Mkataba wa Bandari: Anayekiri makosa na kuomba msamaha asamehewe kisha twende pamoja

Mkataba wa Bandari: Anayekiri makosa na kuomba msamaha asamehewe kisha twende pamoja

Wakiristo wana chuki sana dhidi ya waislam, waraka wa maaskofu na wapingaji wa Mkataba wanaendeshwa na udini tu hamna jengine.
Kuna watu mnafanya jumuia nzima ya kiislamu ionekane ina kasoro ya ufahamu kumbe ni nyie binafsi.
Huu mkataba wa bandari kwani ni wa kiislamu? Au unataka kusema hii serikali ya sasa ni ya kiislamu?
Kwani kuwa na Rais na waziri wa ujenzi waislamu ndio kusema serikali na mkataba ni uislamu?
Mbona kuna Spika Tulia yumo humo ni mkristo? Waziri Kitila wa uwekezaji ni mkristo na msemaji wa serikali Msigwa ni wapiga chapuo?
Wasira na Mwigulu mbona ni wakristo na ndio wapo humo na ni wakristo? Sasa haya mambo ya kusema sijui mkataba ni wa waislamu mnayatoa wapi? Hiyo ni inferiority complex mnayojijengea wenyewe.
Ila sasa ndio nimeelewa ule usemi mnaoupenda sana, "NDUGU YANGU KATIKA IMANI" kwamba unaweza kuisaliti nchi ili kutetea mtu kwa ujinga wake kwa sababu mko katika imani moja ya dini yenu.
Hilo ni tatizo kubwa
 
Bahati mbaya wabunge wengi pamoja na kubebwa 2020 bado wanaamini ukondoo wao ndio tiketi ya kubebwa tena 2025. Hawajui wanatumika alafu uchaguzi unaokuja watatoswa vilevile ili kutengeneza safu zao mpya.

Bunge limepoteza kabisa uelekeo na kuaminika, huu ndio ukweli unaopaswa kuangaliwa kwa makini sana. Bahati mbaya idara zetu za usalama zinaelekea kushindwa kulinda kikamilifu hizi taasisi au mihimili kubakia na nguvu yake ya kikatiba.

Lazima turudi nyuma tujipange upya kama Taifa.
 
Huu mchezo hautaji hasira.
Kunitusi hakutafanya nibadili mtazamo wangu, ni uhuru wa kutoa maoni tu.
Mimi kwa maoni yangu ni udini tu
Wapi nimekutusi nimeuliza swali kwamba wehu nini? Jibu ni ndio au hapana,kama unashindwa kuelewa tofauti ya swali na tusi utaweza kujibu hoja za mkataba mbovu kweli?
 
Elimu ipi unaulizia hii ya wakoloni kutoka Ulaya, tena kwa lugha za kikoloni?
Hiyo niligonga gonga kidogo si haba.
BA business and finance.
MSc Oil and gas management
Kisha nikabadilika kabisa nikagonga
BSc Medical science
Nikapiga BSc Diagnostic radiography
Huku madrasa nina kiwango cha thanawi yaani elimu ya sekondari.
Kuhusu kuandika ujinga naomba tukubaliane kutokukubaliana.
Wakoloni wana msemo wao "Common sense is not common"
Mtazamo wako na wangu hauwezi kuwa sawa
Samahani una umri gani swali personal kidogo limtokana na Jibu lako la elimu Dunia...maan ulichokisoma chote chuoni (Elimu dunia) hizo bachelor zote inatakiwa ukae darasani si chini ya miaka 18 na kibongo bongo hapo huenda ulianza kusma ukiwa una miaka 25 so kwa makadirio huenda una miaka kuanzia 50 na kuendelea (MAWAZO YANGU TU KAMA NI KWELI LAKINI)
Eniwei na mimi ni Muslim kiwango changu ya elimu madrasa ni Mustalahul Hadith (Sayansi ya hadithi) au chuo kikuu kwa elimu yakawaida
 
Mkataba huu urudiwe kwa kuwa huu ni Sumu sio haramu tu ni Sumu katika aspect zote,kiusalama,kiuchumi,kibiashara na kila kitu.
Hatupingi uwekezaji,tunakataa mikataba fiche yenye kuleta hasara kwa nchi na utumwa kwa taifa la kesho.
Vipengele vya mkataba viwekwe wazima,vijadiliwe na Kisha virekebishwe tusonge mbele.
Haraka ya Nini kwenye huu mkataba,kama kuchelewa tumeshachelewa saaana kama nchi,lakini haraka zetu ni kujiweka kwenye tanuri la moto wa gesi,kama Taifa.
Uchelewe ili muendelee kuiba bandarini?
 
Wakiristo wana chuki sana dhidi ya waislam, waraka wa maaskofu na wapingaji wa Mkataba wanaendeshwa na udini tu hamna jengine.
Ukiachana Na jicho la udini mkataba wenyewe upo vizuri kwa mtazamo wako?
 
Kuna watu mnafanya jumuia nzima ya kiislamu ionekane ina kasoro ya ufahamu kumbe ni nyie binafsi.
Huu mkataba wa bandari kwani ni wa kiislamu? Au unataka kusema hii serikali ya sasa ni ya kiislamu?
Kwani kuwa na Rais na waziri wa ujenzi waislamu ndio kusema serikali na mkataba ni uislamu?
Mbona kuna Spika Tulia yumo humo ni mkristo? Waziri Kitila wa uwekezaji ni mkristo na msemaji wa serikali Msigwa ni wapiga chapuo?
Wasira na Mwigulu mbona ni wakristo na ndio wapo humo na ni wakristo? Sasa haya mambo ya kusema sijui mkataba ni wa waislamu mnayatoa wapi? Hiyo ni inferiority complex mnayojijengea wenyewe.
Ila sasa ndio nimeelewa ule usemi mnaoupenda sana, "NDUGU YANGU KATIKA IMANI" kwamba unaweza kuisaliti nchi ili kutetea mtu kwa ujinga wake kwa sababu mko katika imani moja ya dini yenu.
Hilo ni tatizo kubwa
Umewataja wakristo hawa vizuri sana ambao wamejibu hoja za kimkataba vizuri kabisa!

Kwa nini hutaki kusikiliza hoja zao unasikiliza hoja za hao wahuni TEC?
 
Yapata mwezi mmoja uliopita, nikiwa Dodoma nilikutana na watu kadhaa, miongoni mwao ni wabunge wawili, mmojawapo aliwahi kuwa Naibu Waziri hapo awali. Hii ni kabla ya hukumu ya mahakama, ni kabla ya waovu kuwakamata watu walioamua kusimama mbele kupigania rasilimali bandari zetu, na ni kabla ya waraka wa Wahashamu Baba Maaskofu. Wabunge hawa walisema wazi kuwa kwa kweli mkataba wa DP haukupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa bali ulipelekwa ili ionekane umepitishwa na Bunge, na kwamba ilijulikana kuwa ni mkataba mbaya ndiyo maana walizuiwa kuujadili.

Wabunge hawa wakaeleza kuwa kabla ya mkataba huo kusomwa Bungeni, walitakiwa kuhudhuria kikao cha chama ambako walipewa maelekezo kuwa wanatakiwa kuupitisha. Wakaeleza kuwa hata wabunge walioongea, ni wale waliopangwa kuusifia. Na wanahisi Mdee kupewa nafasi ya kuongea, na kisha kuukosoa huenda Spika hakutegemea kama angefanya hivyo.

Wabunge hawa walionekana kutopendezwa na kile kilichotokea, lakini ni kama watu wanaoona kuwa ni lazima kuwa wanafiki ili maisha yaende.

Kama wabunge wangekuwa wanajitambua, wasingekubali kuburuzwa kwa namna hiyo. Naamini, hata ile namna ya hawa watu walivyopatikana (baadhi kutangazwa bila ya kuchaguliwa, na wengine kwa wizi wa kura), na hulka ya unafiki iliyojengeka ndani ya CCM na hata ndani ya bunge lenyewe, hakuna anayekuwa na ujasiri wa kupinga kitu ambacho nafsi yake haikubaliane naye, na mamlaka zilizowapa huwa ubunge, zinataka.

Kwa hapa tulipofika, ni busara sana kwa wale ambao nafsi zao zinawasuta kutokana na uhusika wao kwenye mkataba ule wa hovyo kabisa, kuuvua uwoga na kuuvaa ujasiri, na kutamka wazi kuwa walikosea na hawakutimiza wajibu wao. Waombe msamaha, nina imani Watanzania watawasamehe, tutasonga mbele pamoja. Hiyo haitajalisha kama anayeomba msamaha kama ni mbunge, ni polisi, ni mwanahabari, ni waziri au kiongozi wa chama.

Kwa Rais Samia, kutangaza tu kuufuta huu mkataba, atakuwa ameomba msamaha kiutuuzima, hata asipotoa kauli ya kuomba msamaha.

Taifa letu ni muhimu kuliko chochote anachoweza kukipata, iwe ni rushwa binafsi au ya kitaasisi. Na tujue kuwa hakuna Taifa pasipo umoja, amani na maelewano.

Baadhi wamekwishaanza kuifuata njia hii. Mbunge wa Bunda, yeye amesema wazi kuwa wala hata kuusoma huo mkataba hakuusoma kwa vile hata lugha iliyotumika, hana ujuzi nayo. Watu wa namna hiyo siyo wa kuwabeza, bali tuwapongeze kwa kujitokeza na kuunena ukweli. Mbunge wa Nkasi, yeye alisema wazi kuwa walikokotwa na kuambiwa wanaenda Dubai, hata hawakuambiwa wanaenda kufanya nini. Kumbe ilikuwa kuipa syndicate uhalali.

Najua ugumu upo zaidi kwa wale wanaotajwa kuhongwa pesa taslim, magari na nyumba. Hawa wana hofu kubwa. Maana kukana hadharani kunaweza kuchukuliwa na waliowahonga kuwa waliwatapeli kwa kuchukua pesa na kuwadanganya kuwa watahakikisha kwa vyovyote mkataba unapitishwa.

Mkataba ni wa hovyo, ni haramu na haufai kwa jamii yoyote. Uharamu wake umenenwa na watu wengi, tena wabobezi sana. Kama kuna yeyote ambaye mpaka leo haoni uhovyo wa mkataba huo basi rushwa aliyopewa, siyo tu itakawa imepofusha akili yake, bali rushwa aliyoila imeua na kuteketeza kabisa akili, dhamira na nafsi yake.

Hongereni ma asanteni Wahashamu Maaskofu, hongera na shukrani sana Madeleka, Mwambukusi, Mdude, Slaa kwa kujitoa sadaka kwaajili ya Watanzania. Asanteni sana TLS, Prof. Shivji, Mzee Butiku na Mzee Warioba, kwa maana hamkupindisha maneno ili kuoulizwa manukato uozo.

Ukweli na wema vinaweza kuchelewa, lakini mwishoni lazima ushindi upatikane.
Vyama pia!
 
Elimu ipi unaulizia hii ya wakoloni kutoka Ulaya, tena kwa lugha za kikoloni?
Hiyo niligonga gonga kidogo si haba.
BA business and finance.
MSc Oil and gas management
Kisha nikabadilika kabisa nikagonga
BSc Medical science
Nikapiga BSc Diagnostic radiography
Huku madrasa nina kiwango cha thanawi yaani elimu ya sekondari.
Kuhusu kuandika ujinga naomba tukubaliane kutokukubaliana.
Wakoloni wana msemo wao "Common sense is not common"
Mtazamo wako na wangu hauwezi kuwa sawa
Basi itakuwa ni zile degree za pichu au imani ya kidini umeitumia vibaya hadi imekuharibu.
Elewa hata katika makundi ya extremist wanaofanya vitendo vya ajabu visivyo vya kiutu wamo wasomi wakubwa pia.
 
Masheikh wako wamekujaza takataka kichwani na wewe unabeba tu.

Nyinyi wafuasi wa Mudi mnashida sana vichwani mwenu
Na fikiri tuchangie bila kuwakosea heshima Viongozi hadhim mitume na Manabii waliotumwa na Mungu itakuwa vyema sana
 
Haya sasa.
Tuone
IMG-20230821-WA0002.jpg
 
Sio siri tena!
Sasa hivi makanisani ibada imekuwa ni bandari tu.....
Hata huku vijiweni kwetu ni hilo tu, Fikiria wanachukua bandari zote, hadi za maziwa victoria, Tanganyika na Nyasa. Ni bora waondoe za Ziwani ya Mtwara pamoja na ya Tanga. Yeye DP World apewe ya Dar es Salaam na Bagamoyo. Ili Ikiwa kwa makusudi akipunguza ufanisi ili mizigo iende Kenya ama Msumbiji ama kwingeneko atakakoshinda tena, sisi pia tuna Bandari za kujinasulia.

Unajifungaje kijinga hivo

Wakati unaumia kwa sabotage ya kiuchumi Dini haitakuwepo kukuokoa. Ikumbukwe kwamba hawa wanadamu ambao Dini zinatokea kwao wameanza kuelewa Japan na Korea na China hawakuwa na Dini za Asia ya Kati lakini bado Mungu amewapa mafanikio ya kutosha.

Hivyo affiliations za dini haziwezi kutupatia uahueni wowote.

Tuzingatie mapungufu na ikiwezekana mkataba urudi bungeni urekebishwe na sheria za nchi kuhusu ardhi na State Sovereignty izingatiwe ksiha wapewe Bandari maisha yaendelee.

Lakini kuwapa bandari zote HAPANA
 
Samahani una umri gani swali personal kidogo limtokana na Jibu lako la elimu Dunia...maan ulichokisoma chote chuoni (Elimu dunia) hizo bachelor zote inatakiwa ukae darasani si chini ya miaka 18 na kibongo bongo hapo huenda ulianza kusma ukiwa una miaka 25 so kwa makadirio huenda una miaka kuanzia 50 na kuendelea (MAWAZO YANGU TU KAMA NI KWELI LAKINI)
Eniwei na mimi ni Muslim kiwango changu ya elimu madrasa ni Mustalahul Hadith (Sayansi ya hadithi) au chuo kikuu kwa elimu yakawaida
Nakaribia miaka 46, mwezi wa kumi naingia akipenda mola.
Ni kweli miaka mingi kidogo nilikuwa mwanawazuoni, nilifanya O level, 1992-1995, A level, 1996-1998. BA business and finance De Monfort University , 2000-2003(UK), MSc Oil and gas management Coventry University, 2004-2006 (UK), kisha Barchelor of medical science University of Leicester, 2009-2013 (UK) na BSc Diagnostic radiography Derby University, 2017-2020 (UK)
 
Basi itakuwa ni zile degree za pichu au imani ya kidini umeitumia vibaya hadi imekuharibu.
Elewa hata katika makundi ya extremist wanaofanya vitendo vya ajabu visivyo vya kiutu wamo wasomi wakubwa pia.
Hayo ni maoni yako, na nayaheshimu.
Lakini kwa mtazamo wangu baada ya uchambuzi wa makini sana, shida kubwa ya wapinga mkataba ni chuki tu na udini hamna jengine
 
Ukiachana Na jicho la udini mkataba wenyewe upo vizuri kwa mtazamo wako?
Mkataba hauna tofauti sana na mikataba yetu karibu yote na wakoloni na mabepari kutoka ulaya, ama mikataba yetu na wageni wengine, na hii ni kutokana na uzoefu nilinao wa mikataba ya mafuta na gesi na madini duniani ambayo ni moja ya taaluma zangu
 
Wakiristo wana chuki sana dhidi ya waislam, waraka wa maaskofu na wapingaji wa Mkataba wanaendeshwa na udini tu hamna jengine.
Sijui nilini Islam mmeanza kutumia dini kama kigezo cha ugawaji urithi wa Taifa letu ila siku tukiwa tumegeuzwa watumwa namijeredi migongoni ndomtashituka tuligawa vyathamani sana Suala la Bandali sio lakuangalia kwajicho la propaganda zakidini Bandari nimilango ya Taifa letu acheni kutumia nyama zakondoo wamisaada kufikili
 
Mkataba hauna tofauti sana na mikataba yetu karibu yote na wakoloni na mabepari kutoka ulaya, ama mikataba yetu na wageni wengine, na hii ni kutokana na uzoefu nilinao wa mikataba ya mafuta na gesi na madini duniani ambayo ni moja ya taaluma zangu
Tuwekee hiyo unayoijua tufananishe kifungu kwa kifungu
 
Back
Top Bottom