULUHISHO. Historia siku zote inajirudia. Tunajuwa wakti wa mchakato huo Dr Slaa alikuwa ni KATIBA WA TEC na ndiye aliye alyekuwa kiungo kikubwa katika kufanikisha MoU hiyo. Historia ya sakata hili inaanzia kwenye Azimio la Arusha ambalo kwa wakti huo 1967 lilikuwa na kila sababu ya kutaifisha skuli na mahospital hayo na kuyafanya yawe ya umma. na vile walitaifisha hata majumba na kuikabidhi MSAJILI WA MAJUMBA amnayo siku hizi mnaita SHIRIKA LA NYUMBA. Kwa kadri miaka ilivyokuwa inakwenda Serikali ikashawishika na kushawishiwa kurudisha maskuli na mahospital hayo kwa wenyewe na factor kubwa iliyotumika kurahisisha hilo ndio HIZO SABABU ALIZOZITOA Padre Slaa. Lakin hakugusia kuhusu majumba na hata baadhwi ya mashamba yaliyotaifishwa na Serikali na kushindwa kuendelezwa badala yake yakauzwa . Mfano mashamba ya mkonge kule tanga. Lakin Suala la msingi kwake. Je sababu hizo za Serikali yenu kuendelea kukodi maskuli hayo na mahospitali hayo ipo mpaka leo?

1. Barubaru mbona hutumii akili ndugu yangu?
2. Dr Slaa ameelezea upande ambao yeye mwenyewe alishiriki na si upande wa watu wengine. Kama unataka habari za majumba au mashamba ya mkonge Tanga si waulize waliosimamia huo ubinafsishaji. Kwani hayo majumba na mashamba yalibinafsishwa na Dr Slaa? Yeye ameelezea kwa upande wa TEC (mambo yanayohusu upande wa makanisa) na mtu mwingine aliyekuwa serikalini naye angeelezea upande wa pili. Mbona unakuwa 'narrow minded' hivyo hata unashindwa kuelewa kinachozungumzwa? Maana kama angeelezea upande wa pili ungehoji pia kama yeye ndiye msemaji wa upande huo. Yaani maswali mengine yanakatisha tamaa kabisa!
3. Nikuulize Waarabu walipokuja Zanzibar au Tanganyika walijenga shule na hospitali ngapi? Sitaki nyingi nipe mbili 2: Zanzibar 1 na Tanganyika 1.
 
Baadhi ya watu humu JF wanataka Dr. Slaa aeleze ya BAKWATA. Dabala ya kuwauliza BAKWATA. BAKWATA (ingawa baadhi ya waislam hawaitaki na hawasemi wanataka nani) ndiyo waulizwe..
 
Mjadala huu umetoa picha halisi jinsi gani walimu wa shule ya msingi especially wa darasa la kwanza wanavyopata tabu kuwafanya wanafunzi waelewe. Sasa kama watu wazima na elimu zao inakua ngumu namna hii kuwaelewesha inakuaje kwa mtoto wa darasa la kwanza

Kama umejengewa mazingira ya kulalamika toka wakati uko mdogo basi hutakosa sababu ya kulalamika. Tunaona hapa baadhi ya wachangiaji wanaoipinga MOU wameelewa vizuri ila tatizo hawataki kukubali kama wameelewa matokeo yake wanatafuta vijisababu vingine ( mfano kuna mtu analeta habari ya mashamba ya mkonge). Sasa watu kama hawa kwavile tushawajua hakuna haja ya kuendelea kubishana nao.

Serikali kwa upande wake ina matatizo makubwa sana na sintofahamu yote hii imesababishwa na serikali. Huu ufafanuzi wa MOU ungetolewa mapema na serikali basi kusingekua na mijadala hii badala yake wale wenzenu wenye malalamiko yasioisha wangetafuta lalamiko lingine
 
Mbona serikali imenyamaza ili hali kwenye tamko la maaskofu wakitaka serikali itoe ufafanuzi juu ya hili?Ukimya wa serikali juu ya hili inamaanisha wasemacho waislam wako sahihi,kwani mkataba uko wazi.Kila mwenye akili anaelewa,
Hivi serikali imenyamazia mangapi? Unashangaa? Mbona hawajatoa tamshi kuhusu jamaa aliyemteka Ulimboka? Mkataba umewekwa hapa. Dr. Slaa ametoa ufafanuzi. Unataka nini zaidi ya hayo? Waislamu wanaolalamika wamebugi.
 
unamaanisha mungu yupi,manake mungu kila mtu ana wake kuna wengine mungu wao ng'ombe,wengine anawatoto,wengine anakufa anafufuka,wengine mizimu,wengine......nk
hapo red, naskia jamaa anajitapa kuwa akiwa huko huko kighoma, anao uwezo wa kuuwa panya wote nyumbani kwangu huku lindi bila hata kulazimika kufika nyumbani kwangu. kwa kuwa ni rafikiyo vip waweza kujua anatumia technolojia gani? kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kuwa huko CDM zito lazima ataponzeka tu ikiwa hatabadilika kwani kule jamaa kila saa wao wanamtaja tu Mungu Mungu kuwa ndo kimbilio lao, Ukiaacha zito sjaskia mwingine anayesema anategemea tunguli wala jini. sasa unaona jamaa lazima watofautiane kwa sababu mmoja anatumia giza(zito) katikati ya kundi(CDM) linalotumia mwanga.
 
Hivi serikali imenyamazia mangapi? Unashangaa? Mbona hawajatoa tamshi kuhusu jamaa aliyemteka Ulimboka? Mkataba umewekwa hapa. Dr. Slaa ametoa ufafanuzi. Unataka nini zaidi ya hayo? Waislamu wanaolalamika wamebugi.

Tukiangalia ukweli halisi juu ya umiliki wa mahospital na huduma za afya nchi, sio tatizo kwa mazingira ya sasa Serikali kuendelea kutoa ruzuku katika mahospital ya taasisi za kidini. Labda ingekuwa vizuri uigo huo ukapanuliwa na kuhusisha taasisi zote zisizo za kiserikali zinazomiliki mahospital na vituo vikubwa vya afya nchi. Yawezekana kutokana na uchache wangu wa taarifa nikawa sina ufahamu sana namna serikali inavyosaidia taasisi nyingine zisizo za kiserikali zilizowekeza katika huduma ya afya. Nachotaka kusema hapa ni kwamba badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusainiwa MOU katika ya serikali na taasisi hizo ni bora suala hili likatamkwa katika sheria. Kutamkwa kwa suala hili katika sheria kutaona hisia za kidini zinazojitokeza. Maana, kama sheria ikitamka rasmi haki ya mahospitali ya taasisisi zisizo sa kiserikali yakiwemo mashirika ya kidini kupata ruzuku na ikaweka vigezo maalumu, hapatakuwa na mwanya wowowte wa kulitizama suala hili katika jicho la kidinidini. Litatizamwa kama suala la kawaida la huduma za afya bila kujali nani anatoa huduma hizo ili mradi zinawanufaisha watanzania.

Nikirudi katika huduma za kiafya, mimi naona maafikiano yaliyomo katika MOU hayakidhi matakwa ya mazingira ya sasa kwa sababu kadhaa. Kwanza, maafikiano ni ya kiujumla sana. Hayatoi ufafanuzi huduma za elimu katika hatua gani na wala hayaweki wajibu katika taasisi za kidini. Ni vigumu kujua kama ruzuku inapaswa kutolewa kwa vyuo vikuu, sekondari au shule za misingi? Je itahusu shule zinazotoa huduma kwa watu wote au hata shule za seminari zinazotoa huduma mahususi kwa waumini wa dhehebu husika? Je Serikali kwa kutoa ruzuku itakuwa na haki kwa mujibu wa walipa kodi kudhibiti ada zinazotolewa na mashule yanayomilikiwa na taasisi za kidini? Sababu nyingine ni kwamba kutokana na kuwepo mashule mengi ya sekondari ya kata na mengine yanayomilikiwa na taasisi zingine za kidini zisizo za kikistristo, suala la serikali kutoa ruzuku katika mashule na vyo vya elimu vya kidini halina maana ile ile ambayo pengine lingekuwa nayo katika miaka ya 80. Ni bora hizo pesa za ruzuku zikatumika kuboresha shule za kata ambazo huko mbeleni zinaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa walala hoi na watoto wa wakulima.
 
unamaanisha mungu yupi,manake mungu "kila mtu" ana wake kuna wengine mungu wao ng'ombe,wengine anawatoto,wengine anakufa anafufuka,wengine mizimu,wengine......nk

Hapo red ndipo palipo na jibu la swali lako. na CDM nao ni kati ya hao "Kila mtu". kwa hiyo nao wana Mungu wa kwao na ndo huyo wanayemtegemea.
 
Tukiangalia ukweli halisi juu ya umiliki wa mahospital na huduma za afya nchi, sio tatizo kwa mazingira ya sasa Serikali kuendelea kutoa ruzuku katika mahospital ya taasisi za kidini. Labda ingekuwa vizuri uigo huo ukapanuliwa na kuhusisha taasisi zote zisizo za kiserikali zinazomiliki mahospital na vituo vikubwa vya afya nchi. Yawezekana kutokana na uchache wangu wa taarifa nikawa sina ufahamu sana namna serikali inavyosaidia taasisi nyingine zisizo za kiserikali zilizowekeza katika huduma ya afya. Nachotaka kusema hapa ni kwamba badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusainiwa MOU katika ya serikali na taasisi hizo ni bora suala hili likatamkwa katika sheria. Kutamkwa kwa suala hili katika sheria kutaona hisia za kidini zinazojitokeza. Maana, kama sheria ikitamka rasmi haki ya mahospitali ya taasisisi zisizo sa kiserikali yakiwemo mashirika ya kidini kupata ruzuku na ikaweka vigezo maalumu, hapatakuwa na mwanya wowowte wa kulitizama suala hili katika jicho la kidinidini. Litatizamwa kama suala la kawaida la huduma za afya bila kujali nani anatoa huduma hizo ili mradi zinawanufaisha watanzania.

Nikirudi katika huduma za kiafya, mimi naona maafikiano yaliyomo katika MOU hayakidhi matakwa ya mazingira ya sasa kwa sababu kadhaa. Kwanza, maafikiano ni ya kiujumla sana. Hayatoi ufafanuzi huduma za elimu katika hatua gani na wala hayaweki wajibu katika taasisi za kidini. Ni vigumu kujua kama ruzuku inapaswa kutolewa kwa vyuo vikuu, sekondari au shule za misingi? Je itahusu shule zinazotoa huduma kwa watu wote au hata shule za seminari zinazotoa huduma mahususi kwa waumini wa dhehebu husika? Je Serikali kwa kutoa ruzuku itakuwa na haki kwa mujibu wa walipa kodi kudhibiti ada zinazotolewa na mashule yanayomilikiwa na taasisi za kidini? Sababu nyingine ni kwamba kutokana na kuwepo mashule mengi ya sekondari ya kata na mengine yanayomilikiwa na taasisi zingine za kidini zisizo za kikistristo, suala la serikali kutoa ruzuku katika mashule na vyo vya elimu vya kidini halina maana ile ile ambayo pengine lingekuwa nayo katika miaka ya 80. Ni bora hizo pesa za ruzuku zikatumika kuboresha shule za kata ambazo huko mbeleni zinaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa walala hoi na watoto wa wakulima.

1. Soma polepole ufafanuzi wa Dr Slaa utaona kuwa unayouliza ameyatolea ufafanuzi ni kwa nini ilikuwa kama ilivyo kuhusu huduma za jamii kati ya serikali na makanisa au taasisi za kidini. Pengine kama Nyerere asingetaifisha shule za misheni na hospitali tusingekuwa na haya tunayoyasikia leo.
2. Hoja mpya uliyoiongelea labda ni kupanua wigo wa hiyo MoU. Lakini kwa harufu ya udini ambayo imeshaingia sidhani kama makanisa yatakubali tena. Sijui. Ila mimi ningependa MoU ufutwe kabisa na makanisa au taasisi zingine za dini zisijihusishe tena na huduma za jumla za jamii bali iwe serikali yenyewe na kama zitafanya hivyo zifanye kwa waumini wao tu. Mfano, kama Bugando na KCMC zitabaki chini ya makanisa ziwahudumie Wakristo tu au waumini wale wataokubaliana na masharti ya taasisi hizo.
3. Vilevile iwe hivyo kwa shule na vyuo. Vyuo kama Tumaini, SAUT na sekondari zilizo chini ya taasisi za dini nk zitoe huduma kwa waumini wao tu na si kwa wote na kama waumini wa dini nyingine wakienda huko walipe ada zaidi ili kila mtu awe kivyake.
4. Nadhani kwa kufanya hivi tunaweza kupunguza manung'uniko haya maana inakera hasa kwa watoa huduma kuona kwamba pamoja na jitihada zote wanazozifanya bado kuna kundi fulani la watu wanaona wanabaguliwa na huduma hizo na haziwanufaishi kwa lolote.
 
Tukiangalia ukweli halisi juu ya umiliki wa mahospital na huduma za afya nchi, sio tatizo kwa mazingira ya sasa Serikali kuendelea kutoa ruzuku katika mahospital ya taasisi za kidini. Labda ingekuwa vizuri uigo huo ukapanuliwa na kuhusisha taasisi zote zisizo za kiserikali zinazomiliki mahospital na vituo vikubwa vya afya nchi. Yawezekana kutokana na uchache wangu wa taarifa nikawa sina ufahamu sana namna serikali inavyosaidia taasisi nyingine zisizo za kiserikali zilizowekeza katika huduma ya afya. Nachotaka kusema hapa ni kwamba badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusainiwa MOU katika ya serikali na taasisi hizo ni bora suala hili likatamkwa katika sheria. Kutamkwa kwa suala hili katika sheria kutaona hisia za kidini zinazojitokeza. Maana, kama sheria ikitamka rasmi haki ya mahospitali ya taasisisi zisizo sa kiserikali yakiwemo mashirika ya kidini kupata ruzuku na ikaweka vigezo maalumu, hapatakuwa na mwanya wowowte wa kulitizama suala hili katika jicho la kidinidini. Litatizamwa kama suala la kawaida la huduma za afya bila kujali nani anatoa huduma hizo ili mradi zinawanufaisha watanzania.

Nikirudi katika huduma za kiafya, mimi naona maafikiano yaliyomo katika MOU hayakidhi matakwa ya mazingira ya sasa kwa sababu kadhaa. Kwanza, maafikiano ni ya kiujumla sana. Hayatoi ufafanuzi huduma za elimu katika hatua gani na wala hayaweki wajibu katika taasisi za kidini. Ni vigumu kujua kama ruzuku inapaswa kutolewa kwa vyuo vikuu, sekondari au shule za misingi? Je itahusu shule zinazotoa huduma kwa watu wote au hata shule za seminari zinazotoa huduma mahususi kwa waumini wa dhehebu husika? Je Serikali kwa kutoa ruzuku itakuwa na haki kwa mujibu wa walipa kodi kudhibiti ada zinazotolewa na mashule yanayomilikiwa na taasisi za kidini? Sababu nyingine ni kwamba kutokana na kuwepo mashule mengi ya sekondari ya kata na mengine yanayomilikiwa na taasisi zingine za kidini zisizo za kikistristo, suala la serikali kutoa ruzuku katika mashule na vyo vya elimu vya kidini halina maana ile ile ambayo pengine lingekuwa nayo katika miaka ya 80. Ni bora hizo pesa za ruzuku zikatumika kuboresha shule za kata ambazo huko mbeleni zinaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa walala hoi na watoto wa wakulima.

si vibaya kuboresha MoU kwa sababu after all MoU hiyo si msahafu kma ile misahafu ya kudanganyia watu ya ki-atheist. Its a real thing so changing time, enviroment and circumstances might definitely call for a review and posibly a revision. tatizo kwa nchi yako hii ya kifisadi nani ana mda wa kujishughulisha na reasoning na mikakati ya namna hiyo wakati gesi ya kuiba kupata pesa ya haraka haraka imeshapatikana hapo kusini? ukweli, kuwa kunahitajika utendaji makini wa ku-review, na if necessary ku-revise si tu MoU hii bali MoU nyingi tu zinatumika kuiba raslimali zetu, upo wazi. Tatizo ni kuwa wa kutenda nani? usifocus kwenye vitu, focus kwenye mtengeneza vitu. wengi wetu humu tukipewa kampuni za bakheresa tuziendeshe tutaziua kesho. nachtaka kusema ni kuwa cha thaman hapa si zile kampuni za bakhersa bali cha thamani ni bakhersa na timu yake ya menejiment kupitia zile skills walizonazo. tanzania ya ccm tuna nchi yenye vitu tumekosa watu wenye ujuzi na maarifa. ukitaka haya mawazo yako yafanyiwe kazi unatakiwa urudi nyuma uweke kwanza msingi kwa kuwa na watu wenye ujuzi na maarifa halafu hao watu ndo wafanyie kazi hivo vitu unavyovitaka vifanyiwe kazi. Kwa kuwa kila ushahidi unaonesha kinagaubaga kuwa watu hao WENYE UJUZI NA MAARIFA SI CCM basi nafikiri tunajua, pasi na shaka yoyote, kuwa watu hao ni kina nani.
 
Back
Top Bottom