Barca
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 1,448
- 1,624
Alifanya vizuri sana kuto rudi wakati wa likizo asingesoma kwa amani. Namuomba Mungu kila siku niishi na watoto wangu vixuri wakue wakiwa kwangu. Maisha ya kwa ndugu yana changamoto nyingi sana.Mke wangu alifiwa na wazazi wake wote wawili kwa ukimwi mkali ule wa zamani, hivyo akalelewa na baba yake mdogo tangu akiwa na miaka 8, darasa la pili.
Wife alipofika darasa la saba alibakwa na baba yake mdogo huyo aliyekuwa anamlea na kumtishia kuwa akisema atamuua.
Uzuri wife akawa amefaulu na kuchaguliwa shule ya bweni. Mkoa aliochaguliwa kulikuwa na shangazi yake ambaye ni aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi, hivyo likizo zote zilimalizokia kwa shangazi hadi anamaliza kidato cha nne.
Kipindi cha kusubiri majibu shangazi akawa anamsisitiza kwamba aende kusalimia kwa baba mdogo, ndipo wife akamweleza yote aliyofanyiwa na baba mdogo. Shañazi akaelewa.
Majibu yakatoka wife akachaguliwa kujiunga na shule ya bweni mkoa mwingine ambapo hakuwa na ndugu. Alisoma kwenye mazingira magumu sana.
Kwa kufupisha habari, huyu baba mdogo amefiwa na mkewe na tumezika leo. Jinsi huyo baba mdogo alivyo mchawi, akawa amemwita wife chumbani kwake mida ya saa nne. Wife alipoenda akawa anamlazimisha amlale, kwenye purukushani wife akapiga kelele.
Kwa kweli baba mdogo katia aibu sana.
Kesho tunarudi zetu Dar
Kuna ndugu unaishi nao lakini ukiwa angalia unaona kabisa hata ukiwaachia watoto wako hawata ishi kwa amani. Mimi nilishaapa watoto wangu nikifa wakaishi kanisani. Huko naamini watakua kiimani. Najua nako hakuna salama sana lakini angalau.
Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app