Mke wangu ananiita honey kwa sauti mbele ya ndugu zangu na Mama mzazi

Mke wangu ananiita honey kwa sauti mbele ya ndugu zangu na Mama mzazi

Niite jina lolote kulingana na mazingira tuliopo, kwanini unaniita sweetheart mbele ya ndgu zangu msibani, sio kila mtu anakutakia jema utaumiza wengi, tukiwa nyumbani kaniite lolote unalo taka, Sie wa Africa tuna utamaduni hatuonyeshe mahabah hadharani kabisa, mimi binafsi lina ni kera sanaaa
😂😂😂😂 sawa chief
 
Huu ni mwaka wa 10 nikiwa na mke wangu na tuna watoto watatu, tunaitana Dear miaka yote tangu tukiwa wapenzi mpaka sasa, iwe mbele ya ndugu zangu au ndugu zake hata wazazi na sijawahi kuhisi vibaya naona poa tu hata watoto wetu wamezoea, sijawahi kumuita mama flani au kuitwa baba flani au hata kuitana majina.
Sasa sijui kwako shida inatoka wapi?
Hahaha umenikumbusha mbli mam angu alikuwa anamuita baba kwa jina lake halisi kbsa Johnn

Mkuu kataza hili jambo mambo ya kizungu hayo
 
Soma hoja yangu sio kuiitwa hilo jina hapana tatizo ni mazingira anao niitia hilo jina, inakua kero, kwamiaka yote ananiita hivo tukia home sina shida nalo ila tukiwa msibani kwa ndgu na jamaa nikama linaleta karaha na chuki kwao.
Ndiyo upendo huo muache tu akuite hamna shida itabidi hao wanaokuzunguka wazoee.
 
Wewe una tatizo kubwa mkuu.Hilo ni jambo la kufurahia na hata kupeleka sadaka ya shukrani kanisani na siyo kunungunika unless kama ulioa mtu usiyempenda.
Mimi nina miaka kama saba kwenye ndoa nafurahia sana wife akiniita atakavyo hata iwe kanisani kwenye umati wa kutosha.
 
Back
Top Bottom