KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Aah kwa hapo lazma mgongano wa maslahi utakuwepo.
 
Gardaworld Wana mfumo wanao uogopa... Unaitwa GardaWorld Ethics Hotline kupitia hicho kiunganisha chukua hayo maelezo Yako bila kupunguza ukali wa maneno nenda kayaandike kwenye system yao ya malalamiko ambayo yatafanyiwa kazi makao makuu ya gardaworld Kisha hao unao watuhumu watapokea order ya kurekebisha kero ulizo zifafanua.

System hiyo unaweza kutoa malalamiko Yako kwa kificho bila kutaja utambulisho wako

Ukiona hiyo system inakusumbua unaweza kupiga simu ya malalamiko ambayo itapokelewa moja kwa moja na uongozi wa juu nje ya mipaka ya TanzaniA namba yao ya simu ni 0800780005 namba hiyo ni ya Bure hata kama huna vocha

Hudumia hiyo ni ya kificho na Siri mno hakuna kiongozi wa garda ane penda wafanyakazi wa chini wafahamu njia hiyo...itumie uje unipe mrejesho.

Namba ya Bure ya malalamiko 0800780005

Mtandao wa kutuma malalamiko GardaWorld Ethics Hotline.​
 
Ushauri wa maana kabisa huu.
 
Kumbe Garda wababaishaji hivyo!? Ngoja tusubiri utetezi wao tupime maelezo ya pande zote.
 
Tafuteni mwandishi wa magazeti kama daily news mulipe wachapishe hiyo habari.
Ingawa binafsi yangu sijaona issue ya maana hasa ambayo ni burning ya kulaumu zaidi ya hiyo ya kufanya kikao kwa njia ya spika.
 
Huyu goodluck mtoto wa mwenye masai night club kinondonk kama ndio huyo atawasumbua sana.
Mtoto wa kinondoni vijana huyo halafu kasoma tena mtu wa mauzo halafu muhasibu.

Yeye kwa wazungu target yake wamempa ni kupunguza operating cost na ku maximize profit atawanyonya vibaya sana.
Na bado hajapiga mchekecho wa kwake. Jamaa anahamahama sana kazi ipo shida

Hata Ultimate wakati wa yule.mama mkaburu muisraeli alikiwa operations manager wafanyakazi walikuwa wanalipwa vizuri japi alikuwa katili sana yule mzungu.
 
Sasa SweetPain kama mpango wake ulikua huo si angesambaza link tu. Kuwjaza chumba kimoja na kuwapigia zoom ilimaanisha nn
Najibu Kwa vile umeninukuu japo ID uliyoiandika sio yangu Mkuu.

Nilikua naliwaza kijiwe tu kamanda, hakuna Cha online meeting hapo zaidi ya poor management and leadership. Hauwezi kuwaita watu waje kwenye mkutano na usitake kuonana nao, inatafsiriwa kama dharau.
 
Nyie wenzenu wanaenda kulala mpo nje mnakesha 😄
Ulinzi ni kazi ya Kiphaller sana aisee nilienda kuomba kazi control room pale G4S Nikaambiwa nianze na kulinda kwanza na nikapata training ya ulinzi na ilikuwa ni darasani kama chuo vile kwa miezi miwili. Sasa nikawa nimepangiwa Slip way Hotel yaani ili udumu kwenye kazi ya Ulinzi uwe mnafiki na uwe unajipendekeza sana kwa Ma supervisor, Zone Manager na Viongozi wengine. Aaah kitu hicho kilinishinda nilikuwa naburuzana nao sana kwa mwezi mara mbili napelekwa hearing nikifika hearing nawaburuza tu mpaka nikawa nawaambia tabia ya kunisumbua sumbua sitaki Wanafiki nyinyi nitawashitaki sasa. Duh waliniogopa mpaka wakawa wanajua Mimi ni GetiJeusi. Nikaamua kuachana nao. Yaani Tanzania hii Mlinzi anaonekana kama failure na hana option nyingine ya maisha. Kuna siku nitaanzisha uzi matukio niliyokuwa nakutakana nayo kwenye kazi ya Ulinzi. Tukio kubwa ambalo sitolisahau ni KUWARUHUSU CHURA WA YOMBO KUPIGA PICHA HOTELINI HALAFU WAKAANZA KUMWAGA RADHI MBELE YA WAZUNGU. HILI TUKIO SITOLISAHAU HALAFU WALIKIWA WAMENIPA 30,000. 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…