Mkinga sio mtu wa kushindana nae kwenye Biashara!

Mkinga sio mtu wa kushindana nae kwenye Biashara!

Unajua kujisifu na showoff ni tabia za maeneo nipo kaskazini zaidi ya miaka 8 watu wa huku wanatabia ya kujiona bora hata kwenye vitu ambavyo hawana

Ila watu wa nyanda za juu kusini hawana tibia za hivyo ni vitendo tu

Ni kweli, watu wa Kaskazini sio kwamba wanamaisha mazuri Sanaa Ila ni tabia Yao kujiona superior kuliko wengine,
Na hiyo inatokana na kuwazidi wengine Kwa baadhi ya vitu.

Ila mbona hawajioni Bora kuliko Wazungu 😄😄😄
 
Ni mzunguko sana ndugu yangu hasa kwa biashara mpya inayoanza. Mimi nimejenga sheli imekamilika kila kitu bado mtaji wa kuweka mafuta tu. Nimeomba mkopo kwa dhamana ya ardhi huu mwezi wa nne sasa bado sijapata kisa ni biashara mpya haina hizo business financial report.
Pole sana mkuu nadhan wengine hatujawahi kukutana na changamoto sababu ya connection
Hebu jipige pige uyaweke sawa
 
Top 20 nimekuambia hata hao Wakinga hawapo,

Tatizo unaleta ubishi badala ya kujadiliana ili kujifunza.

Nimekuambia wewe sio mchaga wala Mimi sio mchaga.

Ila hawa wenzetu Wachaga Kama unafuatilia biashara nyingi hapa nchini wapo karibu kila sekta.

Hao wakinga bado Sana, labda wapo kwenye sekta tano tuu,
Hata hivyo bado wanajitahidi kuja vizuri.

Wewe unaleta Ligi za vijiweni.

Level za Wachaga ni wahaya, Wasukuma, Wanyakyusa, Na baadhi ya watu wa Pwani wenye ukaribu na Waarabu
Sijakataa maana yangu wanahang kweny biashara za middle wote jua dunia inaenda Kwa kasi nimewajua wachaga mda sana pia ni ndugu zangu yaani shemeji zangu huko moshi nimekaa

Ninachomaanisha mtoa mada jamaa wanakuja Kwa Kasi mno wakinga mi nimewajua juzi juzi tu ila nilisoma na machalii kama wanna nawafahamu mmoja tumekutana humu Kwa ishu za biashara kwanza ni muaminifu ndo nikaona nijue zaidi kabila lao alinipeleka kariakoo duh ilikuwa 2017 hata kusikia wakinga jina nilikuwa sijui dadaq machalii wanashusha containers hapo bandari Wana mpaka SUV ni wadogo nikasema Hawa jamaa ni noma elimu kidogo wanaitumia vizuri

Na hao washkaji nawafahamu Wana maisha safi machalii range 27 mpaka 30 miaka sikuwa nawajua ila hakuna ana viduka vidogo Dili zao mbao na nguo kuuza Kwa jumla wanashika pesa sema ni wachache yaani kabila lao no dogo

Unaposema wahaya wanashindna na 2achaga Kwa elimu ila biashara sio fame labda wasukuma kweny madini wako nondo

Nenda moshi kaulize madon utakuta ni wale weny ishu za madini ndo wengi akipiga trip Moja moja kashika pesa ndefu kuliko Hawa wa mabasi ni mali kauli
. The smartest guy alikuwa mengi namkubali mno alivuka mipaka Ile ya kuwa na akili za kizungu 🙏🙏🙏alituwakilishw vyema ila waliobaki

Wamiliki wa mahoteli wengi sio wote fuatilia waliibia serikali enzi izo walikuwa wajanja wakapata mitaji mirefu hata huyo ulimtaja sijui mmiliki wa prescious air walipiga mihanya serikalini japo sio wachaga tu ni wengi
 
Wakinga bado hawajafika level ya kujisifu bado wako chini huko.

Huwezi jisifu Kama huna cha kujisifia.

Huoni wahaya unafikiri wanajisifu Bure😀😀
Sawa kwani wahaya Kwa elimu Kuna wa kuwafikia hapa bongo wale hawaibi mitihani Wana damu ya elimu
 
Nimekaa na waaarabu sana kitu nakuambia wachaga sio matajiri wanaomiliki biashara kubwa ni wachuuzi aslimia 90 na hakuna top agent kama walivyo waarabu ndo maana top Ten alikuwa mengi tu ambaye ni marehemu

Tofautisha biashara kubwa na uchuuzi Sasa njoo wanamiliki biashara hapo kati nenda kariakoo sema wakinga kwa idadi ni wachache ila vijana wakikinga wanashika peda ndefu mapema hawana kelele labda vunjabei tu ila wengi wanapesa chafu
Exactly
Pale kariakoo wakinga wanapesa ndefu mno na wanaenda wakitokea tunduma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna mambo huyaelewi vizuri kuhusu hii nchi itakuwa[emoji3][emoji3]

Unapozungumzia kuhusu biashara hii nchi Wachaga ndio the Top, wewe unaleta biashara za nguo za milioni 100[emoji1][emoji1] hao unaitwa matajiri.

Biashara za Wachaga ambazo unaziita za wachuuzi

1. Sekta ya anga
Wachaga ni moja ya kabila yenye kufanya biashara ya anga Kwa kumiliki baadhi ya makampuni ya Ndege, mfano Kampuni za Precious Airlines na zamani Fastjet alikuwepo Lawrence Masha akiongoza kaa share nyingi za Hisa.

Huenda hata Ndege tuu hujapanda ya kutoka DSM kwenda kwenu Mtwara[emoji1][emoji1] hivyo huwezi elewa hizi mambo
Sasa Kama kumiliki biashara za usafiri wa Ndege ni uchuuzi Sawa.

2. Sekta ya usafirishaji na mabasi.
Wachaga ndio wanaongoza Kwa kumiliki makampuni ya mabasi,
travel agency za tour Guide, na hapa ni ukiachana na Wahindi na waarabu.


3. Sekta za Utalii, Mahoteli na STAREHE.
Wachaga ndio wanaongoza Kwa kuwa na mahoteli, sehemu za starehe na hii wengi Hufanya Kwa sababu ya kazi ya utalii.
Wengi WA Wachaga wanamakampuni ya Utalii hivyo wamejenga hayo mahoteli Kwa ajili ya wageni wao.
Usishangae Moshi na Arusha kuwa kinara wa utalii ukadhani sehemu zingine hakuna mbuga[emoji3][emoji3]

Hizi mambo huwezi elewa.

4. Wakala wa vipuri vya magari.
Wachaga kwenye sekta za UWAKALA WA vipuri ndio wanashika namba moja, Kama wewe unayajua magari sio ajabu ukikuta chata kwenye Vipuri vya magari vikiwa vimeandikwa 7General/Saba General ndiye aliyekuwa wakala mkubwa wa vipuri vya Magari hapa nchini.


5. Biashara ya Magari
Wachaga ndio wanaongoza Kwa biashara za kuuza magari.
Sio ajabu Wachaga ndio kabila pekee ambalo atu wake wanajua Aina za magari kuliko kabila lolote hapa nchini.

6. Biashara za Shule.
Wachaga ndio kabila la Kwanza Kwa umiliki WA shule binafsi hapa nchini wakifukuziwa na Wahaya.

7. Nenda sekta za Fedha na Benki hasa pale CRDB alafu useme Wachaga ni wachuuzi[emoji1][emoji1]

8. Sekta ya madini

Tatizo lako unawajua Wachaga Wale wa Tabaka la chini na hii ni kutokana na unaishi mazingira ya namna hiyo.

Mimi sio mchagga Ila kwenye hii nchi utaanza na wahindi, waarabu, Wachaga alafu Sisi wengine tufuate.
Wewe mchaga wa tabaka lipi?

Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Kwa akili yako Mabasi Kama Kilimanjaro express, marangu, Mtei, BM coach, Kimotco, Machame, Lim Safari, n.k Wachaga wanafanya uchuuzi WA gari hizo🤣🤣

Na kwenye Ndege pia nilizokutajia wanafanya uchuuzi.

Hii ndio shida ya kuzaliwa masikini
Wewe kwenye usafiri wa vyombo vya moto wajinga wanavyo vingi sana,mfano mdogo ni superfeo..
 
Kuna watu wanatoka mikoa ya mbali wanaenda kufanya biashara njombe kwa wakinga na wanafanikiwa!,binafsi najua kuwa uchawi upo lakini siamini katika uchawi,mfano umekuja dukani kwangu unahitaji kununua pasi ya umeme halafu mimi sina je utanunua sufuria la kumchemshia maji kisa mimi nauzia uchawi badala ya pasi ya umeme!?
Maneno rahisi mtaji wa hawa jamaa ndio uchawi, kwa sababu wana uwezo wa kuwahudumia watu wengi kwa wakati wanaohitaji hizo bidhaa. Sasa kama mtu huna mtaji wa kutosha unawezaje kusema huuzi wakati wateja huna mtaji wa kuleta bidhaa zinazotakiwa kwenye biashara yako.

UCHAWI NI MTAJI KAMA HUNA MTAJI KILA MAHALI NI KUGUMU.
 
Wewe kwenye usafiri wa vyombo vya moto wajinga wanavyo vingi sana,mfano mdogo ni superfeo..

Wanavyo lakini bado Sana kuwafikia Wachaga tukisema tutaje hapa utabaki mdomo wazi.

Wakinga wanajitahidi wakaze buti mpaka 2050 huko watakuwa wamewafikia Wachaga, maana Wachaga wa sasa kidogo wamepoa sio kama wa zamani
 
Hakuna kitu kama hicho.

Kujimwambafai tu. Hamna lolote. Nioneshe kiwanda kimoja tu cha mkinga kinachotengeneza bidhaa maarufu inayouzika hapa Africa Mashariki. Hakuna.

Nimekuelewa sana wakinga hawana MEGA BUSINESS kama viwanda vikubwa…kulinganisha hata na wachaga…wakinga ni vile wako wengi wanafanya biashara ya aina moja thats it…
 
Ni kweli, watu wa Kaskazini sio kwamba wanamaisha mazuri Sanaa Ila ni tabia Yao kujiona superior kuliko wengine,
Na hiyo inatokana na kuwazidi wengine Kwa baadhi ya vitu.

Ila mbona hawajioni Bora kuliko Wazungu 😄😄😄
Saivi maeneo mengi tupo sawa kiasi chake ila walicho tuzidi kasikazini kulinganisha maeneo mengine ni kitu kimoja usatalabu ulianza kuingia kwao na elimu ila hawana cha ziada
 
Saivi maeneo mengi tupo sawa kiasi chake ila walicho tuzidi kasikazini kulinganisha maeneo mengine ni kitu kimoja usatalabu ulianza kuingia kwao na elimu ila hawana cha ziada
Wakwanza ni wakwanza tu mkuu
 
Back
Top Bottom