Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Nimechek hizi document ni void, the Lebulu's signature has been forged its not a real an kwa anayefahamu sahihi za maaskofu huwa zinaambatana na nini atajua nini ninachoongelea

RayB a void document is a document which is either has not been signed by each parties to the agreement, contains forged materials or signature and contain dates not yet reached. Sasa hii document just because it missing something that you believe is a traditional to your belief of complete signature I think you are mistakenly wrong. Mshaona mmekabwa koo sasa na isingelikuwa waislamu kuipata hii MOU wala msingelisema kitu lakini imeshapatikana mnataka kuikana kama void kuonyesha mlikuwa hampati kitu. Let me advise you one thing waambie waliosign baadhi yao kama kina Edward Lowassa wako hai wakanushe basi itasaidia sana hilo na evidence zitakazofuatia pia wakanushe.
 
Halafu watu wakizungumzia mahakama ya kadhi tu, inakuwa 'udini'. Hii nchi italipuka siku moja kama watu hawataanza kuambiana ukweli kuanzia sasa. Unaweza kuikandamiza jamii kwa muda fulani lakini huwezi kuendelea hivyo daima, maana kila uchao watu wanasoma na wanakuwa na awareness ya haki zao. Kuna mtu humu humu mwenye JF amesema Kikwete ni mdini kwa vile kuna Waislamu wengi kwenye baraza lake la Mawaziri. Katika baraza la mawaziri 50 ni 18 tu ni Waislamu, still, some people wanaona ni wengi kwa vile wamezoea kuona zaidi ya asilimia 70 ni Wakristo. Imagine kama ingekuwa nusu kwa nusu, au hao 32 ndiyo Waislamu!
Unaona Ivory Coast? Nchi yenye asilimia 60 ya Waislamu na miaka yoooooote ya Houphouet Boigny walikuwa kimya. Unaona sasa? Wee Joka Kuu acha porojo....imagine MoU hiyo ilikuwa na Waislamu ungesema pumba unazosema sasa?
 
Unapokoment uangalie coz wanajf tunasoma coments zako na tunakujudge wat kind of person u are! Some of us ar not ready to b honest just for the sake of our nation yani anapenda kuona other side imeegemewa lakini kwasabab ye yuko juu anatetea ili aendelee
 
Unapokua umemwelemea mtu for a long time he gets tired na lazima tu atareact, sasa huyu mtu anaporeact inabdi uwemdogo coz ukiendelea ishu zitakua otherwise na ucombee reaction za aliechoka coz he wont get tired again mpaka kieleweke..!
 
Sijaona kwa nini kuwe na malalmiko yoyote, MoU hii inaweza kuwa na jumuiya ya kiislamu , kama na wao wangeomba wasingekataliwa. Hii ni suala la dini husika kutafuta ku-lobby government. Hakuna aliyewazuia waislamu kuingia makubaliano kama haya na serikali katika kutoa huduma ya afya na elimu kwa wananchi.
Good idea!, ila kuna vitu viwili au zaidi vya kuangalia hapa
1. kuna uhakika gani kuwa huu mkataba ulikuja kuwepo baada ya makanisa kufanya lobbying kwa serikali na si serikali ililobby makanisa
2. kama serikali ilikuwa na good will ya kutowatenga wengine na kama inajua kuwa mikataba ya namna hii ni muhimu sana katika kuzisaidia taasisi za kidini kwanini isingekuwa makini kabla ya kusaini na ikajaribu kuangalia mazingira ya nchi kwa upande wa kidini yalivyo
3. waislamu walishawahi kuomba kujiunga na OIC na kuwa na Kurudishiwa mahakama ya Kadhi lakini mpaka leo hakuna hata moja lililotekelezwa, kuna uhakika gani kuwa Waislamu kama nao wangeomba mkataba wa aina hii wangepewa.
in fact unapocomment u need also to know the political and religious set up ya nchi ilivyo.
 
The Game...what game are you putting forward here? udini? naomba utuwekee proposal ya waislamu au dhehebu lingine iliyowapelekea serikali na ikakataliwa, otherwise go to hell na sumu yako! unless game haushi Tanzania hii au upo Tanzania lakini hujatembea sehemu nyingi za Tanzania hii. miaka mingi iliyopita na hata sasa, taasisi za kijamii za kikristo (elimu na afya) zimefanya kazi kubwa sana bila ubaguzi wa aina yoyote ile.
 
The Game...what game are you putting forward here? udini? naomba utuwekee proposal ya waislamu au dhehebu lingine iliyowapelekea serikali na ikakataliwa, otherwise go to hell na sumu yako! unless game haushi Tanzania hii au upo Tanzania lakini hujatembea sehemu nyingi za Tanzania hii. miaka mingi iliyopita na hata sasa, taasisi za kijamii za kikristo (elimu na afya) zimefanya kazi kubwa sana bila ubaguzi wa aina yoyote ile.

So kufanya kazi kubwa does it justify favorable terms from the government? Kwanini wasiwe fair na kuruhusu jumuiya zote zikafaidika na MOU hiyo? Unajua kwani Game Theory aliiweka hapa hebu soma mjadala kwanza kabla ya kucomment kuna watu walikuwa wakipinga kuwa hakuna kitu kama hicho Game theory akawaletea ikabidilika mjadala na kuwa sasa justification kwani huo mkataba upo. Sumu huja pale kundi la watu wanapokuwa greedy na kutaka kuwa bora kuliko wengine. Sumu huanza pale kunapoanza kuwapo unfairness katika utendaji. Sumu wameianzisha wenyewe wakristo walioshiriki katika hii kitu hakuna kumlaumu Game Theory hapa
 
Mkataba wa Kanisa na Serikali waanikwa

Mwandishi Wetu - Julai 22,
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete, imezidi kuingiwa na misukosuko inayogusa waumini wa dini mbalimbali, na sasa kumeibuliwa hati ya makubaliano (MoU) ambayo Serikali iliingia na makanisa nchini. Makubaliano hayo yalikuwa hayafahamiki kwa Watanzania wengi.

Hati hiyo, ambayo Raia Mwema imepata nakala yake, iliandaliwa na Profesa Costa Mahalu alipokuwa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Katika hati hiyo, iliyotiwa saini Februari 21, mwaka 1992, upande wa serikali uliwakilishwa na mmoja wa mawaziri wake waandamizi wa wakati huo......

Pamoja na kuelezwa kwamba hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa dini kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake, hali ya sasa ni ya pekee tokea kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995, jambo ambalo linakiweka Chama cha Mapinduzi (CCM) katika wakati mgumu zaidi.
hs3.gif
Na sababo hiyo ndiyo iliyompelekea Profesa Dr. Mahalu kupelekwa Italy kama balozi ili iwe rahisi kwake kutekeleza masuala yale nyeti mpaka ilipotokea bahati mbaya kile kiasi alichochota kwenye jengo la ubalozi na kukipekeka kule mahala...... leo ana kesi na itaisha kinyemela kama ilivyo kawaida kwani ile ni mission!
 
..ndugu zangu msipige kelele sana manake Bakwata imekuwa inafadhiliwa tangu miaka ya 60 ilipoanzishwa.

..vilevile mahakama ya Kadhi itabidi ipewe fedha kwa mtindo wa mou kati ya Waislamu na serikali.

..jambo la maana hapa ni Waislamu kujizatiti nao waanzishe hospitali na vyuo vya elimu dunia ambavyo vita-qualify kupewa msaada na serikali.

..mou imesainiwa mwaka 1992, tena Raisi akiwa Mzee Mwinyi, waziri wa fedha akiwa Alhaj Prof.Malima, sasa tatizo liko wapi hapo?

..Mkapa naye ni Mkristo lakini kawapatia Waislamu majengo ya serikali wakafungua Chuo Kikuu.

..mimi nadhani UDINI nchi hii haupo, ila kuna watu wanalazimisha tuuu. kuna watu hawaoni raha Waislamu na Wakristo wakiishi kwa maelewano.
 
..ndugu zangu msipige kelele sana manake Bakwata imekuwa inafadhiliwa tangu miaka ya 60 ilipoanzishwa.

..vilevile mahakama ya Kadhi itabidi ipewe fedha kwa mtindo wa mou kati ya Waislamu na serikali.

..jambo la maana hapa ni Waislamu kujizatiti nao waanzishe hospitali na vyuo vya elimu dunia ambavyo vita-qualify kupewa msaada na serikali.

..mou imesainiwa mwaka 1992, tena Raisi akiwa Mzee Mwinyi, waziri wa fedha akiwa Alhaj Prof.Malima, sasa tatizo liko wapi hapo?

..Mkapa naye ni Mkristo lakini kawapatia Waislamu majengo ya serikali wakafungua Chuo Kikuu.

..mimi nadhani UDINI nchi hii haupo, ila kuna watu wanalazimisha tuuu. kuna watu hawaoni raha Waislamu na Wakristo wakiishi kwa maelewano.

Kumbe ni kelele?wtf

Mkapa ni guilt consius ameua waislamu 1998, 2001 akaamua kutoa majengo hadanganyi mtu ...(mpe mtoto pipi ushenzi)

Udini haupo kabisaaaaa nchi kanisa na wakristo wanapata vyeo na pesa udini utoke wapi?

Taasisi ya kidini inapata hela serikalini, misaada ya kimataifa etc wengine OIC no....hakuna udini kabisaa...

Mtabisha wee siku likilipuka I hope kila mtu ataonja sehemu yake
 
..haya ni maelezo ya aliyepata kuwa Katibu wa TEC kuhusu mchakato mzima uliopelekea kusainiwa kwa "mou."


Katibu wa TEC said:
Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

i) Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School( Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2) Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii, b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria, hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) .

Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo.

Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.

Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando). Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo. Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali.

Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa.

Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa.

Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
 
Negotiation is just a negotiation. Wewe ulitaka iweje? Juzi si kumekuwa na makubaliano kati ya taasisi za dini na serikali kuhusu misamaha ya kodi na mambo yakaenda vizuri? Kusingekuwa na makubaliano hayo unafikiri nini kingetokea?

NEGOTIATION IS NOT JUST A NEGOTIATION!!!, tusidanganyane sote tu watu wazima!!! Kama unayosema ni kweli mbona NEGOTIATION kuhusu serikali ya tanzania kujiunga na OIC inapingwa???????!!!!!
 
NEGOTIATION IS NOT JUST A NEGOTIATION!!!, tusidanganyane sote tu watu wazima!!! Kama unayosema ni kweli mbona NEGOTIATION kuhusu serikali ya tanzania kujiunga na OIC inapingwa???????!!!!!
Acha ubabaishaji ndugu........... kwani hiyo MoU imeitaka serikali kujiunga na kanisa kama ilivyotaka kuwa OIC...........???
 
Mimi nitakachofanya hapa ni kuanzisha shughuli nyingi za huduma za jamii, nitafungua mashule, mahosipitali, majumba ya yatima, succos nk. kupitia dini yangu mpya. Halafu nitakwenda kwa mamlaka kuomba MoU, najua watakubali. Nakushauri na wewe ufanye kama mimi. Ya nini wivu usio na maendeleo.
 
Tatizo liko wapi kwenye hii MOU? Sioni tatizo lolote Hospitali na shule zilizoojengwa na zinazojengwa na Makanisa hayabagui dini. Ukienda mkristo ama muislamu unatibiwa. Ukijaribu kuangalia hizi hospitali zinasaidia sana. Nani hajui leo kuwa KCMC ni hospitali inayosaidia watu wa matabaka yote ya Tanzania? Nenda Arusha Medical Center(Selian).
Tuache chuki na vitu ambavyo havisaidii zaidi ya kuligawa taifa vipande vipande.
Mifano ni mingi .Kikwete kasoma kwenye shule zilizojengwa na hayo makanisa na watu wengi tu ambao sio wakristo wamesoma kwenye hizo shule.
 
"The Government shall provide financial asssistance to Church insituttions and shall seek financial assistance to Church run social services in its bilateral negotiations with foreign governments"


Acheni udini someni makubaliano na muyaelewe. Pili, Nivyema kuelewa vitu na historia yake. Don't pick thinks out of context. Kumbuka kufatia mfumo wa ukiritimba wa utoaji huduma ulipo anzishwa na serikali miaka ya '70 kuliathiri sana mienendo ya utoaji huduma kwa wananchi. Katika Maeneo mengi nchini Makanisa yalibaki kuwa tegemeo pekee la kupata huduma hasa huduma ya afya ambayo, tofauti na elimu, haikutaifishwa. Makanisa yaliendelea kuingia gharama kubwa kutoa huduma hiyo na tena kwa bei nafuu bila ruzuku kutoka serikalini. Kufuatia kulemewa na mzigo wa kuhudumia watanzania (wakristo, waislamu, wa dini nyingenezo na wasio na dini) na kufuatia kuwa jukumu la kutoa huduma hizo ni la serikali hapakuwepo budi serikali kuchangia. Na katika kufanikisha hilo razima yawepo makubaliano. Nitatoa mfano

Katika Wilaya ya Muleba, Tangu uhuru mpaka sasa hakuna hospitali ya serikali inayoweza kufanya upasuaji wa kati na mkubwa (mf. operation ya mama kujifungua). Kuna vituo vya afya vitano tu kimoja kati ya hivyo kimoja ndo kinaitwa hospital ya wilaya. Aidha kuna hospital tatu za Makanisa zenye wataalamu na vifaa vya kutoa huduma kubwa za kihospitali na zimekuwa zikitoa huduma tangu enzi hizo. Kwa makubaliano yanayotokana na walaka tajwa, hospitali moja (RUBYA HOSPITAL) imefanywa kuwa hospitali teule ya wilaya. Je, mtoa hoja anaimanisha hapakuwepo haki ya serikali kufanya makubaliano na kanisa ili watanzania wa Muleba wapate haki ya kutibwa na serikali yao? Kuhusishwa kwa bilateral agreements kunatokana na ukweli kwamba baada ya wafadhili kuona ubabaishaji wa serikali katika kutoa huduma na kufuatia vikwazo vilivyo kuwa vimewekwa na IMF na WB kwa Tz wafadhili waliacha kutoa fedha kwa serikali isipokuwa taasisi binafsi au kufadhili miradi ya wananchi moja kwa moja (In most cases there was no longer direct funding of government budget). Hivyo hii ilikuwa nimojawapo ya njia ambazo serikali ilitumia katika kutatua migogoro yake na wafadhili.

Mara kadhaa waislaamu wamekuwa wakitaja MoU hii kwa kuipotosha, kwamba serikali iliuza nchi kwa wakristo, namaranyingine wanaona misaada ya makanisa inawanufaisha wakristo.Hivi waislamu wangependa taasisi zao, ambazo zinahudumia watanzania wote, zisipate usaidizi wa serikali? Je kama waislamu au wahindu etc. wanaendesha ushirikiano wao na serikali kimbumbu, naimanisha pasispo makubaliano ya maandishi, wa kulaumiwa ni kanisa au serikali?

Tofautisheni maslahi ya dini na taifa.

Ushirikiano uliotajwa hapo juu umewanyima waislamu haki gani? Mfano art XI inaitaka serikali kutoa nafasi za masomo kwa walimu wanaotarajiwa kufundisha katika shule zinazomilikwa na kanisa, hii inatatizo gani?! Kama shule hizo zinahudumia watanzania wote mnataka walimu wao wakajifunzie wapi? (nasikia Makamba na JK walisomea kwenye shule za kanisa)
 
Hii MOU imerudishwa jamvini? Nakumbuka enzi zile za Game Theory!
 
Haya ni madogo kuna mengi sana. Na hii ndio maana maaskofu wanapata jeuri ya kuikemea na hata kukataa viongozi waliochaguliwa kihalali na kwa mujibu wa shera za nchi kama vile Meya wa Arusha maaskofu wamesema hawamtambui na hawatashirikiana nae.

Haya sie yetu macho tutaona mwisho wake
.
 
Big up Joka Kuu.

Hauzi kutenganisha mtu na huduma za lazima? Huduma hata kama zime letwa na nani watu hawa chagui.
Wamisionari ndio wa kwanza kuleta huduma kama elimu, mahospitali pamoja na huduma za kiroho.
Sasa hivi wamepanua hizo huduma kulingana na mahitaji ya watu.
Viongozi wote wa anzilishi wamesoma kwenye hizo taasisi. Iweje tuwe na mawazo ya kusema imependelewa.
Mpaka sasa hivyo kama ni huduma bado ni huduma na bora ukilinganisha na za serekali, Serekali lazima ikubali kwa sababu inapungziwa mzigo.
Angalia hata elimu shule bora ni hizo za taasisi . Utatengenasha vipi huduma hiza na jamii mimi naona badala ya kufikiria upendeleo
wa Dini tunge waunga mkono kwa maana wana harakisha maendeleo ya jamii. Tushindane kwa kutoahuduma bora na nzuri. Mbona waislamu hawaongelei watoto wanafanya vibaya sana kwenye Seminari zao?.
Shule nyingi za mwazo ni za taasisi za binfsi, Mahospitali e,g Bugando, KCMC, na hazi wabagui watu kwa dini?
Suala hili la udini lita watafuna watanzania tusipokuwa makini. Naona imewakalia baadhi kwenye mawazo hakuna lolote bila dini.
Dini ni maisha ya kiroho inayo mwelekaza mtu namna na njia ya kupita angali hapa dunia kueleka kwa muumba.
Ni ngeshauri taasisi ziruhusiwe kuendasha huduma za jamii. bila ya ubaguzi wa dini.
Ndugu zangu waislamu tuwe makini na mambo ya udini, tuki endekaza yatatutafuna, tusijifanye polisi wa kuitete serekali.
Kitendao cha kulaamu Maaskofu wa Arusha ni sawa na kwamba mauaji yale yalikuwa haiwa husu waislamu.
Bali zito ni kauli ya Maaskofu.
Mmejiweka sehemu ya Serekali. Hii ni hatari. Tuboresha hudama zetu za jamii mambo ya imani maadili mema tujenayo toka kwenye nyuba setu za ibada watu waone kwa matendo yetu si kwa maneno yetu. Ulimi ni kiungo kidogo lakini la weza angamiza tulinde maneno ya vinywa vyetu.
Tutafute ukweli na halisia badala ya kuparazi. Tusishabikie udini na viongozi walioko madarakani maana ni wa awamu tu.
Vita vya kiimani ni mbaya na mota hautazimika. Ndani ya familia moja kuna wasio na dini, wakristu na waislamu sasa hapo kazi sijue ianze ndani familia au kwa jirani.
 
Naomba nami niweke wazo maana nawiwa moyoni kwa hili ''je kuna jambo baya au zuri sana katika jamiii?'' ulionalo baya leo kesho laweza kuwa zuri na bado ni lile lile...je MOU ni mbaya au ubaya ni kuifisadi MOU maana hata mimi naweza kuanzisha NGO yangu na nikapata financial assistance{MSAADA WA KIPESA} na bado serikali isipate tija iliyofanya na NGO yangu katika MOU kwasababu suala si kanisa kufanya makubaliano fulani suala je yale makubaliano yataleta tija iliyodhamiliwa tija ya serikali kwa NGO yangu ni kujenga hospitali kwa matibabu, kwa kutibia watu mimi naamua kutibu wanyama hayawani wa mwituni... tija ipo hapo fursa hizi zipo pande zote bila kubagua suala je unazihitaji na je ukizipata zitatimiza tija za MOU?...Isije ikawa mfano wa wale waliopewa shamba kubwa mahali fulani katka mkoa fulani na baada ya miaka 30 wale wa upande x wamejenga nyumba zao na kuuza wakati wale wa upande z wamejenga hospitali na shule na hata watoto wa wale waliotumia vibaya shamba lile wanatibiwa na kupata elimu.....hili nalo suala je serikali ilipata tija?
 
Back
Top Bottom