TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Ishu kwamba iyo kwenda kwao iko kwenye ratiba ya kikazi au aliamua tu ..

Nishaenda road trip nyingi za kikazi zninachojua watu wana mambo mengi sana .
 
Kama mtu ana akili long trip kwa barabara za Tz si salama ... Mkurugenzi anakuwa na hadhi ya juu sio kumuweka njiani masaa 10 ...Akipanda ndege hapo fasta tu.
Lakini inawezekana pia ratiba ilikuwa inamtaka kupita chini, kwa mfano ana ratiba ya Dodoma kwenda Singida baada ya hapo aende Shinyanga, then Simiyu na akitoka hapo aende Mara, kote huko hakuna ndege. Sasa unakuta anaamua kwenda na V8 ili aunganishe safari zote hizo kwa mara moja. Shida ni kwa dereva ambaye atakuwa na uchovu wa safari. Kwa mfano kama alikuwa anatoka Simiyu kwenda Musoma kwa nini hakuamua kulala hapo hapo Bariadi ili aanze safari asubuhi? Serikali haitaki kujifunza kwa nini wasizuie safari za usiku kwa magari ya serikali? Kwamba ikifika saa 12 jioni magari tote yasimame!
 
Umeyasema hayo kwakuwa ni yeye. Vip kuhusu mabasi yanayosafiri usiku??? Au kwako yale mabasi hayaendesgwi na binadamu?? Ajali haina kinga. Hata angepanda ndege ile anachukuliwa uwanjani kuelekea anakokwenda angekumbana nayo tu.
AJALI INA KINGA wachana na huu uswahili uswahili wa kusema ajali haina kinga. Na hii imedhibishwa kisayansi. Ajali nyingi ni man made i.e uzembe wetu. Ndiyo maana usafiri wa ndege uko safe sana kwa sababu wanachukuwa tahadhari kubwa.
 
Mkuu kwa gari ya Aina hiyo, umbali wa safari na majukumu ya anayeendeshwa ni hasara Sana kutembea mwendo mdogo.

Gari inamruhusu kukanyaga Moto, na Sheria za barabarani nazo haziwabani Sana watu wenye nyadhifa kubwa.
Huu ni uposhaji mwingine. Sheria za barabarani hazina mkubwa wala mdogo na zipo pale kwa manufaa ya wakubwa na wadogo.
 
Kwake sawa na Dereva je? Kama naye unamkurupusha tu basi ni hatari,ni bora hata kutafuta Dereva mwingine aliyejiandaa kwa wakati huo
 
Hii ndiyo njia sahihi lakini kwa namna viongozi wetu wanavyoongoza kuvunja sheria na taratibu haitawezekana.
 
Akili za.vijana wengi wa kitanzania ni za kipumbavu! Yanaweza hela tu! Yaani mkurugenzi wa tanesco awe na tamaa na vi perdiem kweli?
 
Au kama ilivyo barabara ya Ubungo mpaka Maili Moja Kibaha
 
Mchina akiongea kiswahil kikimpiga chenga mnaona poa ila mswahili akipigwa chenga nakizingu mnaona dhambi nan anawaroga nyie
Tena siku hizi watu wengi wanapozungumza kiswahili wanaweka dhafuli ya kizungu na kukosea maneno mengine kwa makusudi wakidhani ni ujanja. Mzungu akikosea kiswahili ni vizuri lakini mswahili akikosea kiingereza ni mshamba.
 
Hii ndiyo njia sahihi lakini kwa namna viongozi wetu wanavyoongoza kuvunja sheria na taratibu haitawezekana.
Ni shida sana! NGOs zenye heshima zake ni marufuku kuendesha gari zaidi ya saa 12 jioni. Ukitaka lazima upate kibali cha Country Director. Vinginevyo jiandae kulala njiani! Maisha ya Gissima yangeokolewa leo kama hizo sheria zingezingatiwa maana saa 12 ukute imemkuta yupo ama Shinyanga au Igunga hivyo angelala huko!
 
Ninashauri hata Saa100 na Nchimbi,wakianza kampeni October 2025, watumie chopa nchi nzima,kuepuka haya majanga ya barabarani
 
This high ranking officer are under president secret service hence once you leave your area of duty you mask make sure ume aga vizuri if not hilo ni somo la walio kwenye mfumo.. kwaheri
So haku aga ndio maana kapata ajali?
Sijaelewa umemaanisha kitu gani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…