Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa pekee ambao Wabunge wake Elimu ya chini Wana shahada/degree. Bila Degree Sahau kuhusu Ubunge huko Kilimanjaro

Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa pekee ambao Wabunge wake Elimu ya chini Wana shahada/degree. Bila Degree Sahau kuhusu Ubunge huko Kilimanjaro

Sasa kama watu wanachagua vishoia ndio wataweza kudhibiti madaraka ya Rais?
Ndio msingi wa Gwajima, kuamua kupambana kwa niaba ya Tanzania.

Hatuwezi kuwa na katiba ambayo watu wa hovyo wakibahatika kuishika hiyo nafasi kwa kudra za mwenyezi mungu watubuluze.

Samia katupa somo, hii katiba kwa upande wa mamlaka ya raisi, aitufai.

Huyo mama ni wa hovyo, acha tu.

Cha msingi ni kukubali, hasara; na kuangalia mbele.
 
Kiwango ni hicho hicho nimefanya kazi ya tasaf hiyo Kanda ya kaskazini hata sio vizuri kusimulia
Binafsi niliona Kanda ya ziwa familia nyingi zinajimudu kuliko huko milimani

Takwimu za serikali zinapingana na wewe pakubwa.

Hata hivyo maskini haimaanishi hawapo.

Ngoja nimuite ChoiceVariable atuletee takwimu ujionee.
 
Alafu Serikali ifanye uchunguzi ikiwa wazazi wameelekeza watoto wao kuwasajili Shule za Private kisa tu ni za English Medium basi na yenyewe serikali ibadili angalau nusu ya shule zilioko Kilimanjaro ziwe za English medium kisha ione uelekeo wa Taifa kwa ujumla kuptia kitalu funzo hicho.
 
Ndio msingi wa Gwajima, kuamua kupambana kwa niaba ya Tanzania.

Hatuwezi kuwa na katiba ambayo watu wa hovyo wakibahatika kuishika hiyo nafasi kwa kudra za mwenyezi mungu watubuluze.

Samia katupa somo, hii katiba kwa upande wa mamlaka ya raisi, aitufai.

Huyo mama ni wa hovyo, acha tu.

Cha msingi ni kukubali, hasara; na kuangalia mbele.

Huyo Gwajima angekuwa mkweli asingekuwa Mbunge.
Kura za maoni 2020 hakuwa wa Kwanza, akateuliwa kidhuluma dhulma. Kama angekuwa muadilifu angekataa.

Alafu huyo JPM kama alikuwa anamhitaji angemteua kwenye zile nafasi 10
 
Habari za Asubuhi!

Kule Kwetu Kilimanjaro, Moja ya Mambo muhimu wananchi wanayazingatia kumpa Mtu Ubunge ni Elimu yake.

Unajua Kilimanjaro mtu anaheshimiwa kwa mambo makuu yafuatayo;
1. Pesa
2. Elimu
3. Familia.

Wananchi wa Kilimanjaro hata wale wajinga kabisa ambao hawakusoma hata darasa Moja lazima waulizie elimu ya Kiongozi wanayeenda kumchagua katika nafasi ya Ubunge.

Kwa Wapare na Wachaga ni aibu Kuongozwa na Mtu mjinga ambaye hajaenda shule.
Hata uwe na akili vipi, kule kwetu kama hukusoma bado utawekwa kundi la Wajinga.
"Tetongie shule huo!"
"Madarasa ni madori!"

Hatuwezi kusomesha watoto wetu kwa gharama kubwa alafu wasikie Mbunge wao hakusoma.

Hiyo tumewaachia jamii zingine kwa kweli.

Kuongozwa na vishoia hapana!
Kuongozwa na vibushuti hapana!

Kwanza hata hiyo degree kwa sasa kule Kilimanjaro inaanza kuwekewa Mashaka. Kila familia inakijana mwenye degree.
Ndio maana Wabunge wa Kilimanjaro siku hizi nusu Yao wanazaidi ya elimu ya degree. Wapo wenye masters na PhD.

Ndio maana huwezi sikia mara kwa mara wabunge wa Kilimanjaro awe CCM au CHADEMA wakitia aibu za rejareja.

Kwanza Mtu wa darasa la Saba au kidato cha nne kule Moshi anaanzaje kufikiria kwenda Bungeni ati kuwa Mbunge?
Amwakilishe Nani hasa?

Kilimanjaro hata vijana ambao hawajasoma, walevi, wavuta bangi hawawezi kukubali kuwakilishwa na mtu ambaye hajasoma. Na huo kwetu ni utamaduni.
Lazima shule iwepo ya kutosha.
Lazima pesa angalau iwepo.
Lazima familia uwe nayo. Sio tupeleke wahuni bungeni.

Wewe miaka 40 hujaolewa wala kuoa unataka uchaguliwe kuwa Mbunge, sio kwa Kilimanjaro. Tafuta sehemu zingine huko ukagombee.

Haya!
Gazeti lako linatufundsha Nini?..?
 
Alafu Serikali ifanye uchunguzi ikiwa wazazi wameelekeza watoto wao kuwasajili Shule za Private kisa tu ni za English Medium basi na yenyewe serikali ibadili angalau nusu ya shule zilioko Kilimanjaro ziwe za English medium kisha ione uelekeo wa Taifa kwa ujumla kuptia kitalu funzo hicho.

Sahihi
 
Kusema kweli kama uliwahi kuishi mkoa wa Kilimanjaro hata kama wewe sio mchaga au mpare na umebahatika pia kuzunguka mikoa kadhaa au yote ya Tanzania na Mungu amekuondolea ile roho ya husuda na khiyana utagundua kuwa mkoa wa Kilimanjaro upo level nyingine kubwa kimaendeleo kuliko mikoa yote.....

Unachafuliwa na kasoro ya ulevi tu uliokithiri kwenye baadhi ya maeneo.....
 
Ni kweli Kabisa.
Japokuwa baadhi ya watu hawapendi kusikia mambo haya.

Kilimanjaro Wana standards zao kwenye mambo muhimu iwe ni siasa, ndoa/familia, Mali na KAZI. Hayo maeneo kwao ni nyeti na Wana standards Kali
 
Kwa hiyo Kilimanjaro akina Msukuma hawezi wakapata hata udiwani?.
 
Back
Top Bottom