Nimecheka sana mkuu. Ni kweli hatuoni kwenye historia mababu zetu wakiwa kwenye vita vya dini lakini ni fact kwamba waliuana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya imani potofu.
Ni halali kwa watu kuuawa katika siasa kwa sababu wanapigania maslahi fulani?
Inachopigania dini yangu inaonekana kutoka kwenye matendo yangu. Kama ni kuhubiri amani/upendo/kusaidia jirani/yatima/wajane ,kuondoa madhila/malazi/ukosefu wa elimu kwa kuweka huduma husika za jamii nk au kama ni kuhubiri chuki,vita,kuchoma nyumba za watu za ibada, malalamiko , visasi nk utayaona yote kupitia matendo.
Kwani unafikiri ukifuta hizi dini za Uislam na Ukristo ukabaki na waabudu jiwe/mlima/majoka/mibuyu ndiyo utabaki salama kwa mazingira yetu ya sasa?
Solution ni ndogo tu. Kuheshimu anachoabudu mwenzako. Hata kwenye siasa ni hivyohivyo kila mtu na chama chake, hata kwenye Elimu ni hivyo hivyo hatuwezi kusoma wote kitu kimoja, hata kwenye mpira ni hivyo hivyo hatuwezi wote kushabikia timu moja. Dunia sasa imekuwa kijiji na ni lazima kuvumiliana...Wale dini zao zinazowaruhusu kutishia watu au kuua watu ,akili yetu iliyokuwa brainwashed na elimu ya kikoloni inatuambia wanafanya uhalifu na wanastahili kuchukuliwa hatua na vyombo husika. Sheria zetu(tulioziazima kwa wazungu) ndiyo zinasema hivyo. Wewe unajua na mimi ninajua. Ndiyo maana kuna baadhi ya viongozi wa kidini wapo rumande sasa hivi.