TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Duh..masikini R.I.E.P..
Aisee nimesikitika sana...Nilimkubali sana.
Mwenyezi Mungu naomba Mpumzishe kwa amani.
Ila ninyi madereva wa serikali mna usenge sana ...mnamaliza viongozi jamani!
Washenzi sana...hivi kuajiriwa serikalini ndio kuwa juu ya sheria..you are so Stupid.
Sio madereva tu, Hata hao viongozi ni stupid vilevile.

Utakubalije kukimbizwa kama gazeti na wewe umekaa tu ume relax?

Au hao viongozi hawana mdomo wa kusema punguza mwendo?
 
Hakuna
Sidhani kama mnatenda haki mkisema hivyo. Watu wasio wakurugenzi ndiyo wenye haki ya kusafiri kwa magari na kupata ajali? Jambo la msingi ni kudai barabara zetu zijengwe kwa viwango na madereva na magari yawe ya viwango.
Hakuna Cha kujengwa Kwa viwango, barabara zipo vizuri ni kiburi tuu Cha madereva wa magari ya serkali pamoja na maboss zao, wanajionaga wakiwa barabarani kama vile ni Mali ya baba au mama zao kiburi Cha mavyeo Yao tuu,

Huwa wanakimbiza na kuendesha Kwa rafu sana, mfano ni misafara ya viongozi wakiwa wanapita mabarabarani gari zinakimbizwa as if Kuna mashindano, kiasi kwamba ikipata ajali gari moja zote zinakuwa chapati.

Haya ni mafunzo Kwa wengine, waache viburi na kujiskia, waheshim Sheria za barabarani wasione nchi hii kama ya baba au mama yao, wakumbuke Kuna kifo.
 
Sio madereva tu, Hata hao viongozi ni stupid vilevile.

Utakubalije kukimbizwa kama gazeti na wewe umekaa tu ume relax?

Au hao viongozi hawana mdomo wa kusema punguza mwendo?
Viburu vya tumbo kushiba na uwezo wa kurefusha kamba
 
Kifo ni kifo tu alisikika mheshima mmoja baada ya Ally.Kibao kufariki. Mungu uwaangazie mwanga wa milele na uwape stahiki dhao kwa matendo yao
 
Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva wake ambaye jina lake ni Muhajir Mohamed Haule, wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
View attachment 3302678View attachment 3302679
Picha hapa juu ni Muhajir Mohamed Haule, Dereva wa TANESCO wakati wa Uhai wake

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

R.I.P Home boy.
 
Mchina akiongea kiswahili na kukosea ni sawa kwa sababu hana option pale anapokuwa Tz. Sasa huyu ndugu yetu ana ulazima gani wa kutumia lugha inayompiga chenga wakati kuna kiswahili?
Atasema steshen zote za redio na television nchini zina majina mengi ya vipindi kwa lugha hiyo
 
Latra hawarusu basi la masafa marefu kusafiri kama halina madereva wawili.
Sheria ndivyo inavyosema. Je utekelezaji wake ukoje?? Usanii mtupu. Ukisafiri toka point A kwenda B na ukafika salama mshukuru sana Muumba wako.
 
Hakuna

Hakuna Cha kujengwa Kwa viwango, barabara zipo vizuri ni kiburi tuu Cha madereva wa magari ya serkali pamoja na maboss zao, wanajionaga wakiwa barabarani kama vile ni Mali ya baba au mama zao kiburi Cha mavyeo Yao tuu,

Huwa wanakimbiza na kuendesha Kwa rafu sana, mfano ni misafara ya viongozi wakiwa wanapita mabarabarani gari zinakimbizwa as if Kuna mashindano, kiasi kwamba ikipata ajali gari moja zote zinakuwa chapati.

Haya ni mafunzo Kwa wengine, waache viburi na kujiskia, waheshim Sheria za barabarani wasione nchi hii kama ya baba au mama yao, wakumbuke Kuna kifo.
Sikatai kuwa Tanzania uendeshaji ni mbovu sana na tena siyo kwa magari ya serikali tu bali ni asilimia kubwa ya madereva. Lakini kama unasema barabara zetu zina viwango vya kutosha, well, pengine siyo kosa lako kwani inawezekana hujaona barabara kuu za nchi zilizoendelea. Hata mimi nilipokuwa mdogo kijijini kwetu huko, nilikuwa nadhani wali kwa kuku ndicho chakula cha kifahari na ghali duniani kote.
 
nani anajua siku yake ya kufa? Kama kuna mtu hapa aniambie,lakini kama hakuna mtu ajuaye siku yake ya kufa basi hata MKURUGENZI wa TANESCO hakujua siku na kisababishi cha kifo chake.

kifo ni kifo tu,tutabaki kulaumiana tu badala ya kumshukuru MUNGU kwa maisha ya gissima hapa duniani.

Hata wewe ukifa mkuu,watu watalaumu tu,lakini licha ya lawama zao haiwezi kusaidia kitu.

AHSANTE MUNGU KWA KUMLETA DUNIANI MR. GISSIMA,AMETENDA YOTE ULIYOMTUMA SASA ANARUDI KWAKO. wanadamu tu mavumbi,na mavumbini tutarudi.

MWENYEZI MUNGU ipumuzishe roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.
Useless explanation! Kama umewahi kusoma kitabu cha Kusadikika cha Shaaban Robert basi utakuwa ulikutakana na watu wanaoitwa wasadikika ambao waliishi miaka mingi iliyopita, na walikuwa na mawazo kama yako. Kama hujui siku ya kufa ndiyo usichukuwe tahadhari na kufuata kanuni za maisha salama? Mbona ukiugua unakimbilia hospital?
 
Back
Top Bottom