NDOA YA MITAALA YAMSHINDA DR.MWAKA, AWABWAGA WAKE ZAKE WAWILI ABAKI NA MMOJA.
Baada ya kurindima kwa miaka kadhaa huku akijitapa kuwa yeye ni Mwanaume wa shoka anayejua kuwahudumia, kuwalea vyema na kuwapa dozi ipasavyo wake zake watatu bila wao kugombana wala kuchukiana, huku akionyesha kwa vitendo namna anavyowamudu wake zake hao kwa kuwanunulia Magari ya kifahari, simu za gharama na matashititi mengine.
Hatimae mwisho wa siku yamemshinda, hadi sasa Dr. Mwaka amewatimua wake zake hao wawili amebaki na mwanamke mmoja ambaye anatambulika kwa jina la 'Shimmy', Mwaka ameachana na Mke wake wa kwanza ambaye ndiye alikuwa mke mkubwa na inadaiwa ndiye mwanamke aliyetoka naye mbali na baadhi ya mafanikio yake ya sasa wamechuma wote, ameachana na Mke wake wa pili amebaki na wa tatu kumuoa ambaye ndiye Shimmy.
Sababu hasa za kuachana kwao bado hazijafahamika, kutokana na wao kutokuweka mambo yao kwenye mitandao, lakini kumekuwa na majibizano ya chinichini kati ya mke wa pili ambaye ameachwa, na huyu wa tatu ambaye amebaki, ambapo majibizano yao yamekuja baada ya Dr. Mwaka kumtaka mke wake wa pili aondoke kwenye nyumba yake aliyomjengea yeye na watoto wake wawili kwa madai kwamba kama wameamua kuachana basi kila kitu alichopewa mwanamke huyo kirudishwe, jambo ambalo Shimmy ameonekana kuliunga mkono kwa asilimia zote ili yeye aichukue hiyo nyumba.
Kwa sasa Mwaka na mke wake Shimmy wameenda kupumnzika nchini Marekani na hadi sasa wanakaribia kumaliza mwezi.