Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Status
Not open for further replies.
Mikopo ya muda mrefu lazima ile kwa mkopaji... Usidanganywe na makato.
Ni muhimu kukopa kwa muda mfupi mfupi...maumivu hayatakuwa makubwa sana.
 
Mkuu 250 imefikaje??? Mbona wengine ni 196, ambayo inaleta kama 14 hivi!!!!
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Wewe ndo hujui hesabu mkuu piga hivi
250000×12=3,000,000
3,000,000x6=18,000,000...
Hatari lakini salama
 
Nmb hawana wema hawa
Nilikwenda kuulizia 17 milioni wakaniambia
Makato 378000 kwa mwezi
Muda miaka 6
Bima ya mkopo 1.75%
Process fees1%
Nilichoka,
 
Labda huo ni mkopo kwa ajili ya wapita njia! Yenye maximum risk!
 
Reactions: Obe
ungechukua kwa muda mfupi may be miaka 4 au 3 kidogo ingepungua
 


...bank na mikopo ipo kwa ajili ya kumsaidia mtu/kampuni, tatizo hapa bado kuna uholela. Mabank ya kibiashara si sehemu nzuri sana kukopa kama unahitaji kujifanyia maendeleo binafsi. Mabenki ya ushirika (credit unions) na vicoba au ndugu, ni sehemu nzuri kukopa kwa ajili ya kujiendeleza (bila kuhusisha biashara)
 
Pigeni hesabu wana jf hapo
2014 nilikopa milioni 8
Wananikata 203000
Miaka5
Namaliza mwezi huu may
Sikopi tena,unataabika kudadadeki ,acha Tu
Kinachoniudhi hawa jamaa ni hizo charge zao
 
Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Umaskini hauishi kamwe.
usijekuta hiyo hela ulihonga kimada na nyingine ukafadhili msiba, pole sana,
 
Labda huo ni mkopo kwa ajili ya wapita njia! Yenye maximum risk!

.....tujipe faida ya dhahania, huyu ni mfanyakazi/mfanyabiashara na ana anuani kamili na dhamana kaweka, hii maximum risk ni sky high.

Kukosa sehemu tu ya mtaji, lakini kama akija mtu na mpango wa kuangalia kukopesheka kwa mtu basi wengi tutapata mikopo rahisi. NMB ni bank ya umma( govt ina hisa nyingi) kwa hiyo masuala ya kumnyonya mtu (ili kutoa gawio) hayana maana.
 
Hivi huwa hamuwaulizi wawape details za kutosha na ufafanuzi on payment terms kabla hamjaingoa mkataba? Majuto baada ya kuingizwa king hayasaidii
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…