Mke wangu amepewa taarifa zangu na mtandao wa simu. Kisheria imekaaje?

Mke wangu amepewa taarifa zangu na mtandao wa simu. Kisheria imekaaje?

inawezekana kabisa kama una mtu ndani ya mtandao husika
kuna namba yangu ilifungwa, na ilikua site mbali na nilipo

nikamtaarif rafiki, yeye akawasiliana na rafiki yake
nikapewa PDF ya bounds zote zilizoingia na kutoka, mpaka waliosajili ile namba kabla yangu
nikashangaa
Unachosema ni sahihi kabisa na nilishawahi kuthibitisha. Ila hizi Verified [emoji2960][emoji2960][emoji2960]
 
Kampuni za simu hazihusiki ..anakutishia tu
Kivipi mkuu? Ukiangalie ile print out na simu zinamatch kabisa. Kwa sababu hii printout ni ya kuanzia tarehe 17 mwezi huu so hizo taarifa bado ninazo kwenye simu.
 
Mchunguze mwenendo wake pengine umeoa JINI.
Hahaaa hapana sio jini ni binadamu mkamilifu kbs maana hata akijikata na wembe anatoka damu. Na hata juzi kati tulipata ajaki ya gari kidogo anapiopio mguuni.
 
Ni kweli. Alitaka kujiridhisha kama kweli nilijuwa safari na kupitia hizo printout amethibitisha nilisafiri. Sasa mm ameshanitia hofu sijuzoea kuchunguzwa hivi. Hapa nakusanya nondo iki nimchemshe kidoggo asirudie tena. Nina uwezo wa kumbana mpka kunitajia walimomsaidia.
Ongea nae vizuri kama mume na kuwa makini na maamuzi yako maana usipoangalia hili swala linaweza kuleta athari kubwa tofauti na unavyoweza kuimagine.

Alichokifanya sio kizuri kwa afya ya ndoa yenu, ongea naye kwa kumuelimisha zaidi na kumkanya aachane na huo utoto.
 
Anawezekana ana mtu kwenye kampuni...
Trust me. Watu wanafanya mambo unayoyaona hayawezekani
Inawezekana, mimi nikiwa second year simu yangu ilidukuliwa na demu wangu wa 3rd year tena akaniambia kabisa hata ubadilishe line ntakudukua labda uhame mtandao wa tigo. Ilibidi tuachane tu
 
Tatizo watu wanachukulia hii mitandao poa.

Ila experts wakutosha kuzuia vitu kama hivyo.

Ili upewe printouts lazima mahakama ihusike, polisi, dci
Ndio amepata sasa. Na nimeifuma hata yeue hakutegemea japo na aliogopa sana. Anataka tuichane ila mm nimeihifadhi sehemu salama mpk nipate taarifa za kutosha toka kwake. Na atanipa
 
bado sio rahisi mkuu hata kama kuna mtu unamfahamu..... ni ngumu kuliko tunavowaza...
Ni ngumu sana kuna urasimu mkubwa sana hadi kupata details za mteja, pamoja na mlolongo wote hawezi kufanya mtu mmoja kwenye taasisi lazima ipite mikononi mwa staffs wengi na hapo ndiyo ugumu unakuja siyo wote watakaotaka kuhatarisha kibarua labda kwa donge nono sana.
 
Tatizo watu wanachukulia hii mitandao poa.

Ila experts wakutosha kuzuia vitu kama hivyo.

Ili upewe printouts lazima mahakama ihusike, polisi, dci

Mkuu kibongo bongo vitu ambavyo kisheria au kiutaratibu unafanikisha kuvipata Kwa mwezi mzima kupata basi trust me kuna watu ukiwa nao vizuri unafanikiwa kuvipata ndani ya masaa 24 tu kikubwa ni usiri tu ili usichome vibarua vya watu

Kwahiyo hayo Mambo sijui ya Kuhusisha mahakama,mara polisi, mara DCI huo ni utaratibu tu umewekwa ila haina maana lazima ufuatwe, watafata wale wasio na watu

Nimeona watu wanapata passport ya kusafiria siku hiyo hiyo, akapata kitambulisho cha NIDA siku hiyo hiyo, akapata TIN siku hiyo hiyo,akapata leseni ya biashara siku hiyo hiyo na kampuni ikasajiliwa siku hiyo hiyo
 
Wahenga walisema usimuwekee mtego wa kumfumania kama huna uwezo wa kumuacha.

Kuchunguzana mambo ya simu kwa wapenzi au wanandoa ni ucccchinga na ushamba, kama mtu unaona humuamini si umuache kuliko kuforce maugomvi yasiyo na masingi.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Utoto mwingine huo, mtu umeamua kuolewa bado unamuwinda mume kama mwanafunzi.
 
Kivipi chifu?
Sio rahs , kampuni za simu zinaweza fanya hvyo Kwa command ya vyombo vya dola kuhusu masuala ya kiusalama , kama unabisha print hyo document yako ukawashtaki ndo utajua amekuingiza cha kike .. labda kama ana mtu wake huko lakn bado sio rahs
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Utoto mwingine huo, mtu umeamua kuolewa bado unamuwinda mume kama mwanafunzi.
Yaani inachekesha sana.
Ila apewe tu elimu, aache hizo tabia awe busy kuboresha ndoa yake
 
Back
Top Bottom