Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

Dah pole sana. Kwangu mimi haikuwa mke ila rafiki wa kike. Yani tukiwa kwenye kundi la marafiki au watu tumetoka nao... atanikumbati... kudeka... kunipiga mabusu.. mara aniambie nimkiss... mara nimshike kiuno... mimi nilikuwa sipendi kwa sababu nina aibu sana... kweli watu hutofautiana..
 
Mumeo utakua nae proud hadharani hata akivaa kama Koffi Olomide?
au utamtanguliza kiaina....hahaaa..

kweli labda anaandaliwa kuachwa
Ha ha ha ha kuvaa kama koffi olomide si mchezo....lkn kama tatizo na uvaaji huyo mwanamke angemwambia mume wake kua napenda uwe unavaa hv,tena ana mnunulia mwenyewe.ndivyo wanavyofanya wanawake wenzake kumbadilisha mtu mtindo wa mavazi lkn sio Ku mkwepa...huyo mwanamke Hana mapenzi na jamaa.
 
Pole sana kaka angu,
Nimeumizwa na maneno yako coz I think I feel what you feel,

Kiufupi mkeo hakupendi na anahisi hamuendani, yani ameku shusha thamani yani hata mkiwa na watu wengine anahisi unamtia aibu muda wote,

Kuzaa nae si shida, yupo na ww afanyaje tu ila anajua safari yake bado yaendelea, ana matumaini iko siku atakutana na mtu wa size yake,

Wewe sio mbaya wala sio mzuri ila kwake anakuona unakasoro flani,
Huenda ni mfupi hlf yy mrefu au wote ni wafupi so anahic km hampendezi,
Huenda ni mweusi sana hlf yy ana rangi au nyote ni weusi so anahic km hampendezi,
Huenda mnene sana una likitambi akiongozana na ww ana hic kero,

Ila kabla hujawaza kutafuta mwngn,
Kaa nae chini mzungumze kwa upole, huenda ana kitu atakwambia.

Pole sana.
 
huyo mke kiboko hata kuongea anakuminya mkono dah we siku nyingine akikuminya na wewe mminye then endelea kuchangia mada iliyopo dawa yake tafuta bodyguard wakike uwe unatembea nae around kwa mitoko yote aone wivu labda atajirekebisha
 
  • Thanks
Reactions: nao
HAHAHA AISEE INAELEKEA KUNA JAMBO ZITO SANA NYUMA YA HII HABARI WEWE HUJAJUA TUU..MDADISI TARATIIB IPO SIKU ATAFUNGUKA IKIBIDI MUHOJI MKIWA KWENYE GEGEDO TENA KAKOLEA ANAKARIBIA KUKWEA KALE KA MLIMA KA MARAHA UKIONA ANAKUTOLEA NJE KUJIBU WAKATI HUO FANYA KAMA WATAKA KUMKATISHA UTAMU ATAKWAMBIA TUUUU HAHAHAHA UWII MAGU YUKO WAPI ANIKAMATE MUDA WA KAZI NAANDIKA MAMBO HIZI😱😱😱

Hahahahahaha
 
Fanya utoke outing na Mdogo wake inapotokea ila ndo usimtongoze sasa shemejio akikuuliza why unatoka na Mdogo wake! mwambie mdogo wake yuko comfortable na wewe mtakapo akilalamika zaidi mpe white&black sasa ila kwakuanzia anzisha huu utaratibu wakutoka na shemejio na usimwache mkeo kisa kutoka wote atachange taratibu tu.
 
dah hili lako linahitaji ushauri wa hali ya juu... Nakuahidi nitarudi hapa na Ushauri ambao kiasi flani utakusaidia
 
Wadau heri ya mwaka mpya,

Wife amekuwa hapendi kuongozana nami katika safari mbali mbali misiba, sherehe, outing na kadhalika, sio kwamba anakataa moja kwa moja bali atatafuta sababu ili twende tofauti, na akikubali kwenda anakuwa uncomfortable na uwepo wangu.

Mwezi uliopita wa 12 tulisafiri wote kwenda up country nyumbani kwao mkoani kwa mapumziko ya end year, tulianzia mkoani kwetu, mwisho tukamalizia kwao, sasa tukiwa kwao, mdogo wake wa kike ndie alikuwa akizunguka nami mjini kutalii na kunionesha sehemu mbali mbali, wife alikuwa akinipiga chenga ndipo shemeji akaamua kunipa kampani.

Tuliijadili sana hii tabia ya dada yake ambayo hata yeye akasema ameiona kwa muda mrefu sana, anashindwa kuelewa tatizo ni nini? Sababu sina ulemavu, mwonekano wangu ni wa kawaida, wakiitwa ma handsome siwezi kutoka, lakini pia wakiitwa wabaya pia siwezi kutoka, ni wa kawaida.

Siku ya kuondoka Arusha, tukawa na ugomvi mkubwa sana kwamba nakosaje aibu kiasi kile, kuzunguka na mdogo wake hadi watu kunielewa vibaya, kiasi kuwa akakataa kabisa kwa hasira shemeji asije na sisi Dar maana huwa tunaishi nae, hadi wazazi wao walipomuamuru akakubali.

Tabia hii imenichosha sana kufikia hatua najiona sina thamani, tukienda harusini au outing ya pamoja na marafiki pamoja na waume zao utashangaa kila nikitaka kuchangia mada ananiminya mkono nisizungumze labda nitaongea jambo la kumuaibisha wakati mimi kwanza sio muongeaji, waume wa marafiki zake wataongea wee mimi nipo kimya, mimi nikichangia tu ni ugomvi, ananikosoa mbele yao kila nalochangia tena kwa kunishushua, hivyo nakaa kimya muda wote hadi wengine waulize mbona huongei.

Nilishajiuliza huenda huwa naongea pumba, hata hivyo hapana, mimi huwa ni mtu mwenye kuchagua maneno sana kabla ya kuongea.

Sasa naomba mnisaidie mawazo, tatizo ni nini hasa? Ni suala la muda mrefu hivyo nimeshachoka, nataka kufanya mabadiliko, nahitaji mke mwenye kunithamini na ambae yupo proud of me nahisi huyu hanipendi Ingawa tuna watoto wawili.

Nawasilisha kwenu

Mkuu ukiona manyonya.....?
 
Mkuu pole sana ila nigependa kujua Hugo mke ni kabira gani??? Hapo ntakupa jibu sahihi
 
Inawezekani ni tabia yake tu. Kuna wanaume wanatamani wangekuwa kwenye viatu vyako hamna masuala ya kugandana barabarani, hamna kubebana kwa nguvu kuonana na marafiki zake ambayo stori zao hata hazivutii. Japo kwa kweli mnabidii once in a while muonekane pamoja no matter what.
 
Utamponza mtoa mada wewe! Yani katikati ya raha tena aanze maswali eti "kwanini Jumamosi iliyopita hatukuongozana kwenda arusini"
Hahaaaaaaa, kwanza atasahau swali
 
Back
Top Bottom