kama Bibi yako miaka ya 1970's alikuwa mjamzito means baba/mama yako atakuwa amezaliwa around 1975-1979 hivyo kwa haraka haraka utakuwa unamiaka kati ya 20 mpaka 25.
Kwa umri huo bado haujajua chochote kuhusu ndoa ,unaendeshwa na mihemko ya bata za online ,vitabu vya dini vinasema Mwanamke muheshimu mme wako na mwanamme mpende mkeo na ishi naye kwa akili ,unajua maana yake?
Kwenda kwa jirani tena Mme wa mtu hata mkewe hajui kwamba unatafutiwa kazi ni sawa? Kutafutiwa kazi ni jambo zuri sasa kwanini amfiche mmewe? Kwa ufahamu wako una cases ngapi ambazo mwanamme alimtafutia mkewe kazi halafu mambo yakanyooka? Mimi nina cases karibi 20 ambazo m/me alimtafutia mkewe kazi au alimfungulia biashara ambazo 15 wanawake waliwaacha waume zao na hizo 5 ni tia maji tia maji.
Nani alikwambia fedha ya mwanamke inasaidia mambo ya nyumbani? kati ya wanawake 100 wanaofanya kazi ukipata wa 5 fedha zinasaidia familia ya nyumbani basi shukuru...Mwanamke mama wa nyumbani ndiyo mzuri kuishi naye ,swala la mbele ajuaye Mungu si uliona watoto wa hans pope walikuwa wanalia kwenye mitandao hawana kitu ingawa baba yao alikuwa bilionea na biashara kibao? Unataka kusema mke wa hans pope alikuwa hana biashara au kazi? Familia ngapi Baba ana kazi na mama hana kazi(mama wa nyumbani) zimedumu na watoto wamekuwa watu wakubwa tu serikalini/private sectors? Familia ngapi zimelelewa na Mama bila baba na zimekuwa vizuri?
Bado mdogo sana kuzungumzia changamoto za ndoa ,mwanamke akishaanza jeuri fukuza ,na wengi 99% wakienda huko wanaishia kufukuzwa pia na 1% wanaishi maisha mabovu kuhofia kuchekwa kwa walichofanya wengine wanaishia kuambukizwa kazeze maana wanaenda kujiachia waliona wanabanwa sana kwenye ndoa.
Mkuu, binafsi bibi yangu alitafutiwa kibarua na babu, wadogo zake bibi walisoma ila kwa vile yeye alikuwa first born wazazi wake hawakuwa tiyari na uwezo wakati anamaliza darasa la saba. Hela ya bibi mimi mwenyewe nimeila, sahivi yuko mid 80s anaumwa. Ila babu hajaila hiyo hela. Wewe umeoa kwa ajili yako tu, watoto na wajukuu je?
Wadogo za kiume wa bibi hao nisiwazungumzie sio hoja, wa kike kila mmoja alikuwa na kazi yake. Wa kwanza mumewe niliambiwa alikuwa mtumishi wa umma ila akaacha kazi Rais Mwinyi alipoingia madarakani, akafanya biashara kwa mafanikio ile ruksa ya mwanzo. Akafariki kwa ajali, mjane alikuwa mtumishi wa umma akaendesha familia, akasomesha watoto.
Ndugu wa mume kwa vile mke sio jamii yao wakagawana mali wakaacha yatima na mjane hawana kitu. Bila huyu bibi kuwa na elimu kidogo na kipato kiasi wanae wangeishia kuuza supu ya utumbo, na angeuza vitu ili kukidhi mahitaji madogo.
Mwingine aliolewa hakubahatika kuzaa akaachwa na mume wake. Hakuwa na elimu wala kazi kubwa huyu kaka zake wakampa mtaji amefanya biashara Kibaha miaka sasa.
Mwingine alifanya kazi, mumewe alifariki early 2000s akaacha vitu kiasi. Mke akadunduliza akastaafu akajenga nyumba akafariki akaachia wanae.
Hata mabibi wasio na ajira walikuwa wanaenda kuandaa mashamba, kuvuna, kulisha mifugo, kutengeneza hata gongo ili watoto wavae viatu shule na wanunue daftari. Kuna jamii wanaume wanacheza bao na kupiga soga, mke ndio anachota maji, kulima na kuchanja kuni.
Huu utaratibu wa kuvundika wake ndani mmeutoa wapi.
Tunaelimishana hapa wala sio kupingana.