Habari za jumapili wanajamvi.
Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.
Mimi na mke wangu tangu tufunge ndoa huu ni mwaka wa tisa . Hatukuwahi kuwa na migogoro mikubwa ingawa mikwaruzano ile midogo ilikuwepo.
Sasa katika kipindi cha miaka sita ya ndoa yetu nilimuweka tu nyumbani sikutaka ajishughurishe na biashara yoyote. Mwaka wa sita wa ndoa yetu nilipata ajali ya pikipiki iliyopelekea mimi kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili. Hivyo nilikuwa admitted Muhimbili hospital kwa muda wa kama miezi 3 kabla ya kuruhusiwa.
Kutokana na uwekezeji wangu kwa kipindi chote hiki wakati naugua hatukuwahi kupata Shida ya mahitaji ya nyumbani. Baada ya lile tukio nikajiuliza hivi ikitokea nimefariki Huyu mama ataishije na watoto wangu. Nikamshirikisha nimfungulie biashara ili aanze kujifunza mbinu za utafutaji. Nilipopona tukafungua biashara ya kufanya miamala ya simu na kuuza soft drinks jumla na rejareja.
TATIZO:
Miaka mitatu ya hii biashara imeanza kuniletea matatizo Kwenye ndoa. Wanaume wamekuwa wanapiga simu mpaka juma pili Siku ambayo wanajua hafanyi biashara na mbaya zaidi kuna mmoja nilikuta SMS za mitongozo na wife alikuwa ameshaingia king. Sasa nilimtafuta yule kijana na kuongea naye ingawa alisema alikuwa hajui kama yule mke wa mtu tangu sasa hatomsumbua tena. Mke wangu yeye alijitetea kuwa alimwabia yule kijan kuwa yeye ameolewa lakini aliendelea kumsumbua tu.
Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha kufanya.
NDUGU WA WIFE:
Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo. Wengine mpaka wakadiri kwenda mbali na kusema wao ndio walimpa mtaji niliwauliza ni kiasi gani cha mtaji mlimpa wanasema laki saba. Niliishia kucheka tu kwa sababu hiyo lakini saba haitoshi hata kulipia kodi ya hilo eneo kwa mwaka.
NINACHOOMBA :
Wadau ninachoomba kutoka kwenu ni mawazo jinsi gani niweze kuliweka hili jambo sawa iwe kwa kufunga kabisa biashara yenyewe au vyovyote vile ili mradi ndoa yangu irudi Kwenye amani kama. Mwanzo. Mama mkwe amenikasirikia hivyo yeye sioni kama ni mshauri mzuri kwa mke wangu .
Mniwie radhi kwa maelezo marefu ila nitasoma kila comment ili niweze kupata suluhisho.
Ahsante.
Weka kijana dukani ,
Mke abaki nyumbani.
Jioni ukirudi utaongozana naye kukagua hesabu.
Kuna changamoto nyingi kuoa mwanamke ambaye hakuwa na kazi yoyote au elimu yoyote halafu aje kwako baada ya kumuoa ndo umsomeshe au umtafutie shughuli yà kufanya
Hayo ndiyo madhara yake.
Wanawake ndivyo walivyo.
Mimi nimeshuhudia kwa waalimu wangu wawili wa kiume.
Mwalimu wangu wa kwanza alimsomesha mchumba hadi chuo kikuu na mchumba kupata kazi.Siku ya ndoa mchumba akatoka kuolewa naye akasema siyo taipu yake.
Mwalimu wangu mwingine alioa mke ambaye hakuwa na kazi..Alipomuoa akamuendeleza kielimu na kisha akamtafutia kazi.Baada ya kumtafutia kazi mwanamke jeuli ikaanza ndani ya nyumba.
Ndoa ikavunjika.
Rafiki yangu mwingine alioa mwanamke ambaye hakuwa na kazi na alikuwa ni form four felia.
Akiwa katika uchumba naye akamwandikisha kuristi mitihani akapata crediti ,Walioana na kisha akaenda chuo kurasini mambo ya bandarini.kisha akapata kazi.Walibahatika kupata mtoto mmoja.Mwanamke baada ya kuanza kazi bandarini mambo yakabadilika Ndoa ilivunjika.
Kuna mwingine rafiki yangu alimfungua duka la vifaa vya pikipiki ,Akamuweka mkewe awe ndo muuzaji.Yeye alikuwa na gereji yake sehemu nyingine.
Mwanamke akaanzisha mahusiano na fremu ya jirani wakawa wanaondoka kwenda kulala kwake huyo mwanamke maana mumewe hurudi saa nne usiku.Watu hawakunyimi maneno ,mume akapewa taarifa,Akaandika mtego ,Akawakuta laivu.
USHAURI,
NI VIZURI UKITAKA KUOA UOE MWANAMKE MWENYE SHUGHULI ZAKE AU MWENYE ELIMU YAKE.
LAKINI USIOE MWANAMKE HALAFU WEWE UJE UMSOMESHE KISHA UMTAFUTIE KAZI AU UMFUNGULIE BIASHARA BASI UJUE UMEJITIA KITANZI MWENYEWE.
KWA KESI YA HUYU MDAU HAPO JUU,MIMI NAKUSHAURI
MOSI,Tafuta kijana wa hilo duka na mama muache abaki nyumbani.
Pili,Dhibiti mapato yote,Saa nyingine akiwa na vijisenti vingi huota jeuri.
Tatu,Kama dini yako inaruhusu kuongeza mke basi ni muda muafaka wa kufanya hivyo.
NIULIZE SWALI LOLOTE KAMA HUKU UELEWA AU KWANINI NIMESEMA HIVYO