Mke wa Dr. Mwaka anadai Talaka 3. Sasa yale mafundisho yake ya ndoa tufuate au tumteme?

[emoji846]
FB_IMG_16742466966449719.jpg
 
Ndoa inamambo mengi sana ndugu zangu kama hujabahatika kuoa basi muombe mungu sana akujalie mwanamke mwenye hekma yote hayo unayaona kwa mke wa dr.mwaka n mwanamke kukosa busara na hekima kukimbilia mitandaoni lengo kimchafua jamaa ni seme tuu kuwa ikinyesha ndio utajua wapi panavuja Leo anatak taraka hadharani lakini kesho atataka warudiano kwa sirii ndivyo walivyo wanapokuwa wanatak kuondoka huondoka kwa kelele na kumwaga Siri zote ila akikaa akaona Mambo yamebuma anaitaji suluhu kwa Siri ili arudi aisee wanawake waonenii tuuu Kama hayajakukuta tema matee chinii
 
Kwahy mke mkubw alikua hapewi 100% Ndoige😅
Si mwenyewe unaona hapo alishasahaulika kabisa na mume, kimsingi hamna mwanamke wa kibongo anafurahia ndoa ya wake wenza ni basi njaa tu na huduma zinawafanya kuvumilia ila wakikatiwa huduma tu mbio Bakwata 😀😀😀!

Hata mkeo nyumbani anavumilia michepuko yako ukiwa unamhudumia vizuri tu ila ukikata huduma tu ndio utajua hujui.
 
NDOA YA MITAALA YAMSHINDA DR.MWAKA, AWABWAGA WAKE ZAKE WAWILI ABAKI NA MMOJA.

Baada ya kurindima kwa miaka kadhaa huku akijitapa kuwa yeye ni Mwanaume wa shoka anayejua kuwahudumia, kuwalea vyema na kuwapa dozi ipasavyo wake zake watatu bila wao kugombana wala kuchukiana, huku akionyesha kwa vitendo namna anavyowamudu wake zake hao kwa kuwanunulia Magari ya kifahari, simu za gharama na matashititi mengine.

Hatimae mwisho wa siku yamemshinda, hadi sasa Dr. Mwaka amewatimua wake zake hao wawili amebaki na mwanamke mmoja ambaye anatambulika kwa jina la 'Shimmy', Mwaka ameachana na Mke wake wa kwanza ambaye ndiye alikuwa mke mkubwa na inadaiwa ndiye mwanamke aliyetoka naye mbali na baadhi ya mafanikio yake ya sasa wamechuma wote, ameachana na Mke wake wa pili amebaki na wa tatu kumuoa ambaye ndiye Shimmy.

Sababu hasa za kuachana kwao bado hazijafahamika, kutokana na wao kutokuweka mambo yao kwenye mitandao, lakini kumekuwa na majibizano ya chinichini kati ya mke wa pili ambaye ameachwa, na huyu wa tatu ambaye amebaki, ambapo majibizano yao yamekuja baada ya Dr. Mwaka kumtaka mke wake wa pili aondoke kwenye nyumba yake aliyomjengea yeye na watoto wake wawili kwa madai kwamba kama wameamua kuachana basi kila kitu alichopewa mwanamke huyo kirudishwe, jambo ambalo Shimmy ameonekana kuliunga mkono kwa asilimia zote ili yeye aichukue hiyo nyumba.

Kwa sasa Mwaka na mke wake Shimmy wameenda kupumnzika nchini Marekani na hadi sasa wanakaribia kumaliza mwezi.
 
Zuga tuu asomeshe watoto anaendaje kupumzika marekani wakati ada za watoto wake hajalipa?
 
Back
Top Bottom