Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 6,450
- 17,648
Babati hiyo tukapitwa fyuu na jamaa hawa wa misafad then Askari bila weredi anakuonyesha park park..dereva aligoma mpaka alipoona sehemu yenye nafuu akaweka gari pembeni.Hii misafara kwenye highways utafikiri tumejenga 8 lanes na moja niyakwao kumbe hamna Kila kitu matokeo yake kulazimisha watumiaji wengine wa barabara kupisha hata kama sehemu sio salama.
Unamlazimisha mtu kupisha msafara ilihali upande wakupisha kwa muda huo kuna korongo, wakati mwingine unapishana na msafara alfajiri na yake mataa huku na kule ni hatari aisee.
Tunamsingizia tu,kule Iringa treka imeharibika almoat siku nne ipo palepale tena pembeni kidogo..God has nothing to do with accidents.
Negligence is what causes accidents.
Hakuna tulipomkosea Mungu mpaka siku serikali itapo amaua kushughulikia made madereva wake wanaoendesha hovyo bila tahadhari.Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.
Duh 🙄 !Sasa wewe unafanya kazi ambayo CCM haitaki ikafanywa! Huo ni uchochezi.
Nakumbuka Serikali ilitoa miongozo kwamba viongozi wanapokuwa safarini ifikapo saa. 12 watafute sehemu salama wapaki.Ndio asafiri SAA nane ya usiku? Kuendesha Gari usiku ni hatari sana kwa dereva, abiria, chombo chenyewe na watumiaji wengine wa barabara.
Ndio maana kwenye taasisi zinazoongozwa na watu wenye akili wanakuwa na kitu kinaitwa journey management kabla ya kuanza safari yoyote.
Anaonyesha safari itaanza asubuhi ya SAA ngapi, mtapita njia ipi? Barabara mtakayoitumia ikoje? Mtakula wapi? Mtalala wapi? Etc.
Unapoendesha Gari kukiwa na mwanga wa Asili, dereva huona vizuri na akili inakuwa active.
Kuendesha SAA nane usiku ni hatari sana, boss kalala, dereva anaendesha huku kasinzia
Ajali zote zinasababishwa na uzembe na ujinga.Tunamsingizia tu,kule Iringa treka imeharibika almoat siku nne ipo palepale tena pembeni kidogo..
Katoka kijana huko na Brevis imewaka mbaya ,trekta hii hapa konani na kumebana na yale machuma..unafanyajd unaingia tu nyuma ya Treka..R.I.P
Mkuu upo sahihi sana ,usiku ni habari nyingine.Pia wengine hawana uwezo wa kuendesha safari ndefu sana
Binafsi mfano nina uwezo wa kuendesha safari ndefu masaa 14 mfululizo mchana bila kupumzika lakini maximum.mwisho saa mbili usiku
Ila huwa sili chakula kabisa nikila kikianza kusagika huwa nasikia usingizi wa hapa na pale Nashtuka gari inahama hama kwenye barabara sababu ya usingizi wa kustukiza
Nakuwa natumia tu maji ya kunywa kidogo kidogo ya moto sio baridi nikiendesha
Safari ndefu zaidi ya saa mbili usiku hata kama ya masaa sita hata niwe nimepumzika sitaki kuendesha Kuna kausingizi kakustukiza hapa na pale huhitaji madereva wazoefu hasa wa uendeshaji usiku
Hata marubani wa ndege huhitaji marubani wazoefu wenye night rating kubwa kuendesha ndege usiku
Supidi Kills wanaambiwa kila siku hawaelewi !Tunamsingizia tu,kule Iringa treka imeharibika almoat siku nne ipo palepale tena pembeni kidogo..
Katoka kijana huko na Brevis imewaka mbaya ,trekta hii hapa konani na kumebana na yale machuma..unafanyajd unaingia tu nyuma ya Treka..R.I.P
70% kwa bongo weka na Barabara sana ndio umaliza kila kitu.Ajali zote zinasababishwa na uzembe na ujinga.
Unavyojitisa ❌Hii lugha kwako ni pingu kadri unavyojitisa ndivyo inavyokubana
It is part of learning. As the saying goes "we learn through mistakes"
Kapumbavu wewe!Wakate umeme nusu siku kwa siku 14 kumuenzi mkurugenzi.
Mkuu, mbona unaiburunyua lugha nzuri ya Kiingereza?Unavyojitisa ❌
Unavyojitikisa ✅
Ulienda shuleni kusomea ujinga?
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Pengine tutapata nusra ya hii katakana umeme. Mungu amuweke anapostahili.Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva wake ambaye jina lake ni Muhajir Mohamed Haule, wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
View attachment 3302678View attachment 3302679
Picha hapa juu ni Muhajir Mohamed Haule, Dereva wa TANESCO wakati wa Uhai wake
Wapumzike kwa amani
"Tunayaangaza maisha yako"
TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180
TAARIFA KWA UMMA
TANZIA
Jumapili, 13 Aprili 2025.
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.
Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.
Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.
Imetolewa Na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA
WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA
====
MY TAKE
Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.
Hiyo ajali yake usiombe. Mtu anajikuta amezindukia jehanamu au firdausi.Tunamsingizia tu,kule Iringa treka imeharibika almoat siku nne ipo palepale tena pembeni kidogo..
Katoka kijana huko na Brevis imewaka mbaya ,trekta hii hapa konani na kumebana na yale machuma..unafanyajd unaingia tu nyuma ya Treka..R.I.P