Kwani mkuu unaishi dunia hii hii au kuna nyingine? Mbona hayo ni mambo ya kawaida saana? Tena hata wanaume sikuhizi baada ya ndoa hawataki watoto kwanza wanataka ku enjoy maisha yao kwanza ndio kisha waplan mambo ya watoto.
Wewe umefunga ndoa paap, honeymoon tu ushamjaza mkeo ujauzito. Mnarudi nyumbani anaanza kutapika , kutema mate na kulala siku nzima. Wewe unageuka mtu wa kumhudumia, mipango yako mingine lazima ilale. Kumbuka hapo ndoa changa hamjapata hata chance ya kujuana vizuri ( kwa kuishi pamoja). Visirani vya mimba vinaanza.
Miezi inaenda mtoto huyu hapa, mtoto halali usiku kucha ni kupeana shifti za kubembeleza mara ameumwa unakesha hospitali na asubuhi unatakiwa uingie kazini na ukirudi usaidie majukumu nyumbani na kukesha mkibembeleza mtoto. Utaiona hiyo ndoa ni adhabu.
Okay, ninachotaka kusema ni kwamba ndoa ni zaidi ya kuwa na watoto. Kuna mtu ukimwambia sipo tayari kupata watoto sasa hivi anakubali vizuri tu ila anataka akuoe muendelee kuishi. Na pia kuna ambao wanaoana kwa makubaliano ya kutokupata watoto kabisa (au nasema uongo
mzabzab ? .
Halafu niwaibie siri, huko kujidai kwenu sio waelewa ndio maana mnaoa mnashangaa hampati watoto mnazunguka hospitali zote mnamaliza kumbe ni mkeo tu hataki ila ameona una kichwa ngumu.
Ulizaneni hayo maswali kabla ya kuoana.