Mkataba wa Bandari: Anayekiri makosa na kuomba msamaha asamehewe kisha twende pamoja

Mkataba wa Bandari: Anayekiri makosa na kuomba msamaha asamehewe kisha twende pamoja

Elimu ipi unaulizia hii ya wakoloni kutoka Ulaya, tena kwa lugha za kikoloni?
Hiyo niligonga gonga kidogo si haba.
BA business and finance.
MSc Oil and gas management
Kisha nikabadilika kabisa nikagonga
BSc Medical science
Nikapiga BSc Diagnostic radiography
Huku madrasa nina kiwango cha thanawi yaani elimu ya sekondari.
Kuhusu kuandika ujinga naomba tukubaliane kutokukubaliana.
Wakoloni wana msemo wao "Common sense is not common"
Mtazamo wako na wangu hauwezi kuwa sawa
Nina wasiwasi sana na elimu yako, hivyo vyeti vyako natakiwa kuvipitia nijiridhishe.
 
MKATABA UNAFAA NA HAUNA SHIDA YOYOTE WALIKUWEPO TICTS WAMESHINDWA WACHA WAJE DP WORLD.
 
Yapata mwezi mmoja uliopita, nikiwa Dodoma nilikutana na watu kadhaa, miongoni mwao ni wabunge wawili, mmojawapo aliwahi kuwa Naibu Waziri hapo awali. Hii ni kabla ya hukumu ya mahakama, ni kabla ya waovu kuwakamata watu walioamua kusimama mbele kupigania rasilimali bandari zetu, na ni kabla ya waraka wa Wahashamu Baba Maaskofu. Wabunge hawa walisema wazi kuwa kwa kweli mkataba wa DP haukupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa bali ulipelekwa ili ionekane umepitishwa na Bunge, na kwamba ilijulikana kuwa ni mkataba mbaya ndiyo maana walizuiwa kuujadili.

Wabunge hawa wakaeleza kuwa kabla ya mkataba huo kusomwa Bungeni, walitakiwa kuhudhuria kikao cha chama ambako walipewa maelekezo kuwa wanatakiwa kuupitisha. Wakaeleza kuwa hata wabunge walioongea, ni wale waliopangwa kuusifia. Na wanahisi Mdee kupewa nafasi ya kuongea, na kisha kuukosoa huenda Spika hakutegemea kama angefanya hivyo.

Wabunge hawa walionekana kutopendezwa na kile kilichotokea, lakini ni kama watu wanaoona kuwa ni lazima kuwa wanafiki ili maisha yaende.

Kama wabunge wangekuwa wanajitambua, wasingekubali kuburuzwa kwa namna hiyo. Naamini, hata ile namna ya hawa watu walivyopatikana (baadhi kutangazwa bila ya kuchaguliwa, na wengine kwa wizi wa kura), na hulka ya unafiki iliyojengeka ndani ya CCM na hata ndani ya bunge lenyewe, hakuna anayekuwa na ujasiri wa kupinga kitu ambacho nafsi yake haikubaliane naye, na mamlaka zilizowapa huwa ubunge, zinataka.

Kwa hapa tulipofika, ni busara sana kwa wale ambao nafsi zao zinawasuta kutokana na uhusika wao kwenye mkataba ule wa hovyo kabisa, kuuvua uwoga na kuuvaa ujasiri, na kutamka wazi kuwa walikosea na hawakutimiza wajibu wao. Waombe msamaha, nina imani Watanzania watawasamehe, tutasonga mbele pamoja. Hiyo haitajalisha kama anayeomba msamaha kama ni mbunge, ni polisi, ni mwanahabari, ni waziri au kiongozi wa chama.

Kwa Rais Samia, kutangaza tu kuufuta huu mkataba, atakuwa ameomba msamaha kiutuuzima, hata asipotoa kauli ya kuomba msamaha.

Taifa letu ni muhimu kuliko chochote anachoweza kukipata, iwe ni rushwa binafsi au ya kitaasisi. Na tujue kuwa hakuna Taifa pasipo umoja, amani na maelewano.

Baadhi wamekwishaanza kuifuata njia hii. Mbunge wa Bunda, yeye amesema wazi kuwa wala hata kuusoma huo mkataba hakuusoma kwa vile hata lugha iliyotumika, hana ujuzi nayo. Watu wa namna hiyo siyo wa kuwabeza, bali tuwapongeze kwa kujitokeza na kuunena ukweli. Mbunge wa Nkasi, yeye alisema wazi kuwa walikokotwa na kuambiwa wanaenda Dubai, hata hawakuambiwa wanaenda kufanya nini. Kumbe ilikuwa kuipa syndicate uhalali.

Najua ugumu upo zaidi kwa wale wanaotajwa kuhongwa pesa taslim, magari na nyumba. Hawa wana hofu kubwa. Maana kukana hadharani kunaweza kuchukuliwa na waliowahonga kuwa waliwatapeli kwa kuchukua pesa na kuwadanganya kuwa watahakikisha kwa vyovyote mkataba unapitishwa.

Mkataba ni wa hovyo, ni haramu na haufai kwa jamii yoyote. Uharamu wake umenenwa na watu wengi, tena wabobezi sana. Kama kuna yeyote ambaye mpaka leo haoni uhovyo wa mkataba huo basi rushwa aliyopewa, siyo tu itakawa imepofusha akili yake, bali rushwa aliyoila imeua na kuteketeza kabisa akili, dhamira na nafsi yake.

Hongereni ma asanteni Wahashamu Maaskofu, hongera na shukrani sana Madeleka, Mwambukusi, Mdude, Slaa kwa kujitoa sadaka kwaajili ya Watanzania. Asanteni sana TLS, Prof. Shivji, Mzee Butiku na Mzee Warioba, kwa maana hamkupindisha maneno ili kuoulizwa manukato uozo.

Ukweli na wema vinaweza kuchelewa, lakini mwishoni lazima ushindi upatikane.
Kasheku hata kuongea anaona aibu.
 
Umewataja wakristo hawa vizuri sana ambao wamejibu hoja za kimkataba vizuri kabisa!

Kwa nini hutaki kusikiliza hoja zao unasikiliza hoja za hao wahuni TEC?
Ulivyoandikatu, unaonekana uelewa wako ni duni na hujastaarabika. Aliyestaarabika hawezi kuwaita maaskofu ni wahuni. Labda kama wewe ni wakala wa shetani. Wakala wa shetani humchukia na kumfanya qdui kila anayepunguza wafuasi wa shetani.

Yaani watu waache kuzingarua uchambuzi na maoni ya maaskofu, watu wenye elimu kubwa ya Ulimwengu na theolojia, wamsikilizempiga kelele Mkumbo, mtu ambaye hana uelewa wowote wa masuala ya sheria, uchumi na uwekezaji. Yaani Kitila Mkumbo,profesa wa Saikolojia ndiyo ageuke awe mwalimu wa masuala ya kisheria.

TEC ni taasisi iliyosheheni wataalam wa kila aina, huwezi kuilinganisha na wababaishaji na waimba hadaa, akina Kitila na Chongolo.
 
Ulivyoandikatu, unaonekana uelewa wako ni duni na hujastaarabika. Aliyestaarabika hawezi kuwaita maaskofu ni wahuni. Labda kama wewe ni wakala wa shetani. Wakala wa shetani humchukia na kumfanya qdui kila anayepunguza wafuasi wa shetani.

Yaani watu waache kuzingarua uchambuzi na maoni ya maaskofu, watu wenye elimu kubwa ya Ulimwengu na theolojia, wamsikilizempiga kelele Mkumbo, mtu ambaye hana uelewa wowote wa masuala ya sheria, uchumi na uwekezaji. Yaani Kitila Mkumbo,profesa wa Saikolojia ndiyo ageuke awe mwalimu wa masuala ya kisheria.

TEC ni taasisi iliyosheheni wataalam wa kila aina, huwezi kuilinganisha na wababaishaji na waimba hadaa, akina Kitila na Chongolo.
Ninawaita wahuni kwa sababu wanafanya mambo mengi sana ya hovyo na wakifanya hayo mambo wananchi wanapigaga kelele ila huwezi kuwasikia wakitoa waraka

Mfano sakata la escrow ambapo na baadhi yao walipokea migao ya fedha zetu
 
Basi itakuwa ni zile degree za pichu au imani ya kidini umeitumia vibaya hadi imekuharibu.
Elewa hata katika makundi ya extremist wanaofanya vitendo vya ajabu visivyo vya kiutu wamo wasomi wakubwa pia.
Ni kweli. Wapo extrimists waliosomasanalakino hawakuelimika, hawakustaarabika wala hawana maarifa.
 
Kwa utafiti wangu yakinifu kutoka kwenye jamvi hili jamii forum tu 90% ya wanaopinga mkataba ukifaatilia kwa makini utakuta wanaingiza uzanzibari na utanganyika, kuponda waarabu, na mwisho huwa wanaangukia kwenye uislam na waislam ndio tatizo.
Hivyo kwa muktadha huo, nimefikia hitimisho hilo kuwa wapingaji wa mkataba wanaendeshwa na mihemko ya chuki dhidi ya waislam.
Huo unaouita utafiti wako, hautakiwi kuitwa utafiti. Itakuwa ni takataka fulani iliyomo nafsini mwako uliyoamua kuiita utafiti. Unatakiwa kuiondoa.

TEC ilipinga sera za uwekezaji za Rais Mkapa. Walimpinga kwa sababu ya dini yake?

TEC ilitoa waraka kupinga utawala wa kibabe wa hayati Magufuli, usiozingatia haki za watu. Ilikuwa ni kwa sababu Magufuli alikuwa muislam?

Kwa nini TEC hao hao waliopinga baadhi ya mambo wakati wa utawala wa viongozi wakristo, wakati huo isiwe udini, ila uongozi ukiwa wa muislam, iwe udini?

Yawezekana ukawa umekaa miaka mingi darasani, lakini imeshindwa kukusaidia kuwa na maarifa. Maarifa ni zaidi ya kukaa miaka mingi darasani. Inanikumbusha kuna wakati tulikuwa na mradi wa kati wa hydropower. Tukaomba ushiriki wa serikali uwe katika kutupatia wataalam wa kufanya design na kusimamia. Serikali ikaahidi kutupatia best engineers kwaajili ya hiyo kazi. Wakatupatia engineers wanne, wawili wana masters degree, na wawili wana bachelor. Wakaja na bajeti kubwa ya ajabu. Kwa sababu tumekwishafanya miradi kama hiyo sehemu nyingine pia, hasa South America, tulipatwa na mashaka makubwa. Tukatafuta ushauri kungine. Kila aliyeona andiko lile, alisema ni rubbish. Mradi ule ulikuja kusimamiwa na technician toka Ujerumani, toka hatua ya awali mpaka unakamilika, Gharama ikawa ni kama 35% ya ile bajeti ya wahandisi wa Tanzania. Unaweza kuona dhahiri kuwa huyu mjerumani ana maarifa, hawa wahandisi wa Tanzania walikuwa wamesoma sana lakini hawana maarifa. Na hilo ni tatizo kubwa la Watanzania wengi, wamesoma lakini hawana elimu wala maarifa.
 
Musikitini haiwezekani.
Hilo ni jambo lenu wagalatia
Ninyi kwenu ni sawa, alimradi tu anayepora awe wa imani yenu? Sisi tutaendelea kuzuia uporwaji wa rasilimali za nchi bila ya kuangalia wanaoupigia debe ni wa dini gani. Hatutaangalia ni Mbarawa au Mkumbo, ni Wasira au Johari.

Mporaji ni mporaji, awe mkristo, muislam, hana dini, mwanaume au mwanamke, jina lake linabakia moja tu, kuwa huyo ni adui wa Taifa.letu la leo na la.kesho.
 
Mtu akikosa hoka ya ulinzi wa dhambi alizotenda yeye au mwandani wake kama Kikwete alivyofanya jana, anakimbilia udini ili apate watu wa kumtuliza au sympathy. Mtu anasema udini anaruka hoja kama mkataba wa bandari ni hovyo au siyo hovyo.
 
Wakiristo sisi pia ni ndugu zetu wa damu licha ya kuwa wao wanatuchukia ila sisi tunawapenda.
Kuhusu chuki nimefanya utafiti mdogo hapa kwenye jamvi na huko kwenye mitandao ya kijamii, wanaopinga wengi sio wote ila asilimia kubwa wanasukumwa na udini na chuki dhidi ya DP kwa kuwa ni waislam, hiyo ni fact
Usiende kwa hisia bali weka fikra zako huru.

Ni nani anayewachukia waislam? Sisi wengine familia zetu ni za mchanganyiko, waislam na wakristo. Japo kwa kiasi fulani misimamo ya sisi wakristo na waislam, katika imani, ipo tofauti.

Nakumbuka kwnye ukoo wetu, wapo waliobadili dini na kuwa waislam, hasa kutokana na masuala ya kuoana. Waliobadili toka ukristo kwenda uislam, kwa sababu walikuwa ni watu wazima, hawakutengwa na jamaa zao wa karibu. Lakini wao wao, baadhi waliposema wanataka kutoka kwenye uislam na kuwa wakristo, ilikuwa tafrani sana, wengine mpaka kuwatamkia watoto wao kuwa wangeingia kwenye ukristo, wangewaua. Na wakaanza kuwachukia baadhi ya ndugu kuwa wanaamini ndiyo waliowashawishi watoto wao kutofuata dini za wazazi wao, na kuamua kuwa wakristo.

Kwa ujumla, inaonekana waislam ni too sensitive. Kukitokea kitu chochote, fikra za mwanzo kabisa wanalipeleka kwenye fikra za kidini. Hata akafanyiwa jambo fulani, labda siyo la kufurahisha nafsi yake, kama jambo hilo limefanywa na mkristo, cha kwanza anaanza kufikiria jambo hilo limefanywa dhidi yake kwa sababu yeye ni muislam.
 
Umewataja wakristo hawa vizuri sana ambao wamejibu hoja za kimkataba vizuri kabisa!

Kwa nini hutaki kusikiliza hoja zao unasikiliza hoja za hao wahuni TEC?
Kama TEC ni wahuni basi jibuni hoja je mkataba uko na vipengele sawa sawa kwa maslahi ya Taifa au ni mihemuko tu.TEC wahuni sawa,je wewe utakuwa na hali gani?
 
Hata huku vijiweni kwetu ni hilo tu, Fikiria wanachukua bandari zote, hadi za maziwa victoria, Tanganyika na Nyasa. Ni bora waondoe za Ziwani ya Mtwara pamoja na ya Tanga. Yeye DP World apewe ya Dar es Salaam na Bagamoyo. Ili Ikiwa kwa makusudi akipunguza ufanisi ili mizigo iende Kenya ama Msumbiji ama kwingeneko atakakoshinda tena, sisi pia tuna Bandari za kujinasulia.

Unajifungaje kijinga hivo

Wakati unaumia kwa sabotage ya kiuchumi Dini haitakuwepo kukuokoa. Ikumbukwe kwamba hawa wanadamu ambao Dini zinatokea kwao wameanza kuelewa Japan na Korea na China hawakuwa na Dini za Asia ya Kati lakini bado Mungu amewapa mafanikio ya kutosha.

Hivyo affiliations za dini haziwezi kutupatia uahueni wowote.

Tuzingatie mapungufu na ikiwezekana mkataba urudi bungeni urekebishwe na sheria za nchi kuhusu ardhi na State Sovereignty izingatiwe ksiha wapewe Bandari maisha yaendelee.


Lakini kuwapa bandari zote HAPANA
Umenena vyema
 
Nakaribia miaka 46, mwezi wa kumi naingia akipenda mola.
Ni kweli miaka mingi kidogo nilikuwa mwanawazuoni, nilifanya O level, 1992-1995, A level, 1996-1998. BA business and finance De Monfort University , 2000-2003(UK), MSc Oil and gas management Coventry University, 2004-2006 (UK), kisha Barchelor of medical science University of Leicester, 2009-2013 (UK) na BSc Diagnostic radiography Derby University, 2017-2020 (UK)
Ila ujinga umekujaa kichwani pamoja na mlolongo wa elimu uliyonayo unashindwa kufikiri sawasawa
 
Back
Top Bottom