Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Hakuna cha kujadili, kama unataka kusikilizwa wewe tu tutajadili nini unadhani. Hutaki kusikia wengine wanasema nini, umeshikilia kile unachoamini wewe.
Post vizuri attachment Yako nije nikupe shule
 
Kama issue ni Milima basi Morogoro au Kilimanjaro au Arusha zote zingekuwa Nyanda za Juu..

Nakwambia Muingiliano wa Kijamii ni mkubwa Dom kuliko Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini..

Watu wa Iringa vipi mnakataa ndugu zenu? Nendeni Dom huko
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mleta mada huna hoja. Bora muda ulioutumia kuandika thread ungeutumia kuuza ubuyu, pengine ungeinigiza faida ya Tshs 200/=.
 
Ila ukiangalia kiundani zaidi kwa jiografia ya nyanda za juu kusini mkoa ambao upo katikati ni njombe kwa nini nasema hivo tunachukulia junction ya makambako ukitoka makambako hadi iringa ni km 164 ,makambako mbeya 172km ,makambako had songwe 274 ,makambako ruvuma km 292 na distance ya makambako tunduru ni sawa na makambako sumbawanga na mkoa wa iringa una mwingiliano mkubwa zaidi na njombe na si mbeya na ndo maana hata soko la Kanda la mazao nyanda za juu kusini wanajenga makambako ,matank ya ku supply mafuta yanajengwa makambako, NFRA nyanda za juu kusini ipo makambako ingawa now wameongeza matawi na ukifuata histori hata wazee walishaliona Hilo ndo maana iringa ndo ilikuwa makao makuu ya nyanda za juu kusini yakaja kuhamishwa na kupelekwa mbeya ambapo kiuhalisia sio katikati hebu tafakari mtu WA mkoa WA ruvuma ,iringa mbeya ni mbali
FB_IMG_16767644099419941.jpg
 
Ila ukiangalia kiundani zaidi kwa jiografia ya nyanda za juu kusini mkoa ambao upo katikati ni njombe kwa nini nasema hivo tunachukulia junction ya makambako ukitoka makambako hadi iringa ni km 164 ,makambako mbeya 172km ,makambako had songwe 274 ,makambako ruvuma km 292 na distance ya makambako tunduru ni sawa na makambako sumbawanga na mkoa wa iringa una mwingiliano mkubwa zaidi na njombe na si mbeya na ndo maana hata soko la Kanda la mazao nyanda za juu kusini wanajenga makambako ,matank ya ku supply mafuta yanajengwa makambako, NFRA nyanda za juu kusini ipo makambako ingawa now wameongeza matawi na ukifuata histori hata wazee walishaliona Hilo ndo maana iringa ndo ilikuwa makao makuu ya nyanda za juu kusini yakaja kuhamishwa na kupelekwa mbeya ambapo kiuhalisia sio katikati
Weka ramani acha porojo Mkuu

Sasa Njombe kwamba Iko Katikati ihamishiwe Dom au? Katikati Kwa muktadha gani? Kwa kuwa tayari Makao Makuu ya Kanda yanajulikana hiyo sio kesi tena..

Mambo ya Maghala ya nrfa yapo kuanzia Katavi, Sumbawanga,Songwe, Makambako,Ruvuma ndio kabisaa..
Soko la Kanda ndio soko gani ikiwa Tunduma na Momba DC wameshajenga masoko makubwa ya kimkakati ya mazao ya nafaka?

Njombe Ina Muingiliano mkubwa na Iringa ipi? Wilaya ya Makete,Ludewa na Wanging'ombe ni kama za Mbeya so no way Iringa ndugu zake Wagogo..

Hoja yangu Iko pale pale,Iringa ihamishiwe Kanda ya Kati,Dom pale wanajenga Logistics kubwa hakuna mtu wa Iringa atafuta bidhaa Mbeya au Dar Wakati anaweza pata hapo Dom Kwa bei rahisi zilizoletwa na Sgr ikizingatiwa Iringa Dom ni jirani.
 
Weka ramani acha porojo Mkuu

Sasa Njombe kwamba Iko Katikati ihamishiwe Dom au? Katikati Kwa muktadha gani? Kwa kuwa tayari Makao Makuu ya Kanda yanajulikana hiyo sio kesi tena..

Mambo ya Maghala ya nrfa yapo kuanzia Katavi, Sumbawanga,Songwe, Makambako,Ruvuma ndio kabisaa..
Soko la Kanda ndio soko gani ikiwa Tunduma na Mimba wameshajenga masoko makubwa ya kimkakati ya mazao ya nafaka?

Jaribu kufuatilia vizuri uundaji WA Kanda na kwanini walianzisha miji ya mkakati kwa nyanda za juu kusini kijiografia mbeya sio katikati huo ndo uhalisia imagine wakajenga soko la mazao mkoa WA njombe , wakaweka logistic hub ana hajagani mtu WA iringa kwenda dodoma na hii mada ilishajadiliwa siku nyingi Sana
 
Hata Rukwaa enyewe isiwepo huku juu kusini, iwepo huko magharibi.
Rukwa ni Nyanda za Juu Kusini pure maana inafanana mazingira,utamaduni na aina za shughuli za kiuchumi na Nyanda za Juu Kusini.

Mfano upande wa Magharibi ni Mikoa ya joto kuanzia Tabora,Kigoma na Katavi wakati Rukwa ni Mkoa wa Baridi sababu ya Milima.

Makao Makuu ya Kanda ya Magharibi Yako Kigoma,huo umbali wa km 600 nani anataka wakati Kwenda Mbeya ni km 330 tuu..

Mwisho ukiacha Arusha-moshi,Mbeya-Tunduma na Morogoro -Dar ,hakuna Mkoa mwingine una route nyingi za Mabasi kushinda Mbeya -Sumbawanga tena panda zote Huku Juu ufipani na kule chini Bonde la Ziwa Rukwa..
 
Jaribu kufuatilia vizuri uundaji WA Kanda na kwanini walianzisha miji ya mkakati kwa nyanda za juu kusini kijiografia mbeya sio katikati huo ndo uhalisia imagine wakajenga soko la mazao mkoa WA njombe , wakaweka logistic hub ana hajagani mtu WA iringa kwenda dodoma na hii mada ilishajadiliwa siku nyingi Sana
Mbeya sio Katikati na hawafuati Katikati ila Waliamua Mji mkubwa na ulioko sehemu ya kimkakati ndio kigezo..

Kigoma imekuwa Makao Makuu ya Kanda ya Western sio ishu ya Katikati ila Mkoa wa kimkakati ambao unafikiwa na Kutegemea na Mikoa mingine kirahisi..

Mbeya inategewa na Mikoa hii mingine sana kuliko Iringa,Iringa ilishajitenga kule and so Kwa kuwa Dom ndio jirani kwake na influence yake huko ndiko kunaifaa ,sijajua Kwa nini Wahehe wanakataa kuwa sehemu ya Central Zone wakati makabila,giografia na hali ya hewa vinaingiliana sana.
 
Weka ramani acha porojo Mkuu

Sasa Njombe kwamba Iko Katikati ihamishiwe Dom au? Katikati Kwa muktadha gani? Kwa kuwa tayari Makao Makuu ya Kanda yanajulikana hiyo sio kesi tena..

Mambo ya Maghala ya nrfa yapo kuanzia Katavi, Sumbawanga,Songwe, Makambako,Ruvuma ndio kabisaa..
Soko la Kanda ndio soko gani ikiwa Tunduma na Mimba wameshajenga masoko makubwa ya kimkakati ya mazao ya nafaka?

Njombe Ina Muingiliano mkubwa na Iringa ipi? Wilaya ya Makete,Ludewa na Wanging'ombe ni kama za Mbeya so no way Iringa ndugu zake Wagogo..

Hoja yangu Iko pale pale,Iringa ihamishiwe Kanda ya Kati,Dom pale wanajenga Logistics kubwa hakuna mtu wa Iringa atafuta bidhaa Mbeya au Dar Wakati anaweza pata hapo Dom Kwa bei rahisi zilizoletwa na Sgr ikizingatiwa Iringa Dom ni jirani.
Hata gari za njombe iringa zipo za kutosha
 
Mbeya sio Katikati na hawafuati Katikati ila Waliamua Mji mkubwa na ulioko sehemu ya kimkakati ndio kigezo..

Kigoma imekuwa Makao Makuu ya Kanda ya Western sio ishu ya Katikati ila Mkoa wa kimkakati ambao unafikiwa na Kutegemea na Mikoa mingine kirahisi..

Mbeya inategewa na Mikoa hii mingine sana kuliko Iringa,Iringa ilishajitenga kule and so Kwa kuwa Dom ndio jirani kwake na influence yake huko ndiko kunaifaa ,sijajua Kwa nini Wahehe wanakataa kuwa sehemu ya Central Zone wakati makabila,giografia na hali ya hewa vinaingiliana sana.
Mkoa wa iringa una wilaya tatu wilaya inayofanana na Dom ni iringa dc kilolo eneo lao kubwa wanalima miti ,chai nk hivo hivo na mufindi
 
Ukiacha Mufindi,hizo zingine kama Kilolo in upande wa mvua na upande wa ukame eg Ilula Hadi mpakani na Moro ni purely Dom climate type..

Hata Dom Wilaya ya Mpwapwa sio kame ,watu wengi hawajui hii,kule kunapata mvua ya Wastani..

Lakini Mikoa mingine ya Nyanda za Juu ni mvua kwenda mbele ndio maana huwezi Kuta nyumba za tembe hata Moja au za udongo kama zilivyo Iringa na Dom.
 
Back
Top Bottom