Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Bwana Mbuzi ipo hivi.
Kiwanja yes ulinunua na haukujenga. Hivyo ujenzi umeufanya ukiwa ndani ya ndoa.

Bila kwenda mbali sana, unawajibika kumuongeza mke kwenye umiliki wa hiyo nyumba.

Wengi watakushauri kulingana na hisia zao na siyo facts
 
Muache aandike,acha roho ya kimaskini. Kwani akiandika tatizo lipolyse wapi ?Atazikwa nacho in case akitangulia kufa ?
 
Bwana Mbuzi ipo hivi.
Kiwanja yes ulinunua na haukujenga. Hivyo ujenzi umeufanya ukiwa ndani ya ndoa.

Bila kwenda mbali sana, unawajibika kumuongeza mke kwenye umiliki wa hiyo nyumba.

Wengi watakushauri kulingana na hisia zao na siyo facts
Kiwanja ni chake alinunua yeye kabla sijamuoa nami nonacho changu ila first priority kwa ajili ya kukaa familia na watoto kuweza kwenda shule ni kiwanja chake ndio maana nikaanza kukiendeleza chake japo hata changu nimepiga msingi. Tatizo ni yeye alivyoaanza kubadilika baada ya kuhamia na sasa ananyemelea umiliki. Sina tatizo kama umiliki ukiwa wake lakini akabaki na tabia yake ya awali lakini kwa dalili alizoonesha ndoa itakuwa mashakani
 
Kiwanja Acha aandike jina lake,kutaka au kulazimisha na jina lako liwepo si u gentleman ukizingatia alinnunua kiwanja yeye. Kujenga ktk kiwanja chake iwe kama umempa zawadi na isiwe sababu ya wewe kujimilikisha kisa vyumba viwili ulivyosimamisha
 
Huwezi kumwachia tu. Yaani mwachie tu afanye anavyotaka.

Ana akili za kimaskini sana.
 
Mimi alitaka tuandike majina yetu wote wawili kwenye hati. Nikafanya mpango likasndikwa jina lake tu.

Najua hata ikitokea mgogoro wanangu watakua mikono salama. Ikitokea nimetangulia mbele za haki kabla yake, hawatapata msukosuko kutoka Kwa ndugu zangu.

Mie naweza kuanza maisha popote nikaishi hata kwenye Banda, kama wanangu wako salama inatosha.

Pia ni fikra pitiful sana kuanza kuhangaika na umiliki wa Mali mnapikya kwenye ndoa, changamoto zipo kwenye ndoa zote, kujikuta sana kwenye nani anamiliki kipi kati yenu ni dalili ya mahusiano hafifu au ukosefu wa afya ya ndoa. Ni kama vile mnaishi Kwa kutegeana na wakati wowote mnaweza kutengana.
 
Niwie radhi kwa kutokusoma kwa makini post yako

Ni kwamba, umiliki wa nyumba ni wenu wawili na hili anzia ustawi wa jamii ngazi ya Tarafa ili kuweka kumbukumbu vyema na wana utaratibu wa kuwaelewesha wanandoa mambo haya.

Pia kumbuka hiyo nyumba imejengwa after marriage kila mali inayopatikana ni mali ya wote equally....

Unaweza kumtafuta mwanasheria akakushauri vyema kuhusu hili
 
Nakuongezea jambo.Kitu cha mke hubaki kuwa cha mke daima.Na cha mume huwa cha familia.Usipoelewa nakuchapa makofi bwana mbuzi.
Hahaha! Nipo tayari kuchapwa makofi kama nina kosa. Ninachong'ang'ania hapa Mimi sio umiliki bali ni madhara ya ndoa yetu baada ya umiliki wake maana kuna hali ambayo Mimi sinaandika humu baada ya kuihamishia familia pale kwenye hiyo nyumba ambayo kuna vitu nisipo virekebisha mapema vikikomaa vitakuwa na madhara makubwa kwenye mahusiano yetu ya ndoa na itaathiri ustawi wa watoto wetu kitu ambacho Mimi sitaki kitokee nikiwa hai nahitaji watoto wangu wakue katika maadili mema na niwape mahitaji yao kadiri ninavyojaliwa na Mungu
 
Mkuu tumia akili ili umfilisi biashara yake ili heshima irudi ndani ya nyumba, wanawake waki Afrika wakipata pesa wanaweuka.
Kumfilisi sitaki maana maisha haya huyajui nataka ajue biashara asiwe tegemezi maana huwezi jua nani anatangulia.
 
Asante mkuu you are gentleman!!
 
Umemaliza
 
Usiruhusu hicho kitu,kataa kwa nguvu zote,huyo anakujaribu aone uta Fanya maamuzi gani,
Weka msimamo mpaka aogope,
Wa kwangu alishawahi kuleta story kwamba viwanja ninavyo nunua tuandike majina yetu wote wawili,nikamwambia kama anaona maisha yake hayana uhakika kuwa na Mimi,na Mimi kama mmiriki wa mali zinamfaidisha yeye na watoto,basi abebe vitu vyake asepe,aende akatafute dume limnunulie viwanja!!
Miaka mitano imepita sasa,alishika adabu,amekubali matokeo
 
"Ndugu zako wanakuombea sana usipate mali ila wanakuombea usalama na amani.Mpenzi/Mke wako anakuombea Upate mali ila hakuombei usalama na amani anataka ufe arithi mali"

Mwisho wa nukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…