Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,265
- 2,252
Nimeishalitahadharisha hili jambo, yaani wajichanganye hao viongozi waingize ukabila kwenye hili sakata, mwisho wake utaonekana tu.Hivi kwa nini kila siku ni kelele tu wengine wanasema Chato iwe mkoa na wengine wanasema Chato isiwe mkoa. Mimi nafikiri ni wakati sasa serikali ikaachana na hiyo hoja ya Chato kuwa mkoa mpaka kutakapokuwa na muafaka. Kwani kwa sasa mambo yanavyoenda ni kama vile hiyo hoja ya mkoa wa Chato imegeuka na kuwa ishu ya kikabila ambalo ni jambo la hatari sana kwenye umoja wa nchi yetu.
Kwa mtizamo wangu naona serikali kama inazo pesa za kuanzisha mkoa au mikoa mipya basi mikoa inayostahili kuanzishwa mikoa mipya ni Tabora na Morogoro kutokana na ukubwa wao na si vinginevyo.