Ila wanawake ni kama wamezaliwa na ujinga wa asili hivi
Ni nadra sana kumkuta mwanamke anawaza hata miaka 2 mbele.
Miaka 3 nyuma,wife kuna kipindi wakati naanza maisha nilisema nimshirikishe mke wangu kwenye mipango
Basi nikawa napiga deal mixer kazi kwa mwezi Nampa 700k mara M.1 sometimes 650k..
Hapo achana na budget ya emergency ambayo Kila mwezi nilikuwa naweka 250k.
Sasa siku nayopewa termination of contract najua kabisa emergency funds Nina km 5.8M huku kwingine najua nina kama 14M.
Nikajisemea hapa sitaki tena Ajira nitaendelea na mishe zangu, Sasa namwambia wife mkataba wangu umeisha hautaongezwa zilete zile hela tufanye mahesabu tujue tunaanza wapi..
Nashangaa mtu anatoa machozi, mimi moja kwa moja nikajua mke wangu kaumia kusikia Sina Kazi nikaanza kubembeleza mbona akiba tunayo na kazi zipo nyingi sana kwenye fani yangu!!Ni vile tu mi sina mpango wa kuajiriwa baada ya mda nikamwambia lete hela tufanye mahesabu akaenda kuchukua kama 650k kaweka kitandani,mi nikamwambia lete zote akasema ndo hizo zimebaki....
Kumbuka mi najua nina 20M. Kasoro hivi aisee hasira zilinipanda ghafla pumzi ikawa inakaba km nataka kupata presha hivi aiseeee pembeni kulikuwa na kastuli flani hivi napendaga kuwekea simu usiku nikiwa nalala, kuna roho iliniingia ya kikatili nilitamani nishike kistuli nimbamize nacho Cha kichwa bahati nzuri niligeuka kumuangalia sura yake na mke wangu ana sura ya kipole sanaaa na kamwili kake kalivyo kadogo plus mimi nishawahi kufanya mazoezi makali ya boxing nikisema nipige liver shot moja naweza hata kuua...
Nikatoka nikaenda kukaa sebuleni kwanza nawaza si ningemuumiza sana!!hivi presha ndo inashika vile!nilijiogopa sana kwakweli.Sijawahi kumpiga toka tumeanza mahusiano ila nikapata picha kwanini wanaume wanapigaga wake zao tena bora mwenye mkono wa kupiga makofi maana atakuwa anapiga kdg kdg,mimi niliwazA kumuumiza yaani ukimuona unasema eee huyu mwanaume kweli katili..nilijiogopa sana kwakweli.
Siku 3 sijui nifanye nini kusema popote naona aibu siwezi mwambia mama yangu siwezi kusema kwao siwezi mwambia rafiki yangu yaani nimekaa nalo moyoni natoka naenda kushinda Bar nikifika tu mlango wa nyumbani hasira zinawaka moto ,kazi sina akiba yangu ya mambo yangu ilikuwa ni 3.5M plus 650k tu Hela yote ndo wife kawapa ndugu zake wafungue biashara, nyingine kajenga choo Cha baba yake nyingine kanunua mavitu Yao ya kike.
Niliumia sana sanaaaaaa kilichokuwa kinaniuma ni mwanamke ambaye nimeoa aje anisaidie maisha ndo anakuja nishusha,mwanamke ninayemshirikisha kila kitu ndo anakuja kuwa adui yangu,nimemaliza mkataba na ndo hapo hapo napokea taarifa km hiyo.Sina mtu wa kumshirikisha kitu maana wakumshirikisha ndo huyo kazingua.
Mda wote nawaza ukatili tu sasa kimtu chenyewe hataukipiga kofi vzr kinazima.Nssf nilikuwa na 27M.pssf nilikuwa na 11M.Nikasema nianze kule kwanza.
Changamoto nilikuwa nayo kipindi kile ni nawezaje kukaa nae chini kupanga nae maisha mwanamke wa namna hii na je maisha nitapanga na nani? Nawezaje kumfungulia Biashara mwanamke wa namna hii??Nani nitaongea nae stress zangu za maisha?Nani atanifariji pale Mambo yakuwa yakienda mrama?Nani anayenionea huruma kama sio mke wangu?Kifupi alinitisha sana sababu niliamini nipo salama halafu nikagundua nahitaji kuwa makini maana sio kweli kwamba nipo salama.
Huyu mwanamke sijawahi kuprove kunisaliti na ana heshima kiasi chake nadhani hapo ndo alipoponea,mi nilikuwa willing kuvunja ndoa ila hivyo vitu viwili ndo deal breaker kwangu basi nikapata mafao nikaweka sehemu kazaa nikawa naingiza 3M. Per month Maisha yakarudi sawa.
Sijawahi kumwambia ila Nikampa adhabu kuu mbili sitakaa nikufungulie biashara,sitakaa na wewe kujadili maendeleo ya familia,tupige story tucheke tule tulale ila my next move itakuwa siri yangu siku zote...
Kiukweli hili jambo lilinifanye nisiwazingatie kabisa wanawake, Mungu aliposema tuishi nao kwa akili alijua kabisa hawa watu hajawapa akili ya utambuzi,Sasa km mwanaume nae huna akili basi familia inakosa mwenye akili...