Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
Tatizo kubwa la hii post na aliyeiandika ni upungufu mkubwa wa hekima, pamoja na elimu aliyonayo na uwezo wa uchambuzi.Halafu ikisemwa hapa kuwa Tanzania kuna udini (hivyo watu watibu ugonjwa huu badala ya kujaribu kuuficha) mimacho na mipovu inawatokaaaa..... Phewwwww
GT anaheshimika sana kwa kutoa mada zenye kina , lakini katika hili ana sikitisha.
Badala ya kuona the positive side of social services zinazotolewa na taasisi za dini za Kikristo yeye anaona kuwa na hizo taasisi ni maadui zake.
Ikumbukwe kuwa taasisi nyingi za aina hii zilitaifishwa na Nyerere na kufanywa za kitaifa na hivyo kuwa faidisha wananchi wote kwa ujumla na zinaendelea kufanya hivyo hata leo.
Taasisi za Kiislamu hazijazuiwa kutekeleza na kuomba misaada serikalini au kwingineko katika kuimarisha huduma za jamii.
Kama alivyosema Mwafrika hapo juu, wenzetu wa imani nyingine wengine hata wakielimika mioyo yao bado huwa imepandwa nafsi za chuki na upingaji wa maendeleo. Maendeleo ambayo hata wao wanayahitaji.