Mkeo aliwahi kukulaza lock up, baada ya kutoka maisha yalikuwaje?

Mkeo aliwahi kukulaza lock up, baada ya kutoka maisha yalikuwaje?

Kuna saa lazima mpitie kashkash, inawakumbusha iwapo bado mnatakana. Mahusiano yakipoa sana nayo yanaboa.
Sasa badala ya kurudi wakayamalize eti wanamshauri sijui apotee aende mwezi au miwili alaa watoto hawa wa 2000 atalipa na mabua, yeye katoa kipigo mwisho kaenda huu kwenye ndoo kati watu 30😂😂😂 arudi nyumbani tu.
 
Msamehe mke wako muendelee na maisha yenu na mlee watoto kama kawaida.
Kwanini wewe ujione una haki ya kumpiga mikanda 'hatari' alafu yeye kukushtaki uone nongwa? Angeshupalia ukae mahabusu ingekuwa ishu nyingine, lakini kitendo cha ku react haraka kufuta kesi ni wazi hata yeye alichukia ulivyo mpiga hata kama alikosea.
Mzee hao watu sometime michosho sana. Usikute mchizi katikati ya majibizano aliambiwa unafikiri mimi ni kama mama yako asiyeoga. Come On.
 
Hali zenu?

Wakuu, siku ya jumatano majira ya saa 1 jioni nikiwa nimefika nyumbani kutoka mihangaikoni, kulitokea kutokuelewana na wife,nikajikuta napandwa na hasira nikamshika nikachomoa mkanda wangu wa suruali nikamtandika nao hatari alivyopata upenyo akakimbilia nje.

Kumbe mashosti zake wakawa wamemshauri akimbilie kushtaki polisi, akaenda kituo cha police kushtaki,baada kama ya lisaa hivi nikasikia nagongewa na balozi wa nyumba kumi akiwa kaambatana na Askari polisi wawili, wakaniambia nahitajika kituo cha police kwani mke wangu kaenda kushtaki kuwa nimempiga.

Sikuwa mbishi nikawaomba nibadili nguo na niweke mazingira ya nyumba sawa kwani watoto na dada wa kazi hawapo.

Basi bana nikafika kituo cha police pale kaunta nikamkuta wife kakaa yuko na mashosti zake kama wawiili nikachukuliwa maelezo yangu kisha nikafunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili, nikaingizwa lock up, kwa sababu ilikua usiku afande mmoja hivi akaniambia kosa linadhaminika kama kuna jamaa zangu wako around niwacheck waje wanidhamini

Lakini pia akanishauri kwa jinsi anavyoona nina hasira bora nilale tu mle lock up kuepusha madhara kwani nikisema nitoke usiku ule ningeweza kumdhuru zaidi wife na pale lock up ni sehemu salama zaidi. Basi nikawa nimemuelewa yule afande nikatulia mpaka asubuhi,kulivyokucha nikaomba simu yangu pale kaunta nikawapigia jamaa zangu wakaja wakaniwekea dhamana.

Hapa nilipo toka nitoke lock up nimeona nikae kwanza kwa jamaa angu kujiepusha na huyo mwanamke,ameisha enda police mwenyewe kuwaambia hana nia ya kuendelea na hiyo kesi hivyo anaomba ifutwe, Askari kama kawaida wamemtoa pesa kidogo.

Sasa toka jana naona ananitumia watu kuja kumuombea msamaha kuwa alikosea kunilaza lock up.

Hapa niko stranded nimsamehe au nimfanyaje na baada ya kumsamehe maisha yetu hapo ndani yatakuwaje?

Kama kuna yeyote amewahi kupitia hii changamoto anisaidie mawazo.
Mara tatu kwangu,nimepajua selo na kupazoea ni huyu mwanamke alinipeleka.
Mpk nilihama kwangu nikaanza maisha upya mbali huko.
Can you imagine mpk leo huyo yupo ananiita Baba, mzee, Baby, asali,darl.
Miaka 25 imepita.
 
Nampongeza afande kwa busara kubwa aliotumia kukushauri kulala lockup. Kumbe wakati mwingine lockup ni kweli ni kwa ajili ya usalama wako na wa mtu mwingine. Ungetoka nje usiku huo bado emotions zipo juu chochote kibaya kingeweza kutokea

Afande alimshauri hivyo huku ana m please mke wa jamaa, na baada ya mda huwa wanawala wake zenu maana ni mlango mzuri sana wa kupitia!
 
Kwa hiyo yeye alivyompiga mwenzie sio kosa safi sana kwa huyo bibie iwe funzo kwa wenzie🐒,Kwanza ulimshushia kipigo kikali sana mpaka akakupeleka police na huenda ndio tabia yako kumpiga ila siku hiyo ulizidisha dozi hata ningekuwa mimi ningekulaza Selo dadekii.
Umlaze selo mtu unayempenda? Hapo ndoa ishaanza kufa kama bigjii imeanza kuisha sukari ndio maana kuitupa huoni uchungu.
 
Yeye anajiona ana haki sana, japo kampiga, wanaume baadhi niwanafiki sana, hapo utakuta ndugu zake wanamperemba aachane naye, na huenda kosa lilikuwa lake.
Mwanamke wa kukupeleka polisi huyo sio mke ni jangili. Mke yapaswa awe mstahimilivu na mwenye hekima ya kujua akipigwa ni sehemu ya maonyo kuwa anatoka nje ya reli. Sasa mke unampiga kibao tu kashakimbilia polisi kweli?!
 
Sijui nisimulieee au nipiteee.....🤔🤔🤔🤔

Ukubwa jalala, nyani mzee amekwepa mishale mingi.
 
Msamehe lakin kaa nae kikao kizito mpe term and condition. Muelez kwann ulimuadhibu na ajue waz Kua utamuadhibu tena akizngua
 
Back
Top Bottom