Kitu ambacho ukijui labda nikupe elimu leo, Butiama ni kijiji, Nyerere hakutaka Ardhi ya Zanaki ipoteze asili yake, alijitahidi kwa akili kubwa kutunza asili kama Maasai.
Nimrod Mkono ni tajiri kitambo lakini alikuwa anakaa Nyumbani kwa baba yake Buswege, baada ya Nyerere kufa sasa Nimrod Mkono akashusha hekalu la nguvu Nyumbani kwake akahama kwa baba yake.
Nyerere angekuwa hai asingekubali Butiama kuwa wilaya, ni mtu hakutaka kabisa kuona Ardhi ya Zanaki inajengwa mahekaru.
Kitu cha msingi alichokifanya Butiama ni Kujenga hospitali ya wilaya kijijini Butiama na kanisa kubwa katoliki lilijengwa pale kitambo.
Musuguli na Butiku wote wanatoka Butiama ñilioneshwa Nyumbani zao ni za kawaida wote walimuogopa Nyerere, sijui kwa sasa kama wamefanya maajabu, hii ndio siri ya Michael ya Wazanaki kutowa wasomi na watu walioshika Madaraka makubwa lakini hakuna aliyewekeza kwao wa wala Kujenga maghorofa kama ya uchagani, mchawi wao ni Nyerere.