Sensa ya watu na makazi 2022, Mkoa wa Kilimanjaro ulikua na wakazi 1.8M, taarifa ya Azam inasema asilimia 7.3 ya watu wa Kilimanjaro ni wazee na inaongoza Tanzania kwa Asilimia (sio idadi ya wazee) Asilimia 7.3 ya 1.8M ndo hio wazee 130K.
So kilimanjaro haiongozi kwa idadi ya wazee bali ratio ya wazee na vijana ni kubwa kule kutokana na vijana wengi kutoka kutafuta maisha kwengine.
Baada ya Kilimanjaro ni Mtwara, same Story na sitashangaa in future Kigoma pia ikafuatia kutokana Na waha watoto wanavyokimbilia mijini.
View attachment 3084820
Ukiangalia data zetu hapo
-Dodoma ina asilimia 4.8 ya wazee percentage wise ni ndogo kuliko Kilimanjaro na mtwara ila idadi ni kubwa sababu asilimia 4.8 ya watu zaidi ya milioni 3 inakuja zaidi ya wazee 140,000 ambayo inaizidi kilimanjaro
-pia Tanga ukiangalia ni hivyo hivyo Asilimia 5.1 ya watu 2.6 ni humo humo roughly 130K sawa na Kilimanjaro na zaidi ya Mtwara ila haijatajwa sababu Percentage wise ni ndogo
So bottom line wakuu hizo ni data za Asilimia yaani Ratio ya wazee ukicompare na makundi mengine ya Umri na Sio data zinazoonesha idadi kubwa ya wazee.
Nimeambatanisha na Sensa ya watu Na makazi ikitoa huo mchanganuo.