Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Habarini wapendwa.

Wadau, Mke wangu kapata kazi Taasisi moja ya Kiserikali lakini Kapangiwa Mkoani (Shinyanga). Tupo na watoto wawili sasa, mmoja ni mdogo ananyonya (Mwaka mmoja).

Sasa nina changamoto moja,

Kwanza nimemshauri kwa kuwa ndio anaenda kwenye mazingira mapya asiende na watoto awaache, ila yeye anahisi hataweza bila watoto hasa huyu mdogo, hiki kitu kinaniumiza kichwa sababu hatujui ni lini taasisi yake itakubali kumhamishia hapa nilipo.

Wazoefu naomba mawazo yenu!

Ahsante:
Tutampokea Kwa bashasha zote,wewe Baki unalinda nyumba huko uliko
 
Wewe baki alone acha mama abebe watoto na msaidizi

Achana na mambo ya Hali ya hewa. Hata kule Kuna maisha fresh tu

Muhimu, narudia tena muhimu dumu kwenye mawasiliano na mkeo akiwa huko
Mawasilia o ya whatsapp kwa mke na mume ni uwongo tuu
 
Hii kazi hakwenda, na nadhani ukifuatilia kwenye hilo thread hapo nilisema... this time around kapata kwenye Taasisi ya Kiserikali
Wewe ndo unawaweza watu waliopinda wa hapa JF hapo lengo lake uonekane muongo Safi Shem Darling wangu.Haya tuendelee na madam jibu umechagia vipi?Mimi Kama Shem wako nakushauri acha waende huko watakuwa salama tu bila neno.Wewe kubaki na watoto is Big No.Watoto Wana vile vihoma vya kupandisha joto usiku is only a mother can understand this and take immediate measure to it.
 
Kuishi Mkoa mwingine na mkeo awe anafanyakazi Mkoa mwingine, hapo ni suala la muda tu. Baada ya mwaka mmoja tu kilakitu kitakuwa wazi. Huyo mkeo atakuwa na mume mwingine na wewe utakuwa na mbadala wa mkeo.

Binafsi sitaruhusu kitu kama hiki kitokee kwa mke wangu. Labda kama anaenda kwenye semina ya wiki moja na kurudi lakini sio kuhamia kikazi.
 
Kuishi Mkoa mwingine na mkeo awe anafanyakazi Mkoa mwingine, hapo ni suala la muda tu. Baada ya mwaka mmoja tu kilakitu kitakuwa wazi. Huyo mkeo atakuwa na mume mwingine na wewe utakuwa na mbadala wa mkeo.

Binafsi sitaruhusu kitu kama hiki kitokee kwa mke wangu.
Too dangerous ,
 
Kwaiyo mkuu akienda uko itakuwa double chance?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kwa % huwa inakuwa hivyo....... hapo achague moja tuu huyu jamaa kumzuia asiende ama amuache aende.
Au akubaliane na lolote litakalokwenda kutokea japo wapo wanawake huitunza heshima ya wao kuwa mama. Hawagawi tupu abadani kama wanawatoto
 
Mzee baba ukitaka ujitundike ubaki na huyo mtoto,hasa watoto wachanga ni wasumbufu kinoma,mm nlidhani naweza kaa na mtoto nliachiwa 2hrs nliona kama wiki sitakuja sahau.
Huyu Housegal wangu anastahili kujengewa sanamu- maana sijapata tabu yoyote kwenye kulea hawa vijana wangu, tupo naye huyu Binti mwaka wa 6 huu
 
Huyu Housegal wangu anastahili kujengewa sanamu- maana sijapata tabu yoyote kwenye kulea hawa vijana wangu, tupo naye huyu Binti mwaka wa 6 huu
Mshukuruuu sanaa huyo bintiii...!! Kulea kazii sana aisee nashangaa jamaa Anavyolilia mtoto... Nahisi anataniaa hii ni chai
 
Wewe watoto wa mwaka mmoja utawaleaje mkuu?? Tena mmoja ndo ananyonya kabisa. Waache waende na mama yao. Wakifika umri wa kuanza shule waje kwako
 
Back
Top Bottom