Mke wangu amesema kwasasa hayuko tayari kuzaa, kuna mambo yake anamalizia kwanza

Mke wangu amesema kwasasa hayuko tayari kuzaa, kuna mambo yake anamalizia kwanza

Kwanini aolewe kama anataka kuendelea na hayo mambo yake?
Kwanini huyo kaka aoe mwanamke mwenye mambo yake?
Unamkuta mtoto wa watu na kazi yake,biashara zake unataka aache hayo yote ili umuoe ni nani mwenye utimamu atafanya hivyo?
Ukute huyo jamàa yenu mwenyewe mnaemtetea kutunza familia mwenyewe hawezi ndio maana bibie anaomba muda aweke mambo sawa ndio aingie kwenye uzazi .
Huwezi jua ni Kwa faida Yao wote
Hili suala ni lao
 
Iwapo moja wa wanandoa anakataa kushika mimba/kuzaa baada ya ndoa, ndoa hiyo inakuwa batili.

Huenda kuna taarifa muhimu hakukushirikisha kabla hamjaoana - jambo ambalo linakomelea ubatili wa hiyo ndoa.
 
Kabla ya kuoana si walipatana tutajuaje?
Mimi kama mwanamke nimeongea pale Kwa ufupi kugusia suala la mimba linaweza kuwa gumu bila kutafajia na mambo uliyoanzisha yakaporomoka Kwa kukosa uangalizi.huo ni mfano tu
Hili suala ni la wao kukaa chini wapatane.sio la mmoja kumvimbia mwenzie
Kwa mazingira yalivyo hakuna hayo mapatano, kuna mmoja amemvimbia mwenzake, miaka miwili ya ndoa hataki kubeba mimba, biashara zipo, kazi zipo ukisema hautaki kubeba mimba leo kwa sababu zitasimama, hakuna siku utabeba utakimbizana na hayo mambo kwakuwa bado hautataka uyumbe na umri hausubiri ndiyo yale mwanaume anataka watoto wanne kwa sababu umri umeenda unajikuta unaishia kupata wawili
 
Kabla ya kuoana si walipatana tutajuaje?
Sasa hapa ndio umeandika nini?
Unaniuliza mimi au unajiuliza wewe au unamuuliza mleta mada?

Mimi kama mwanamke nimeongea pale Kwa ufupi kugusia suala la mimba linaweza kuwa gumu bila kutafajia na mambo uliyoanzisha yakaporomoka Kwa kukosa uangalizi.
Umejuaje kua kuna mambo aliyo yaanzisha? kabla ya kuolewa au kabla ya kuanzisha hayo mambo hakujua hilo? kwanini asimtaarifu mumewe?
huo ni mfano tu
Hili suala ni la wao kukaa chini wapatane.sio la mmoja kumvimbia mwenzie
Wakae chini mara ngapi wakati mke kagoma kuzaa?
Hiyo Mbuzi ni ya kutwanga talaka tu wala haihitaji mjadala,wanawake wapo wengi sana wanao itafuta ndoa.
 
Kwanini huyo kaka aoe mwanamke mwenye mambo yake?
Unamkuta mtoto wa watu na kazi yake,biashara zake unataka aache hayo yote ili umuoe ni nani mwenye utimamu atafanya hivyo?
Ukute huyo jamàa yenu mwenyewe mnaemtetea kutunza familia mwenyewe hawezi ndio maana bibie anaomba muda aweke mambo sawa ndio aingie kwenye uzazi .
Huwezi jua ni Kwa faida Yao wote
Hili suala ni lao
Kwa hilo swali lako tumuulize pia Bibie kwanini ukibali kuolewa ukiwa na mambo yako? Na unaona kabisa ipelekea kusimama?

Jamaa yetu hatumtetei tunamsema kwamba amezingua mpaka hapo wife aseme ana mambo yake halafu mume hayo mambo huyajui na anakupangia huo ni uzembe
 
Kwa mazingira yalivyo hakuna hayo mapatano, kuna mmoja amemvimbia mwenzake, miaka miwili ya ndoa hataki kubeba mimba, biashara zipo, kazi zipo ukisema hautaki kubeba mimba leo kwa sababu zitasimama, hakuna siku utabeba utakimbizana na hayo mambo kwakuwa bado hautataka uyumbe na umri hausubiri ndiyo yale mwanaume anataka watoto wanne kwa sababu umri umeenda unajikuta unaishia kupata wawili
Haya
Mwisho wa siku watajua wenyewe.
Ndio maana siku hizi zinavunjika kimasihara
 
Kwanini asimalizie mambo yake kwanza kabla hajaolewa, ndani ya ndoa hakuna democras Mkuu, kwenye familia msemaji na muamuzi wa mwisho ni Baba pekee, usilete mambo ya majadiliano yasiyo na msingi, yaani mambo yake ni muhimu kuliko wewe?
Huyu mwanamke kama hataki mimba hatoipata! Ni yeye mwanaume aamue anaweza kuishi na mwanamke anayemaliza mambo yake kwanza au la. Kama hawezi apige chini, kwani sh ngapi?
 
Yawezekana hata uzazi changamoto kwake hivyo anajificha kwenye kumaliza mambo yake!

Akueleze hayo mambo yake uone kama yana mashiko,aache janjajanja!
 
Wanajukwaa, hali zenu jamani

Sasa ndugu zangu naomba niwaeleze kuwa Ndoa yetu ina miaka miwili sasa, na tangu tufunge ndoa na Mke wangu nimekuwa na hamu kubwa ya kupata mtoto. Lakini hivi karibuni nilimwambia mke wangu, Neema, kuwa nahisi umefika wakati wa kuanzisha familia.

Lakini aliniambia kwa sasa hayuko tayari kuzaa kwa sababu bado anamalizia mambo yake kwanza kisha ataamua sasa lini aweze kupata mtoto. Lakini pia hamu yangu ya kuwa baba na shinikizo kutoka kwa wazazi wangu vinanipa mawazo.

Na kwa kweli nashindwa kuelewa.
Kuzaa sio kazi, kazi kulea. Kumbuka miaka ya mwanzo mama, ambaye ametulizana kichwa na roho anaweka msingi mzuri wa makuzi ya muhimu zaidi. Kwahiyo kama amesema bado vumilia tu mwaego
 
Wanajukwaa, hali zenu jamani

Sasa ndugu zangu naomba niwaeleze kuwa Ndoa yetu ina miaka miwili sasa, na tangu tufunge ndoa na Mke wangu nimekuwa na hamu kubwa ya kupata mtoto. Lakini hivi karibuni nilimwambia mke wangu, Neema, kuwa nahisi umefika wakati wa kuanzisha familia.

Lakini aliniambia kwa sasa hayuko tayari kuzaa kwa sababu bado anamalizia mambo yake kwanza kisha ataamua sasa lini aweze kupata mtoto. Lakini pia hamu yangu ya kuwa baba na shinikizo kutoka kwa wazazi wangu vinanipa mawazo.

Na kwa kweli nashindwa kuelewa.
Kabla nitoe maoni yangu naomba kuuliza,

Mkeo ni hawa wanawake wasomi?...
Au ni hawa mabinti wanaofuga makucha ya kubandika?
 
Back
Top Bottom