Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Hae
Yan huwez kututenga na watu wa njombe tunaoongea rugha moja au watu wa usangu tunao ongea rugha moja huo ni ukichaa
Haelewi kwamba Chief mkwawa wa uhehe alipata kuoa binti wa chief Merere wa Usangu.
 
Sijui Kuhusu hayo mengine ila mimi nahisi sababu za kijamii na kiutamaduni ndio hasa zinazounganisha mikoa hii ya nyanda za juu kusini. Kwa ufahamu wangu nafikiri wahehe wanafanana zaidi na watu wa Njombe na Mbeya kuliko wwnavyofanana na watu wa Dodoma na Singida. Kwa hiyo mtoa mada unataka kusema idadi ya wagogo waliopo Iringa inazidi idadi ya wabena na wakinga?
Sababu nilizokutajia hapo Juu ndio uhalisia,wangekuwa wanaingiliana kama unavyodai wewe hata Mkoa usingegawanywa Kwa kufuata makabila..

Pili nimekwambia hata Sasa Njombe Ina Maingiliano ya Kijamii na Kiuchumi zaidi na Mbeya na Songea kuliko Iringa,wahehe ndugu zao Wagogo.
 
Hae
Haelewi kwamba Chief mkwawa wa uhehe alipata kuoa binti wa chief Merere wa Usangu.
Mzee Usangu Iko Mbeya Wala haiko Iringa,kuoleana hata Sasa watu wanaoleana ila ukweli ni kwamba Watu wa Iringa ndugu zao Wagogo.
 
unatakiwa kuwa na heshima kidogo. kwahiyo unataka kuiunganisha iringa na singida na dodoma? unaelewa maana ya nyanda za juu kusini? iringa ni nyanda za juu (milimani), dodoma kuna nyanda? singida kuna nyanda? wamekuchosha nini?
Kama issue ni Milima basi Morogoro au Kilimanjaro au Arusha zote zingekuwa Nyanda za Juu..

Nakwambia Muingiliano wa Kijamii ni mkubwa Dom kuliko Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini..

Watu wa Iringa vipi mnakataa ndugu zenu? Nendeni Dom huko
 
Mzee Usangu Iko Mbeya Wala haiko Iringa,kuoleana hata Sasa watu wanaoleana ila ukweli ni kwamba Watu wa Iringa ndugu zao Wagogo.
Mkuu yaani ukifika usangu uongee kihehe wana kisikia fresh kwa kuwa rugha yao ni kama kibena tuu. Ko sie huku ni wamoja ila hao kina Mwigulu hatuwajui. Kwanza wanatisha
 
Wabena kamwene, wahehe kamwene. Wabena Ndauli, wahehe ndauli, wabena weuli wahehe weuli. Wakinga nao ni salamu tuu ila maneno yote kama wabena tuu. Harafu wakinga tena wanakuja kufanana rugha na mnyakyusa hadi raha. Acheni kutupeleka dodoma sie hatujuani na wanyiramba
Kama mbaelewana Kwa hiyo wabena Huwa wanasalimiana kamwene au mapembero si ndio?
 
Mikoa 26 ya Tanzania Bara imegawanywa kwenye Kanda 7 za Kiutawala.

Mkoa wa Iringa Kwa Sasa uko Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Ingefaa Kwa Serikali kuiondoa Iringa Nyanda za Juu Kusini na kuihamishia Kanda ya Kati Kwa sababu zifuatazo

1.Sababu za Kijiografia.

Mkoa wa Iringa u ko jirani na Dodoma Makao Makuu ya Nchi na Kanda ya Kati kuliko Mbeya(Makao Makuu ya Nyanda za Juu Kusini).
Kutoka Iringa Hadi Dodoma ni km 260 vs Iringa Mbeya km 350.As we speak Iringa na Dodoma Ina Muingiliano mkubwa wa Watu via usafiri kuliko Iringa na Mbeya,so ni sahihi Kwa Iringa kuwa included Central Zone.

2.Sababu za Kijamii(Muingiliano wa Kikabila)

Kabila la Wagogo ambao ndio kabila kuu la Mkoa wa Dodoma pia linapatikana Kwa Baadhi ya maeneo ya Iringa hasa Wilaya ya Iringa hivyo Muingiliano wa Kijamii na Kitamaduni ni mkubwa baina ya Iringa na Dodoma kuliko Iringa na Mbeya..Aidha Kabila la Wahehe pia wapo Dodoma..

3.Sababu za Kimazingira.

Iringa Ina Haki ya hewa ya semi -Arid (Nusu jangwa) sawa sawa kabisa na hali ya Dodoma au Kanda ya Kati kiukumla.
Ukitoa Wilaya ya Mufindi na Baadhi ya maeneo ya Kilolo ,Iringa yote ni Semi Arid..

4.Sababu ya Kiuchumi/Biashara na Kijamii.

Mkoa wa Iringa unategemea Huduma zake nyingi kutoka Dodoma na Dar lakini sio Mbeya kutokana na kuwa jirani na Dodoma..

Sasa Kwa sababu hizo ni Wazi Iringa inafaa iwe Kanda ya Kati badala ya kuwa Nyanda za Juu.

Kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni Iringa Pekee ambako unaweza Kuta nyumba za udongo na nyasi ambazo zinapatikana Kwa wingi Dodoma,Singida na maeneo ya Kanda ya Ziwa na Pwani huko..View attachment 2657397
Kwa hiyo shida ya Iringa kutoendelea ni kuunganishwa na mikoa ya nyanda za juu kusini? Au siyo? Basi tuipeleke kati. Tuunganishw na Morogoro, Manyara, Singida, Iringa na Dodoma, ili kuleta maendeleo. Au siyo?
 
Mkuu yaani ukifika usangu uongee kihehe wana kisikia fresh kwa kuwa rugha yao ni kama kibena tuu. Ko sie huku ni wamoja ila hao kina Mwigulu hatuwajui. Kwanza wanatisha
Acha habari zako,ndugu zenu ni Wagogo ambao wapo Dom na Iringa,Wahehe wapi Dom na Iringa pia..

Hao wa sijui tunasikilizana na blaa blaa kama hizo sio,nimekutajia sababu Zenye mashiko kabisa hapo Kwa nini muwe Kanda ya Kati na sio Nyanda za Juu..

Nakuuliza swali jingine,ukifika stand ya Iringa Costa nyingi zinaenda wapi Kati ya Dom au Mikoa mingine?
 
Kwa hiyo shida ya Iringa kutoendelea ni kuunganishwa na mikoa ya nyanda za juu kusini? Au siyo? Basi tuipeleke kati. Tuunganishw na Morogoro, Manyara, Singida, Iringa na Dodoma, ili kuleta maendeleo. Au siyo?
Ipelekeni huko huko mnakotaka kama hamtaki ndugu zenu wa Dodoma..

Njombe imeamua kuwa na Mbeya sio Iringa.

Umewahi kuona nyumba za udongo au tembe Njombe au Mbeya au Rukwa ama Songwe? Ila Iringa na Dom zimejaa.
 
Back
Top Bottom