Mkoa wa CHATO wazaa mgogoro wa kiutawala, kikabila na kielimu

Upuuzi mtupu,Chato peke yake haijitoshelezi kuwa mkoa ndio sababu inataka wilaya za mikoa mingine it can't stand alone.
Kama hitaji la mkoa kisheria linakidhi.
1.Makao makuu yawe nje ya Chato.
2.Jina la mkoa liwe nje ya Chato.
Ugomvu wote ni marehemu.
Angekuwa hai hata mkuu wa mkoa angekuwa tayari yupo Chato na hakuna wakubisha.
Jiji la Dodoma nani alijadili
 
Wewe unatakaje mkuu

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Butihama nayo iwe mkoa, wamege Serengeti, Musoma V, Bunda, Rorya na Tarime. Butihama ni ya mhasisi wa Taifa. Ala!
 
Hivi kwa nini kila siku ni kelele tu wengine wanasema Chato iwe mkoa na wengine wanasema Chato isiwe mkoa. Mimi nafikiri ni wakati sasa serikali ikaachana na hiyo hoja ya Chato kuwa mkoa mpaka kutakapokuwa na muafaka. Kwani kwa sasa mambo yanavyoenda ni kama vile hiyo hoja ya mkoa wa Chato imegeuka na kuwa ishu ya kikabila ambalo ni jambo la hatari sana kwenye umoja wa nchi yetu.

Kwa mtizamo wangu naona serikali kama inazo pesa za kuanzisha mkoa au mikoa mipya basi mikoa inayostahili kuanzishwa mikoa mipya ni Tabora na Morogoro kutokana na ukubwa wao na si vinginevyo.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato ana kesi ya kutoa rushwa na uvuvi haramu, halafu wasukuma sio wasomi, unachanganyaje wasomi na wachunga ng'ombe
Wahaya wangetoa Rais au waziri mkuu. Msukuma ndio msomi kuliko hao
 
Pole. Kigoma walisharidhia siku nyingi
Kakonko iko mkoa wa Kigoma, inahusishwa vipi na huo mgogoro wenu wa ukabila? Anzisheni Mkoa wa Chato bila kuimega Kakonko kwa sababu hakuna vikao vilivyoridhia mkoa wa Kigoma kumegwa.[emoji848]
 
Hawa wanatapatapa tu, undeni Chato yenu iwe mkoa bila kuzigusa mikoa mingine. Tafuta clip ya JPM (RIP) akiwa Tunduru alafu mheshimiwa diwani na wewe utuletee hiyo aliyotoa ahadi hapo Chato iwe mkoa. Kwanza Chato ina hadhi gani ya kuwa mkoa?
Kwani Lindi ina hadhi gani ya kuwa mkoa ?
 
Wewe ebu tulia tukujuze. Mkoa wa Rukwa wakati unaundwa mwaka 1974 walimega Mpanda toka Tabora na Sumbawanga toka Mbeya au ulikuwa hujazaliwa ?
 
Hakuna cha chato ni takatifu, wahaya hatutaki wamege mkoa wetu iwe mvua au jua lazima tulipiganie hili, kwanza serikali ilishatutenga zamani, kitakachofuata mbeleni huko ni sisi kuangalia namna ya kuwa nje ya Tz. Na tena wakijichanganya wakaingiza ukabila kwenye hili sakata moto utakaovuka Kagera mbeleni utaenda kulikosesha taifa amani, chonde chonde taasisi zetu za ulinzi na usalama liwekeeni taswira hili suala mkizubaa halitakuwa na mwisho mzuri kwa sasa na siku zijazo.
 
Nani aliye hai ? CUF au CHADEMA ? CCM itaendelea kuongoza nchi hii mpaka ichoke yenyewe maana hatuwezi kuongozwa na magaidi. Aidha, hakuna chama mbadala wa CCM.
Tuwaache wafu wa kijani waendelee kuwazika wafu wao.
 
Kagera ilishamegwa, unataka imegwa mara ngapi ndugu.
 
Tabora haina vigezo. Ni mapori tu eneo kubwa.
 
Wahangaza na wasubi si huwa mnawaita nyamahanga, leo wamekuwa watamu ? Tulieni sindano iwaingie, Chato lazima iwe mkoa
 
Imegwe mara ngapi

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…