Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa

Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa

Wanatakiwa wafanye-verification ya hizo mali kwenye mamlaka zinazohusika kwa mfano kama nyumba kupitia ardhi utajua mmliki ni nani, TRA, Halmashauri na serikali za mitaa/vijiji ni mamlaka zinaweza kusaidia wakati wa verification lakini inategemea na mali husika.
Yaani Mimi nakudai 90,000/= halafu leo hii unipitishe kwenye processes zote hizo ambazo ni obvious zitangharimu pesa ambayo ni kubwa zaidi ya hiyo nnayokudai??

Bro sisi sio benki sisi ni microcredit companies ambazo wasimamizi wakuu wa mambo yote ni serikali za mitaa tu basi na ndio maana kwenye mikataba yao lazima pawepo na muhuri wa serikali za mitaa hili kuonesha kwamba ni makubaliano yanayotambuliwa na serikali...

Kwa hiyo kudeal na hao wadaiwa sugu hatuna haja ya kupitia huko koote unakosema wewe.
 
Sisi hatupigi kelele ila tunaelekeza sheria zilivyo ukija ukaenda tofauti wewe na muajiri wako wote mtapata tabu, ndio maana unaonaa oya leo anavyowakana wafanyakazi wake ambao wameenda kinyume na sheria
Oya ndio anayehangaika sasahivi kusafisha jina lake na hapo bado kuna penalties za bot lazima aadhibiwe ndio utaratibu ulivyo
Watu wataendelea kukopa kwa mujibu wa sheria ila ukidai kinyume na sheria jela inakuhusu
Mbona unatetea hao wadaiwa sugu walishindwa kuheshimu makubaliano?
 
Hao OYA ni hatari balaa, kuna sehemu walikuwepo wametega IST moja nasikia watu wanasema anadakwa mtu sasa hivi...mara Mama mmoja akiwa na mwenzake kaambiwa "haya leo tunaondoka na wewe ingia kwenye gari, wewe kila siku unatupiga chenga chenga tu na kuambiwa umehama unapokaa, ingia kwenye gari" jamaa wanaongea kwa sauti hadi watu kujaa, yule mama nilimhurumia asee.

Hali inatisha wakuu
 
Mbona unatetea hao wadaiwa sugu walishindwa kuheshimu makubaliano?
Siwatetei ila mikataba si ipo hakuna mkataba wowote duniani wa bank unaoruhusu matumizi ya nguvu, kama halipi unafuata utaratibu kurecover tofauti na hapo utajikuta jela kama hawa jamaa wa oya, nenda mahakamani huku interest yako inaendelea na mdeni anaweza kukufidia gharama za kesi inategemea mahakama itaamua vipi ,huna sababu ya kujitafutia matatizo wakati sheria zipo
 
Yaani Mimi nakudai 90,000/= halafu leo hii unipitishe kwenye processes zote hizo ambazo ni obvious zitangharimu pesa ambayo ni kubwa zaidi ya hiyo nnayokudai??

Bro sisi sio benki sisi ni microcredit companies ambazo wasimamizi wakuu wa mambo yote ni serikali za mitaa tu basi na ndio maana kwenye mikataba yao lazima pawepo na muhuri wa serikali za mitaa hili kuonesha kwamba ni makubaliano yanayotambuliwa na serikali...

Kwa hiyo kudeal na hao wadaiwa sugu hatuna haja ya kupitia huko koote unakosema wewe.
Labda dhamana ya mkopo isiwe Hati ya nyumba au gari la sivyo ikitokea dispute kushinda kesi mahakamani itakuwashida.
 
Hao OYA ni hatari balaa, kuna sehemu walikuwepo wametega IST moja nasikia watu wanasema anadakwa mtu sasa hivi...mara Mama mmoja akiwa na mwenzake kaambiwa "haya leo tunaondoka na wewe ingia kwenye gari, wewe kila siku unatupiga chenga chenga tu na kuambiwa umehama unapokaa, ingia kwenye gari" jamaa wanaongea kwa sauti hadi watu kujaa, yule mama nilimhurumia asee.

Hali inatisha wakuu
Kwanini usingemlipia Hilo deni Sasa kama ulimwonea huruma?

Vipi ulijaribu hata kuwaskiliza hao jamaa wa OYA jinsi walivyosumbuliwa na huyo mama mpaka anafikia hatua ya kuwadanganya amehama?

Watu kama wewe ndio huwa mnaonea huruma mpaka mafisadi yakitumbuliwa, yaani hawaangalii chanzo Cha tatizo Bali unajikita zaidi na matokeo
 
Hawajakutana na watu wanaojua sheria. Kumlazimisha mteja wako kuingia kwenye gari kwa nguvu ni kinyume cha sheria hiyo ni unlawful arrest kwa sababu issue ya mkopo ni civil case wala si criminal case. Nashangaa kusikia eti wanaenda majumbani mwa watu usiku kukamata kitu ambacho ni unlawful.
 
Labda dhamana ya mkopo isiwe Hati ya nyumba au gari la sivyo ikitokea dispute kushinda kesi mahakamani itakuwashida.
Mtu akuja kukopa kwanza anawaambia Hana mume, anaweka dhamana vitu vya ndani kama friji,TV,makochi,Oven n.k

Na anawasisitizia kabisa vyote hivyo ni vya kwake amenunua kwa pesa yake na Yuko tayari vichukuliwe siku akishindwa kulipa mkopo huo.

Haya inatokea kweli ameshindwa kulipa na mkataba umeisha siku mkienda kivibeba mnakutana na kijeba pale anajutambulisha kama mume wake anawaambie vitu vyote vilivyomo ndani ni vya kwake na mke wake Hana hata kimoja, kwa hiyo muondoke nyumbani kwake.. Sasa kwa scenerio kama hii unafikiri ni nini kitatokea? Kwamba maafisa mikopo waondoke mikono mitupu kwa sababu eti walindanganywa na huyo mteja wao??
 
Polisi ndio kazi yao kulinda amani na kutulinda dhidi ya wahalifu ndio maana tunawapa bunduki na mabomu kwa ajili hiyo
Bank kazi yake kukopesha hela na kuna mikataba ambayo inatoa remedy mtu akishindwa kulipa, remedy zipo nyingi, ila hakuna sehemu yoyote bank inatakiwa kutumia nguvu ndio maana hata bank imewakana leo kwa kutoa tamko kwamba halijawatuma kutumia nguvu, kutumia nguvu ni jinai
Jamaa unaongea utafikiri hao polisi huwa wanatekeleza majukumu yao kwa kuufuata formalities kama zinavyosema..

Wewe unafikiri Kuna mtu angekuwa anajichukulia hatua mwenyewe kama huko polisi kusingekuwa Kuna gharama?
 
Unawakingia sana kifua wana oya, wewe ni mmoja wao wauaji?

Wacha kuruka sarakasi na scenario ambazo hazihusiani na kesi hii ya mauaji
Wewe ni mmoja wapo ya wadaiwa sugu ambao mnajua tu kupokea hela ila kulipa ahaaa???
 
Hii Nchi hali ya Umasikini wa kipato ni Mkubwa sana

Imagine Mkopo wa shilingi 200,000 wanakaa miezi 3 hadi 6 hadi kushindwa kulipa.

Wakati Mume angechukua hilo Jukumu la kuulipa huo mkopo sidhani kama angeshindwa kulipa walau shilingi 60,000 Kwa Mwezi ambapo ni wastani wa kusevu shilingi 2,000 Kwa Siku
Hali ya umaskini wa kipato imeongezeka kwa kasi ya 5G lakini kila kukicha ni sifa jinsi uchumi ulivyoimarika.Mume asingeweza kuchukua jukumu la kulipa huo mkopo kwa sababu ni mume jina tu.Real men wanatunza wake zao kwa hiyo sababu ya kukopa na kuhangaika hangaika haipo.
 
Mkuu
Hata kama unafaidika lazima ukweli usemwe.
1. Hii mikopo ina riba kubwa hivyo ni chanzo cha umasikini kwa wakopaji na wizi kwa wakopeshaji na wanaonea wale wa hali ya chini.
Ni kosa la BoT kama regulator, Oya kama mkopeshaji mwenye riba kubwa na mkopaji mwenyewe mwenye kujua au kutokujua riba ilivyo kubwa. Mkopaji alitakiwa aachane na mkopo kama una riba kubwa, kitendo cha kusaini maana yake amekubali kulipa riba hiyo.

Wote watatu wana makosa ila kibepari zaidi, Oya hawana kosa sana inabaki huruma t BoT ndio inatakiwa ifanye strict regulations ambazo hazipo na mkopaji atumie akili kufanya maamuzi.
2. Unapokopesha unatakiwa ufanye tathimini ya uwezo wa mtu kulipa na si tamaa ya kuchukua vilivyo vyake.
Kwamba kwa akili yako unaona huo mkopo ni wa kumshinda mtu mzima mwenye akili timamu na nguvu? Kwahiyo kampuni isidai 60,000 kisa mkopaji hana uwezo?
 
Kwanini usingemlipia Hilo deni Sasa kama ulimwonea huruma?

Vipi ulijaribu hata kuwaskiliza hao jamaa wa OYA jinsi walivyosumbuliwa na huyo mama mpaka anafikia hatua ya kuwadanganya amehama?

Watu kama wewe ndio huwa mnaonea huruma mpaka mafisadi yakitumbuliwa, yaani hawaangalii chanzo Cha tatizo Bali unajikita zaidi na matokeo
😊
 
Ni kosa la BoT kama regulator, Oya kama mkopeshaji mwenye riba kubwa na mkopaji mwenyewe mwenye kujua au kutokujua riba ilivyo kubwa. Mkopaji alitakiwa aachane na mkopo kama una riba kubwa, kitendo cha kusaini maana yake amekubali kulipa riba hiyo.

Wote watatu wana makosa ila kibepari zaidi, Oya hawana kosa sana inabaki huruma t BoT ndio inatakiwa ifanye strict regulations ambazo hazipo na mkopaji atumie akili kufanya maamuzi.

Kwamba kwa akili yako unaona huo mkopo ni wa kumshinda mtu mzima mwenye akili timamu na nguvu? Kwahiyo kampuni isidai 60,000 kisa mkopaji hana uwezo?
Kampuni inayoua kwa 60,000. Hata nchi zilizoendelea walipambana na hizi shark loans just to protect the vulnerable individuals.
Hii ni kujifaidisha kwa wale ambao ni weak ones.
Eti mtu anakopa 100,000 anarudisha 150 000 ndani ya mwezi. Hii ni laana.
 
Back
Top Bottom