Hili siyo ombi bali ni tamko kuelekezwa serikali ya Tanzania kuhusu MoU ya serikali na kanisa.
Tunaitaka serikali ifute MoU hiyo na fedha zinazopelekwa kanisani zielekezwe kwengine.
Kwa sasa Tanzania ilipofikia hakuna sababu ya kubaki na kutimiza yaliyomo kwenye MoU hiyo. Ikiwa huduma za afya, hakuna hospitali isiyotoza pesa kwa huduma hizo. Kwa hiyo serikali haina tena sababu ya kuelekeza pesa hospitali za kanisani.
Ikiwa ni elimu, Tanzania imetangaza elimu bure kwa wote mpakamwanafunzi anapofikia kiwango cha elimu kwa kukopeshwa. Na hapa hakuna tena sababu ya serikali kuelekeza pesa kwa watoa elimu wa kanisa.
Soma zaidi:
-
MoU kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini
-
Kweli huo mkataba kati ya serikali na mashirika ya dini hauna ukomo wakati wenyewe wanatoza pesa raia kwenye hizo hospitali na shule zao?
Nionavyo binafsi:
Tungeendelea na mjadala wa UBORA dhidi ya USIVYOBORA mkataba husika.
Huku kwingine tunaenda kukata miti tuliyokalia na haitatusaidia. Tunapoteza mwelekeo, nguvu na nyenzo.
Ukimnyooshea mwenzio vidole, vingine vinakusonta wewe pia na ukitaka kumtafuta nyoka anzia miguuni kwako. Hakikisha usafi wako si wa kutilia mashaka.
Tutafakari:
East Africa Muslim Welfare Society(EAMWS) kwenda BAKWATA.
Ilikuaje?
1: BAKWATA iliundwa kwa msaada wa nani?
2: Kulikuwa na kujikwaa au kusimama kulingana na misingi husika kiislamu?
3: Ni nani alaumiwe au apongezwe?
4: Chuo kikuu cha TANESCO kiligeukaje kuwa taasisi rasmi ya dini?
5: Je Serikali haina mahusiano na taasisi za kiislamu kweli?
Ismailia ni watu gani? Unajua miradi yao?
6: Je tumechagua vyema ushiriki wetu na Serikali uwe wa namna gani?
7: Je huduma zitolewazo huhitaji cheti cha ubatizo kuzipata kwa ulinganifu?
8: Shule za jumuiya za chama tu imekuwa shida kuziendesha, katafute kwa nini waliona MOU ni njeama kuliko kuchukua miradi husika?
9: Kasome kwa nini iliyochukuliwa hapo awali ilirejeshwa na kueekwa MOU.
Wakati mwingine tuingie kanisani kujifunza wenzetu wanajiendesha vipi? Kujenga kanisa/kujijengea uwezo kwa miradi husika ndani ya uwezo wao kabla ya serikali kuingia ndani.
Tusikurupuke na tusiyumbishwe na vitu vidogo tukajikata miguu.