Bro 🤣nitajie ukoo unaingia pale top 20 Wacha kukariri maisha biashara za uchuuzi ngumu kuendeleza kama ukoo zaidi mtaingizana katika Ajira Kwa vyeti feki na upendeleo muwe middle class income earners ila sio mtajiri kama waarabu na typically ya wakinga
Mkuu kuna mambo huyaelewi vizuri kuhusu hii nchi itakuwa😀😀
Unapozungumzia kuhusu biashara hii nchi Wachaga ndio the Top, wewe unaleta biashara za nguo za milioni 100😄😄 hao unaitwa matajiri.
Biashara za Wachaga ambazo unaziita za wachuuzi
1. Sekta ya anga
Wachaga ni moja ya kabila yenye kufanya biashara ya anga Kwa kumiliki baadhi ya makampuni ya Ndege, mfano Kampuni za Precious Airlines na zamani Fastjet alikuwepo Lawrence Masha akiongoza kaa share nyingi za Hisa.
Huenda hata Ndege tuu hujapanda ya kutoka DSM kwenda kwenu Mtwara😄😄 hivyo huwezi elewa hizi mambo
Sasa Kama kumiliki biashara za usafiri wa Ndege ni uchuuzi Sawa.
2. Sekta ya usafirishaji na mabasi.
Wachaga ndio wanaongoza Kwa kumiliki makampuni ya mabasi,
travel agency za tour Guide, na hapa ni ukiachana na Wahindi na waarabu.
3. Sekta za Utalii, Mahoteli na STAREHE.
Wachaga ndio wanaongoza Kwa kuwa na mahoteli, sehemu za starehe na hii wengi Hufanya Kwa sababu ya kazi ya utalii.
Wengi WA Wachaga wanamakampuni ya Utalii hivyo wamejenga hayo mahoteli Kwa ajili ya wageni wao.
Usishangae Moshi na Arusha kuwa kinara wa utalii ukadhani sehemu zingine hakuna mbuga😀😀
Hizi mambo huwezi elewa.
4. Wakala wa vipuri vya magari.
Wachaga kwenye sekta za UWAKALA WA vipuri ndio wanashika namba moja, Kama wewe unayajua magari sio ajabu ukikuta chata kwenye Vipuri vya magari vikiwa vimeandikwa 7General/Saba General ndiye aliyekuwa wakala mkubwa wa vipuri vya Magari hapa nchini.
5. Biashara ya Magari
Wachaga ndio wanaongoza Kwa biashara za kuuza magari.
Sio ajabu Wachaga ndio kabila pekee ambalo atu wake wanajua Aina za magari kuliko kabila lolote hapa nchini.
6. Biashara za Shule.
Wachaga ndio kabila la Kwanza Kwa umiliki WA shule binafsi hapa nchini wakifukuziwa na Wahaya.
7. Nenda sekta za Fedha na Benki hasa pale CRDB alafu useme Wachaga ni wachuuzi😄😄
8. Sekta ya madini
Tatizo lako unawajua Wachaga Wale wa Tabaka la chini na hii ni kutokana na unaishi mazingira ya namna hiyo.
Mimi sio mchagga Ila kwenye hii nchi utaanza na wahindi, waarabu, Wachaga alafu Sisi wengine tufuate.