Nijuavyo mzee wa kichaga mwenye watoto 6 kuna uwezekano mmoja yupo tanroads, mwingine ni Dokta mloganzila na mwingine ni businessman na waliobaki ni walevi wa kutupwa, mzee kajengewa hekalu lina mbuzi, kuku, mashamba ya migomba n.k.
Mzee ana bima kubwa, ana bank account akikohoa tu KCMC maana hata nyumbani kuna Ndinga ya maana full tank na kiyoyozi, hivyo hakuna sababu ya kufa mapema.
Sasa njoo huku kwetu umanyemani, uziguani, ugogoni, undengelekoni mzee ana wake 3 na watoto kumi na tisa katika hao watatu ni wapiga lamri, wawili wagema mnazi, 6 ni walevi wa kufa mtu wanaotembelea ugali wa dochivele yaani ugali wa nyumbani, watatu wauza madafu, wawili fundi baiskeli, wawili ni bodaboda, wailobaki ni vibaka na wazee hawa wanaamini anayetoa riziki ni Mungu na wote waliishia la pili mwezi wa tatu lakini huko uchagani ukatae shule utakula mabuti ya UTOSI lakini huku kwetu hata usipoenda shule hakuna anaekuuliza.
Mzee hana bima kukicha anapiga uji au togwa, mchana ugali Ngogwe mchanganyiko na bahundred yaani bamia, kula nyama hadi tajiri jirani afe halafu mnataka aishi miaka 90? Unisamehe tu maana ndo uhalisia