Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa pekee ambao Wabunge wake Elimu ya chini Wana shahada/degree. Bila Degree Sahau kuhusu Ubunge huko Kilimanjaro

Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa pekee ambao Wabunge wake Elimu ya chini Wana shahada/degree. Bila Degree Sahau kuhusu Ubunge huko Kilimanjaro

Habari za Asubuhi!

Kule Kwetu Kilimanjaro, Moja ya Mambo muhimu wananchi wanayazingatia kumpa Mtu Ubunge ni Elimu yake.

Unajua Kilimanjaro mtu anaheshimiwa kwa mambo makuu yafuatayo;
1. Pesa
2. Elimu
3. Familia.

Wananchi wa Kilimanjaro hata wale wajinga kabisa ambao hawakusoma hata darasa Moja lazima waulizie elimu ya Kiongozi wanayeenda kumchagua katika nafasi ya Ubunge.

Kwa Wapare na Wachaga ni aibu Kuongozwa na Mtu mjinga ambaye hajaenda shule.
Hata uwe na akili vipi, kule kwetu kama hukusoma bado utawekwa kundi la Wajinga.
"Tetongie shule huo!"
"Madarasa ni madori!"

Hatuwezi kusomesha watoto wetu kwa gharama kubwa alafu wasikie Mbunge wao hakusoma.

Hiyo tumewaachia jamii zingine kwa kweli.

Kuongozwa na vishoia hapana!
Kuongozwa na vibushuti hapana!

Kwanza hata hiyo degree kwa sasa kule Kilimanjaro inaanza kuwekewa Mashaka. Kila familia inakijana mwenye degree.
Ndio maana Wabunge wa Kilimanjaro siku hizi nusu Yao wanazaidi ya elimu ya degree. Wapo wenye masters na PhD.

Ndio maana huwezi sikia mara kwa mara wabunge wa Kilimanjaro awe CCM au CHADEMA wakitia aibu za rejareja.

Kwanza Mtu wa darasa la Saba au kidato cha nne kule Moshi anaanzaje kufikiria kwenda Bungeni ati kuwa Mbunge?
Amwakilishe Nani hasa?

Kilimanjaro hata vijana ambao hawajasoma, walevi, wavuta bangi hawawezi kukubali kuwakilishwa na mtu ambaye hajasoma. Na huo kwetu ni utamaduni.
Lazima shule iwepo ya kutosha.
Lazima pesa angalau iwepo.
Lazima familia uwe nayo. Sio tupeleke wahuni bungeni.

Wewe miaka 40 hujaolewa wala kuoa unataka uchaguliwe kuwa Mbunge, sio kwa Kilimanjaro. Tafuta sehemu zingine huko ukagombee.

Haya!
Nchi yote ingekuwa hivi bungeni kusingekuwa waimba pambio za kusifu na kuabudu serekali ingekuwa ni fire kwa kwenda mbele muhimili wa serekali wangekuwa wanajiuliza mara mbilimbili kupeleka mambo yao ya hovyo.
 
Kweli sn alafu ujue mchaga wavidudu nikama msukuma/mzaramo alofika fomusikis🤣.

Wasukuma na morogoro sijui mapogolo yale ndiyo wanaongoza kutupelekea mazwazwa bungeni?kuanzia kibajaji,bbtale,msukuma nawenzie.
Nchi inaamshwa na kina hayati mrema, Mbowe,mdee,Lema,ndesamburo etc.

Kigoma kwambaaali sema shidayao wasaliti saana na wananunulika kirahosi kama aisikrimu za baresa sijataja mfano wa zito na tumbili hiyo ntataja nikiulizwa
 
Mnasemaga Wahaya tunapenda sifa, wachaga mnazidi " Sisi kule kwetu Bukoba/Kagera elimu kwa mbunge hatuulizi tena, ni sawasawa ni kuulizia oxygen kwenye uhai, ni Pie, kule kwetu, uwe na Elimu, Uwe una exposure - umeenda US vile etc, uwe unabonga kiingereza zaidi ya Kinyambo au Kihaya, uwe una sifa za kuwa waziri - yaani ukipata ubunge uwe na 60% ya kuwa waziri".Hatulingi sisi lkn hatuhongelei elimu tena, sababu elimu tunayo tayari, tunatafuya sifa zingine"
Hahahaha
 
Habari za Asubuhi!

Kule Kwetu Kilimanjaro, Moja ya Mambo muhimu wananchi wanayazingatia kumpa Mtu Ubunge ni Elimu yake.

Unajua Kilimanjaro mtu anaheshimiwa kwa mambo makuu yafuatayo;
1. Pesa
2. Elimu
3. Familia.

Wananchi wa Kilimanjaro hata wale wajinga kabisa ambao hawakusoma hata darasa Moja lazima waulizie elimu ya Kiongozi wanayeenda kumchagua katika nafasi ya Ubunge.

Kwa Wapare na Wachaga ni aibu Kuongozwa na Mtu mjinga ambaye hajaenda shule.
Hata uwe na akili vipi, kule kwetu kama hukusoma bado utawekwa kundi la Wajinga.
"Tetongie shule huo!"
"Madarasa ni madori!"

Hatuwezi kusomesha watoto wetu kwa gharama kubwa alafu wasikie Mbunge wao hakusoma.

Hiyo tumewaachia jamii zingine kwa kweli.

Kuongozwa na vishoia hapana!
Kuongozwa na vibushuti hapana!

Kwanza hata hiyo degree kwa sasa kule Kilimanjaro inaanza kuwekewa Mashaka. Kila familia inakijana mwenye degree.
Ndio maana Wabunge wa Kilimanjaro siku hizi nusu Yao wanazaidi ya elimu ya degree. Wapo wenye masters na PhD.

Ndio maana huwezi sikia mara kwa mara wabunge wa Kilimanjaro awe CCM au CHADEMA wakitia aibu za rejareja.

Kwanza Mtu wa darasa la Saba au kidato cha nne kule Moshi anaanzaje kufikiria kwenda Bungeni ati kuwa Mbunge?
Amwakilishe Nani hasa?

Kilimanjaro hata vijana ambao hawajasoma, walevi, wavuta bangi hawawezi kukubali kuwakilishwa na mtu ambaye hajasoma. Na huo kwetu ni utamaduni.
Lazima shule iwepo ya kutosha.
Lazima pesa angalau iwepo.
Lazima familia uwe nayo. Sio tupeleke wahuni bungeni.

Wewe miaka 40 hujaolewa wala kuoa unataka uchaguliwe kuwa Mbunge, sio kwa Kilimanjaro. Tafuta sehemu zingine huko ukagombee.

Haya!
Hivi Mrema alikuwa Mbunge wa wapi? Yule Mrema wa TLP
Mwamba hata kabla ya degree yake amewahi kuwa Mbunge wa Hai

Acha Generalization
 
Hili jambo mara kadhaa huwa nawambia watu wangu wa mkoa wa Rukwa,lakini hawasikii,Mbunge kama yule wa Sumbawanga mjini unampeleka mbungeni kufanya nini ? Kama sio kichekesho.

Kuna madiwani wako mkoa wa Rukwa hata kusoma na kuandika ni kipengele 😀
 
Hali hii imeanza lini au ndio sababu Lema alichagua Arusha? Vipi kuhusu aliyekuwa mbunge wa Hai Mh. Mbowe? Kama ni awamu ya tano je, walichaguliwa au walipitishwa? Je, waliopo wana uwezo wa kufikiri nje ya boksi kama Kishimba?
 
Wabunge wasio na elimu kazi yao ni kwenda kuponda elimu bungeni. Waone watu kama msukuma na kishimba michango yao yote ni kuzodoa wasomi. Kwa maoni yao kipimo cha elimu ni pesa.
 
Kusema kweli kama uliwahi kuishi mkoa wa Kilimanjaro hata kama wewe sio mchaga au mpare na umebahatika pia kuzunguka mikoa kadhaa au yote ya Tanzania na Mungu amekuondolea ile roho ya husuda na khiyana utagundua kuwa mkoa wa Kilimanjaro upo level nyingine kubwa kimaendeleo kuliko mikoa yote.....

Unachafuliwa na kasoro ya ulevi tu uliokithiri kwenye baadhi ya maeneo.....
Maendeleo Kwenye Aspects zipi ndugu kikulacho
 
1.Hivi naomba kujua jimbo la vunjo lipo wilaya gani.
2. Wilaya ya mwanga ina majimbo mangapi ya uchaguzi

3.Mrema alikuwa mbunge wa vunjo au moshi vijijini.
4. Basil mramba alikuwa mbunge wa jimbo gani
5.Nani alikuwa mbunge wa same mashariki kabla ya kilango
 
Maendeleo Kwenye Aspects zipi ndugu kikulacho
Mimi binafsi nayatafsiri maendeleo kwenye aspect kama huduma bora kijamii kama vile afya,elimu, maji na umeme......makazi bora, miundombinu ya bara bara inayounganisha wilaya zote za mkoa mzima iwe za Lami au za kokoto lakini zinapitika kipindi chote cha mwaka....
 
Ukitaka upate Fair Comparison kati ya Kilimanjaro na maeneo mengine hebu linganisha kwenye village level......achana na pale manispaa...
 
Back
Top Bottom