Mkeo aliwahi kukulaza lock up, baada ya kutoka maisha yalikuwaje?

Ningekua Mimi ndo Uyo mkeo ningehakikisha unalala huko siku 3 Na msamaha ungeomba wewe soon Mimi😡😡😡😡😡
 
A
Ilikua leo nipelekwe mahakamani,ila kwa sababu mlalamikaji amesema hana nia ya kuendelea na kesi na ameomba tuyazungumze wenyewe,so tuko hapa polisi kwenye dawati la jinsia sijui wanataka kutuambia nini.
Aisee pole mkuu hyo imeisha mnaenda tu kupewa counseling kwa siku nyingine but tayari wife atakuwa amekupunguzia spidi kwenye kudeal nae next time. Na pia atachukulia hiyo km gia ya kukutishia siku nyingine mtakapogombana so ni lazima tu utapoa kiaina. Maisha kwa sasa lazima yatabadilika mkuu.
 
Alafu wewe ebu njoo huku maana na shida na mtu kama wewe
 
Kuna shemeji yangu hivo hivo alimpiga dada akampeleka polisi alitolewa asubuhi na kesi akaifuta sasahivi wanaishi fresh tu ata ikitokea ugomvi anaondoka uko nje akirudi wanayazungumza yanaisha....nakushauri samehe tu mwanamke apigwi na akipigwa lisiwe pigo la kujeruhi mpige kofi moja tu begani au mgongoni ondoka katafute cha kukufanya hasira zipungue
 
Yaani hapo kosa ishakuwa wewe kulazwa ndani na sio wewe kumpiga yeye!
Wewe uli react ukampiga na yeye ka react akaenda kukushtaki. Nyote mmefanya makosa kama binaadam
Na kwa nini watu wazima mfike kupigana kama wtt. Wewe kwani huyo binti wa watu umekabidhiwa na wazee wake ili umpige au umtunze?
 
Mwanamke wa kukupeleka polisi huyo sio mke ni jangili. Mke yapaswa awe mstahimilivu na mwenye hekima ya kujua akipigwa ni sehemu ya maonyo kuwa anatoka nje ya reli. Sasa mke unampiga kibao tu kashakimbilia polisi kweli?!
Kama nimekuelewa ni kwamba mtu mmoja kumpiga mwingine ni maonyo, ila kupelekwa polisi kwa kosa la kudhuru mwili sio maonyo ni ushetani!!!!! Inafikirisha sana.
 
Msamehee mkuu. Ludi nyumbani uishi na mkeo. Uzi ni harakati tu katika kufika inchi ya ahadi. Ludi nyumbani mwamba.
 
Siku wife akifanya hivyo ndio basi tena, we will part ways.
 
Mimi sijawahi

Lakini kichwani mwangu mimi ni kwamba mtu yeyote (siyo mke tu bali hata awe ndugu jirani au rafiki) akishanipeleka polisi, ustawi wa jamii, mahakamani, takukuru au ofisi yoyote ya serikali ya kimamlaka basi tayari huyo namuweka pending katika ubongo wangu. Mara nyingi ikifikia mambo hayo huwa nakaa upande wa kushindwa nauliza tu anavyotaka yeye natimiza kisha navaa tinted mpaka akili imkae sawa. Huyo anaingia kwenye black memory yangu

Labda iwe kwamba njia zingine zote alifanya zikagonga mwamba ikawa hakuna namna yoyote zaidi ya kunipeleka huko lakini siyo kufanya kama fasheni. Mfano jirani mmepishana kidogo kuhusu mpaka hajakuita mzungumze hajawaona hata wazee wanaoweza kukuweka kitako wala hajafanya chochote moja kwa moja kakimbilia ofisi za ardhi kisa anapajua!

Kuhusu ushauri nakushauri chukua uamuzi ambao hauna madhara pande zote (yaani uamuzi unaojenga zaidi kuliko kubomoa)
 
Kila binadamu ana kiwango chake cha uvumilivu

Ikifika hiyo hatua ni rahisi sana ku-react Kwa kufanya jambo ambalo Kwa muda huo anahisi litampa amani

Kitendo cha Mkeo kukupeleka kituo cha Polisi, kinaonesha alivyoshindwa kuzuia hasira zake kwako mara baada ya wewe kumpiga.

Tushukuru Mungu tunaishi Tanzania, Nchi ambayo haijaweka Sheria Kali kuhusu Mume kumpiga Mke/mpenzi

Ingekuwa Nchi zilizoendelea, huwa Wana mashtaka makali sana juu ya hayo

Huku Tanzania Mume anampiga Mke wakati mwingine hadi kumvunja shingo/Mkono ama wakati mwingine hata kumtoa Uhai

Kumbukeni adhabu aliyopewa Mwanamuziki Chris Brown baada ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna

Wanaume tujitahidi kuzuia hasira mbele ya hawa wapenzi/wake zetu

Wanawake kiasili ni waongeaji, na kamwe Wanaume hatuwezi kuwafikia Kwa kuongea

Hivyo vyema wakati mwingine kujiepusha hata Kwa kwenda kibanda umiza kuangalia Mpira, hata kama nyumbani umelipia king'amuzi chako

Wanasema kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake...

Tukumbuke kuna baadhi ya Wanaume wenzetu walishindwa kuvumilia maneno ya wake zao wakajikuta wanawapiga kawaida, lakini kumbe Mke ndiyo anafariki Dunia hivyo kuishia kufungwa jela maisha
 
Hhhhhh turudie wasamehe
 
......Kachuke begi, then potea mwezi mzima,ngoja kwanza mashosti zake waendelee kumpa ushauri.
 
Kuna lugha za maudhi tu alinitamkia, nikajikuta nimemlabua.
Kama ungempiga kimahaba sizani kama angeumia kiasi hicho akatoka nje, kwanza mke na mme inatakiwa ungemalizia chumbani sasa wewe unampiga mtu kwa mkanda? Halafu sasa wewe kwanini umruhusu atoke nje akiwa analia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…