Mkoa wa Mara ni moja ya mikoa ya iliyo nyuma kimaendeleo katika nchi hii

Mkoa wa Mara ni moja ya mikoa ya iliyo nyuma kimaendeleo katika nchi hii

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
491
Reaction score
1,907
Nimefika wilaya ya Tarime daah ni hovyo kwelikweli, stand ni mbaya. Hakuna daladala zaidi ya probox mnawekwa hata 10 hadi kwenye buti huko.

Sehemu kubwa ya wilaya na mkoa ni pori tu, ikifika saa mbili watu wamelala mji hauna watu.

Maji ni tatizo japo wamepakana na ziwa victoria.

Watu wa huko wamekaa kishari tu na hawacheki ovyo ovyo.

Yaani kutoka makutano kwenda bunda ni pori tu hata ukitekwa hupati msaada. Nimetembea baadhi ya mikoa lakini Mara hapana kupo tofauti!
 
000382ca-fb3c-41d1-9652-77abf155f7cb.jpg
 
Inawezekana umehadithiwa ndugu, kutoka makutano Hadi bunda ni pori!

Ukitoka makutano Kuna vijiji na mitaa kadhaa yenye zahanati, vituo vya afya na hata vituo vya polisi,

Mfano makutano- nyakanga- irimba- kiabakari- nyamikoma- mwibagi- bitaragulu- manyamanya unaingia bunda mjini hizi zote nimekutajia senta za barabarani Tena zilizochangamka pita kiabakari hapo mjini kabisa bro
 
Fanya kilichokupeleka. Inaonekana hujatembea mikoa mingi hapa Tz. Mkoa wa Mara vijiji vyake karibia vyote isipokuwa Rorya ni kama Mjini.

Barabara uhakika All seasons, Maji laini, usafiri uhakika. Usiku ni wa majambazi. Mwisho siyo kwa umuhimu nimefanya kazi Mara 9 yrs siwezi linganisha na Mikoa mingine 15 niliyopiga kazi. Msosi frssh bei chee. Matunda ya kila aina.
 
Hujatembea kama hivyo ndio vigezo unavyotumia kupika umaskini wa watu. Hivi wewe ulishafika kigoma uone mapori? Usha fika katavi?

Usha chochora ukafika lindi na mtwara? Hebu zunguka Tanzania kwanza afu urudi kufanyia masahihisho uzi wako
 
Back
Top Bottom