Mke wangu amepewa taarifa zangu na mtandao wa simu. Kisheria imekaaje?

Mke wangu amepewa taarifa zangu na mtandao wa simu. Kisheria imekaaje?

Ni kweli. Alitaka kujiridhisha kama kweli nilijuwa safari na kupitia hizo printout amethibitisha nilisafiri. Sasa mm ameshanitia hofu sijuzoea kuchunguzwa hivi. Hapa nakusanya nondo iki nimchemshe kidoggo asirudie tena. Nina uwezo wa kumbana mpka kunitajia walimomsaidia.
Kama unajiamini kua wewe ni msafi,sasa wasiwasi wako ni nini?
 
Wakuu!

Wiki 2 zilizopita nilisafiri kikazi kwenda mkoani kwa kazi ya siku 5. Siku moja kabla ya kurudi nyumbani nikaongezewa kazi ya wiki moja nyingine.

Kimbembe kikawa kwa wife nyumbani hakunielewa. Kukatokea kupishana ila mm sikujali sana coz sikuichukulia serious sana na kweli nilikuwa mkoani kikazi. Yeye akawa anadai nipo hapahapa Dar kwa michepuko yangu.

Sasa jana nimerudi home toka mkoa nimekuta ana printout ya mawasiliano yangu yote ya kwenye simu. Kwa maana ya kwamba niliifuma karatasi inayoonyesha nimewasiliana nani, wakati gani, yupo wapi na mm nikiwa wapi. Na nilimpombana zaidi akadai ana uwezo wa kupata mpk voice clip zangu kwa ninaowasiiliana nao.

Japo ilimthibitishia ni kweli nilikuwa nimesafiri lkn imeniogopesha sana. Kwa stage hii aliyofikia huyu anaweza kunidukua chochote kile kwenye simu yangu.

Wataalam wa sheria naomba mnisaidie hii kisheria imekaaje, Je kwa kuwa yeye ni mke halali wa ndoa, ni haki yake kupewa hizo taarifa? Vp kama nikiamua kuishtaki hiyo kampuni mimi kama mteja wao je sheria itanibeba?

Sina nia ya kuprocess kesi yoyote lkn nataka tu kufahamu.

Majibu yenu tafadhali.
Huyo kaenda kwa Hackers sio mtandao wa simu mzee
 
Mkianza kutumia sheria za mahakamani...na kuendeleea kudokoa dokoa simu
Dah hiyo combination hapo inazaa uadui wa kutosha.
Msifikie mbali sana kuchunguzana na kuhukumiana.
Usitumie sheria.
Kaa nae ndoa ikishaingiza zaidi ya mtu mmoja
Sio ndoa tena ni kikundi.
Ongea nae.
Utatia doa ndoa yako.yeye kashakosea ila wewe ukienda kisheria atakua kasawazisha...means itakua ndo mwanzo wa kupelekana mahakamani mpaka uzikwe wap itaamuliwa mahakamani.
Speaking from experience....ongea nae kwa urafiki zaidi usitumie sheria.
Ila kama hakuamini kwa kiwango hicho mzee
Mpo kipindi kigumu sana.
Muombe Mungu...usizid kufungua zaidi milango ya kuingiza shetani katika familia yako.
Ila muonye kwa maneno
Yaani mawasiliano yake yamedukuliwa halafu unataka ajinyenyekeze kuongea kiurafiki kama vile yeye ndiye mkosaji?

What if aliyempatia hayo mawasiliano mke wake ni mchepuko wa mke wake? Kwa hiyo ajinyenyekeze ili kumlinda mchepuko wa mke wake?
Hapo swala ni moja tu, kutafuta mwanasheria ampatie hiyo document kwa nia ya kufungua kesi ya kudai fidia.

Wakili wake ndiye ata follow up na mengine yatajulikana mbele ya safari.
 
Yaani mawasiliano yake yamedukuliwa halafu unataka ajinyenyekeze kuongea kiurafiki kama vile yeye ndiye mkosaji?

What if aliyempatia hayo mawasiliano mke wake ni mchepuko wa mke wake? Kwa hiyo ajinyenyekeze ili kumlinda mchepuko wa mke wake?
Hapo swala ni moja tu, kutafuta mwanasheria ampatie hiyo document kwa nia ya kufungua kesi ya kudai fidia.

Wakili wake ndiye ata follow up na mengine yatajulikana mbele ya safari.
Akitaka kufanya hivyo basi awe tayari kumpoteza Mkewe coz nae ataunganishwa kwenye hiyo kesi.
 
Hii ni hatari Sana mkuu.

Ushauri wangu, japo najua unampenda Sana mkeo ila shika mkononi hiyo document Kisha mwambie ili usalama uwepo humu ndani akutajie aliem printia zaidi ya hapo asikusemeshe na asikujue kwa chochote hadi amtaje. Baada ya hapo stop kula ndani na usimfanye. Baada ya wiki kama hajamtaja beba begi lako hamia hata kwa mshkaji mwambie utarudi akimtaja

Sometimes onesha uanaume kidogo mkuu. Simama kama baba
 
Back
Top Bottom