Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Msaidizi yupo na ndio anaplan kwenda naye, hofu yangu ni hali ya hewa kubadilisha hawa watoto maana bado wadogo, mwanzo niliwaza huyu msaidizi abaki lakini niongeze msaidizi wa pili wa kulea watoto.
Kwani we ukisikia shinyanga unawazaje kwani? Hiyo hali ya hewa ina maana unataka kusema hakuna watu wanaoishi au unadhani shinyanga ni jehanamu???
Kwa taarifa yako shinyanga unayoiwazia wala sio kama hiyo. Shinyanga ni town tena pa kishua unless iwe ni shinyanga DC
 
Ndg. Watoto wako wanachangamoto za kiafya zinazazosababishwa na kubadili mazingira?

Ila wazazi wengine mnatia hasira sana. Mnadekeza watoto kama mayai. Mnatuandalia taifa la hovyo.

Kama hutaki watoto wahame mkoa tena wakakae na mama yao hivi kesho unaweza kumruhusu huyo mtoto ashike jembe akalime?!

Anyway, hata kama utawatafutia wasidizi elfu 7 hao watoto, unadhani watakuwa replacement ya mama yao?! Peleka watoto kaishi na mama yao huko.
Yaani sijui anadhani shinyanga ni rural sana au wanaishi watu gani sijui.
 
Shinyanga hakuna hali mbaya ya hewa ni jua na kavumbi kama mbugani, la hali ya hewa mbaya ondoa! Labda lingine
Na mjini pako poa simple tu!

Hata maeneo ya kupanga naweza kushauri atafute kambarage etc ni pazuri na karibu na town.. asikae mtaani sana kwa wananzengo
Kambarage, bugweto, burugalila, majengo mapya, mwasele, kitangili, nyanhende karibu na jeshini ndio sehem zilizotulia na zenye nyumba nzuri.
 
Habarini wapendwa.

Wadau, Mke wangu kapata kazi Taasisi moja ya Kiserikali lakini Kapangiwa Mkoani (Shinyanga). Tupo na watoto wawili sasa, mmoja ni mdogo ananyonya (Mwaka mmoja).

Sasa nina changamoto moja,

Kwanza nimemshauri kwa kuwa ndio anaenda kwenye mazingira mapya asiende na watoto awaache, ila yeye anahisi hataweza bila watoto hasa huyu mdogo, hiki kitu kinaniumiza kichwa sababu hatujui ni lini taasisi yake itakubali kumhamishia hapa nilipo.

Wazoefu naomba mawazo yenu!

Ahsante:
Hama Mfuate uishi nae,using'ang'anie kukaa Dar
 
Mwache aende nao Kama unayo nafasi kakae nao hata mwezi mmoja hivi ili kuweka mazingira sawa
 
Mwaka mmoja anaweza achishwa au unasemaje Mkuu, sema mawazo yenu yananisaidia hapa kumake decision
Wacha hizo mwamba mwaka mmoja huwezi kukaa naye wewe mwanaume unataka kutudanganya! Watoto waache waende na mama!
 
Kambarage pa kiduwanzi kule.

Nyumba za kizamani (zile za vyumba vitatu kushoto vitatu kulia katikati korido limejaa madumu ya wapangaji).

Maeneo classic kwa mtu aliyetoka Dar ni Majengo Mapya na Lubaga
Huyu naye anashauri kitu gani hiki? Eti Kambarage! Nyumba ziko Majaengo mapya, Viwanja Vya Mwadui, Bushushu, na Lubaga siyo mbaya!
 
Tatizo la nchi za kiafrika miundo mbinu ingekuwa ulaya treni za umeme dakika tu upo mji.
 
Back
Top Bottom